Wilson Gamba
JF-Expert Member
- Mar 1, 2013
- 820
- 917
Habari za siku wana jamvi,
Nimekuwa kimya muda mrefu hii ni kwa sababu ya majukumu yaliyokuwa yamenibana.Tumekuwa tukishudia au watu kuleta mada hapa juu ya kuumizwa au kutotimiziwa mambo muhimu katika ndoa au dharau katika ndoa au kuumizwa kwa vigezo vya fedha au mafanikio ya mtu kifedha.
Aliyeko kwenye ndoa na hii kupelekea ndoa nyingi za watu kuwa katika hali mizozo mikubwa. Nakuja na ombi kwenu nina mchakato wa kuanza utafiti juu ya kwanini wasomi wengi kwa sasa hawaoani uthamani wa kuoa au kuolewa.
Kama itaungwa mkono ifanyike, maswali dodoso yatawekwa hapa na taarifa zote zitakusanywa kwa umakini kwa ajili ya kufanyia utafiti. Idadi ya njia zote za kupata takwimu zitakuwa mbili mahojiano pamoja na maswali dodoso yatakayowekwa hapa na kisha kutumwa kwa email itakayotumika kwa kazi hii.
Tafadhali hii itafanyika tu kama idadi ya waunga mkono itakuwa kubwa. Pia repoti ya utafiti itawekwa hapa kuweza kuisaidia jamii kuipitia kwa lengo la kuisaidia jamii yetu katika kuishi na kulea familia zao kwa amani na kuwa mfano bora kwa jamii ya kitanzania.
Mungu awabariki