Utafiti: Kukosa usingizi wa kutosha hupelekea kupungua kwa Nguvu za Kiume

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
KUKOSA usingizi wa kutosha kunaweza kusababisha kufifia kwa nguvu za kiume.

Madaktari wanasema kuwa mwanaume anachukuliwa kuwa amepata usingizi wa kutosha usiku iwapo atalala kwa kati ya saa saba na tisa. Hata hivyo, watu wengi huwa hawazingatii muda huo kutokana na aina ya kazi wanazofanya au shughuli nyingine za kutafuta riziki.

Utafiti uliofanyiwa wanaume 2,676 wa zaidi ya umri wa miaka 67 nchini Amerika, ulibaini kuwa wale ambao hukosa usingizi wa kutosha hukumbwa na changamoto ya upungufu wa nguvu za kiume.

“Utafiti umeonyesha kuwa kukosa usingizi wa kutosha kunapunguza uzalishaji wa mbegu za kiume kwa mwanaume na hilo linachangia kukosekana kwa hamu ya mapenzi na pia ashiki wakati wa tendo la ndoa.

Utafiti huo huo unaonyesha pia kupungua kwa mbegu za kiume pia kunasababisha ukosefu wa usingizi,” ilisema ripoti ya utafiti huo.

Ukosefu wa usingizi wa kutosha pia hupunguza kinga mwilini na kusababisha iwe rahisi mwanaume kukumbwa na magonjwa kama shinikizo la damu, ugonjwa wa sukari na unene.

“Asilimia 20 ya vijana kuna uwezekano mkubwa wamepungukiwa na mbegu za kiume kutokana na shughuli za kutafuta riziki,” akasema Mtaalamu Karen Rowan kutoka Uingereza kwenye jarida linalochapisha habari za afya, LiveScience.

Kwa hivyo, wale ambao hulala chini ya muda wa saa sita utafiti umeonyesha wanaweza kuwatungisha wapenzi wao mimba kwa asilimia 31 huku wale waliolala kwa muda wa saa tisa zaidi wakiwa na asilimia 49.

Chanzo: Taifaleo.ke
 
Ni mtego huo ili wanaume waanze kulala alafu wakose pesa wasipewe mbunye tupinge usingizi kwa nguvu zote au nasema uongo ndugu zanguni ?
 
Ni kweli kabisa sababu hata Hormones imbalance husababishwa na kukosekana kwa usingizi ambapo huchochea testosterones hormone kutoratibu vizuri gametiume na Me kukosa kushawishika/kuvutiwa kihisia kabisa na kujamiiana na Ke sababu hakuna genye za kutosha kwenye korodani.

Pia huenda baada ya raundi 1 tu ndiyo ikawa baibai kutorudia nyingine.
 
HAWA WATAFITI NAO WAMEZIDI, MARA CHAKULA, MARA USINGIZI, MARA MAZOEZI.. YAANI VURUGU VURUGU

SAWA TUTALALA SAA 6-8 KWA SIKU
 
Kama NI nguvu za kiume alooo nipo tayari kulala saa 2 na nusu usiku na kuamka saa moja kamili asbh
Ndugu yangu kukosa usingizi ni kukosa hela tuu. Una hela unakosaje usingizi. Hizi tafuti zingine hazinaga mbele wa nyuma kama mche wa sabuni tuu.
 
Ndugu yangu kukosa usingizi ni kukosa hela tuu. Una hela unakosaje usingizi. Hizi tafuti zingine hazinaga mbele wa nyuma kama mche wa sabuni tuu.
Mimi nikiwa na hela ndo nakosa usingizi maana Lazima nikaveshe k vant mpk saa Saba ila nikiwa Sina mapema TU hata taarifa ya habari haipandi nalala saa tatu
 
Mimi nikiwa na hela ndo nakosa usingizi maana Lazima nikaveshe k vant mpk saa Saba ila nikiwa Sina mapema TU hata taarifa ya habari haipandi nalala saa tatu
Dah tupo complete opposite. Mie nikiwa na hela hapo ni kugegeda mrembo then nauchapa usingizi safi kabisa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom