Utafiti: Akili inanywea kuanzia miaka 40

Sizinga

Platinum Member
Oct 30, 2007
9,101
6,027
Utafiti uliofanywa na vituo bingwa duniani unaonyesha kuwa watu wengi akili(brain) inaanza kupwaya pindi unapofikia miaka 40 na kuendelea. Hii imeushangaza ulimwengu ukioamini kwamba akili ya mtu inapwaya kuanzia miaka 60. Utafiti huu unaonesha kumbukumbu za mtu afikapo miaka 40 zinapungua kwa kadri miaka inavyoongeza 40+, Hii ilijumuisha idadi ya watu 7000, ambao walifanyiwa research na watu wenye aged 40 mpaka 49 ndio walionyesha wanapoteza kumbukumbu zaidi. SOURCE: GAZETI LA KISWAHILI MWANANCHI(Kama sijakosea) MY TAKE: Hapa Tanzania kwa system yetu ya elimu inaonesha watu wengi wenye umri kati ya 15-30, wapo masomoni(mostly 1st degree). Wengi wanaanza kulitumikia Taifa kuanzia miaka 30+ either kuajiliwa au kujiajili...so kuna miaka 10 tu inayobaki wakati akili bado iko fresh ya kulitumikia taifa hili. Hii ni hatari sana kwani kuanzia miaka 40+ na kwa maisha haya ya sasa yenye stress inaonesha kabisa tunapiga hatua 5 mbele na 10 tunarudi nyuma. Je kweli Tutafika??
 
Ukishangaa ya Musa utaona ya Firauni
Umeona taarifa ya jana kile kibabu kilichoapishwa ikulu
Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi, hata kuonahaoni

It was the shameful thing ever seen tangu huu mwaka uanze.
 
mmmh,sasa mimi ndio najiandaa nikalambe Phd Itakuwaje jamani,maana umri wangu umevuka hapo sasa nina 43 mbona watafiti wananikatisha tamaaa
 
Kuna utafiti mwingine uliodai kuwa Nyuki kwa jinsi maumbile yake yalivyo hawezi kupaa. Watafiti walidai kuwa umbo la nyuki, uzito wake na kasi ya mabawa yake hayamruhusu kupaa kabisa.
Bahati nzuri Nyuki huwa hasomi tafiti, hivyo anapiga zake mabawa na kupaa kama kawaida, tena kwa spidi nzuri tu. Na matokeo yake tunakula asali inayosaidia kujenga afya zetu (naam hata tukiwa na miaka 60).
Ukisikiliza tafiti utaogopa hata kutoka nje ya nyumba yako asubuhi.
By the way, life starts at 40 ... Now this is a fact!
 
NAKUBALIANA NA WEWE JAPO SIO LAZIMA TAFITI HIYO ILIYOFANYWA HUKO KWA WAZUNGU IWE APPLICABLE NA HUKU KWETU AFRICA. Labda kama watafanya utafiti na huku kwetu africa kuthibitisha hilo.
 
sikubaliani na hili kabisa'mimi mbona ni 40 na najihisi iko fresh kuliko nilivyokuwa 30?labda watoe ufafanuzi wa kutosha au waeleze kwa undani inanywea vipi
 
Yaani ni kweli twafwa!! manake haiingii akilini mtu mpaka 30+ bado una vibahasha mkononi kutafuta ajira...bongo bana
 
Hivi kwa mujibu wa Katiba ya JMT (1977) Mgombea U-Rais wa JMT anapaswa kuwa na umri gani?
 
possible kwa baadhi ya watu. Haimaanishi wa2 wote, mi naamini wengine wakireach 40 ndo kwanza akili zinazidi. Na km imekusudiwa kupoteza kumbukumbu (sahau) hayo ni maradhi hata mtt wa miaka 17 anaweza kua nayo.
 
Kasema watu wengi, siyo wote. Kwa hiyo mi sikatai wala sikubali kwani as a scientist, I need some proof!!
 
Kuna kitu kinaitwa associated factors kwenye medicine. Hivi ni visababu vinavyoweza kupelekea tatizo,ingawa kuwepo au kutokuwepo hakumaanishi moja kwa moja mtu yuko unsafe au safe:
km
>sigara ni a/factor ya saratani ya mapafu.
>unene/obesity ni a/factor ya high bp.
>kuzaa sana (grandmultiparity)ni a/factor ya saratani ya kizazi.
>kutokuzaa ni a/factor ya uvimbe wa tumbo(fibroid).


BACK TO THE TOPIC MTOA MADA TUELEZE HIYO NI DIRECT FACTOR AU ASSOCIATED FACTOR,AND HOW?!
... No evidency No permission to speak !!!
 
Unapofikia umri huo akili ndiyo inafikia full capacity ila mwili una anza kuchoka from abuse of your activities. Akili na busara zinaongezeka kutokana na knowlage ulio acumulate. Akili ita anza kuchoka na kupoteza kumbu kumbu kuanzia miaka 60 na kuendelea isipokuwa kama una ugua maradhi ya elxehmer.
MIAKA 40 NI MTU ANAEANZA KUWA NA BUSARA
 
Back
Top Bottom