Utabiri Wa Wakati Ujao

Mtayarishaji

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
291
199
Je, umewahi kujiuliza maisha yako na ya familia yako yatakuwaje wakati ujao?

Je, unafikiri utapata ufanisi, au utakumbwa na umaskini?

Je, utapata watu wanaokupenda, au utakuwa mpweke?

Je, utaishi muda mrefu, au maisha yako yatakatika ghafla?

Wanadamu wamejiuliza maswali hayo kwa maelfu ya miaka.




Leo, wataalamu huchunguza jinsi hali zinavyoendelea duniani na kutumia habari hizo kutabiri mambo yatakavyokuwa. Ingawa baadhi ya mambo wanayotabiri hutokea, mengine huwa kinyume kabisa na matarajio yao.

Kwa mfano, katika mwaka wa 1912, Guglielmo Marconi, mvumbuzi wa teknolojia ya kurusha mawimbi hewani bila kutumia nyaya alitabiri hivi: “Enzi mpya inayokuja ya kurusha mawimbi bila kutumia nyaya, itakomesha vita.” Na ajenti wa kampuni fulani ya kurekodi ( Decca Record Company), ambaye aliwagomea wanamuziki wa kikundi cha
the Beatles katika mwaka wa 1962, aliamini kwamba vikundi vya kucheza gitaa vilikuwa vinaelekea mwisho wake.

Watu wengi hugeukia wale wanaowasiliana na roho ili kutafuta habari kuhusu wakati ujao. Baadhi yao hutafuta ushauri kutoka kwa wanajimu, na makala za utabiri wa nyota zinapatikana kwa ukawaida kwenye magazeti mengi. Wengine nao hutafuta habari kwa wabashiri wanaodai kwamba wanaweza “kujua” wakati ujao wa mtu kwa kusoma kadi za kubashiri, namba, au alama za viganja vya mikono.

Wakiwa na hamu ya kujua mambo yangekuwaje baadaye, baadhi ya watu walioishi nyakati za kale walienda kwa waaguzi, wa kiume au wa kike, ambao waliwapatia habari kutoka kwa miungu waliyodai kuiwakilisha.

Kwa mfano, inasemekana kwamba Mfalme Croesus wa Lydia alituma zawadi zenye thamani kubwa kwa mwaguzi aliyeishi Delphi, Ugiriki, na kumwomba amweleze matokeo yangekuwaje ikiwa atapigana na Koreshi wa Uajemi. Mwaguzi huyo alisema kwamba Croesus akienda kupigana na Koreshi, “milki kubwa” itaangushwa. Croesus alienda vitani akiwa na uhakika kwamba angeshinda vita hiyo, lakini kwa kusikitisha milki yake kubwa ndiyo iliyoanguka!

Utabiri huo haukuwa na maana yoyote kwa sababu ungeonekana kuwa wa kweli bila kujali ni nani ambaye angeshinda vita hiyo. Croesus alipoteza kila kitu kwa sababu ya kutegemea habari za uwongo.



Je, wale wanaotumia njia za kisasa ili kujua kuhusu wakati wao ujao, wamepata mafanikio yoyote?
 
Back
Top Bottom