Etwege
JF-Expert Member
- Jul 4, 2018
- 7,380
- 18,175
Balozi Humphrey Polepole kabla ya kutekwa na kupotezwa alitabiri mambo mengi kwa nchi yetu Tanzania ikiwa itaendelea kuwa chini Rais Samia (2025-2030). Leo nawaletea tabiri mbili tu ambazo nimeona zimeanza kuonekana dhahiri.
Rais Samia kutowaheshimu watanzania baada ya uchaguzi mkuu
Humphrey Polepole alionya kuwa ikiwa Rais Samia atalazimisha uchaguzi na kujipitisha kuwa Rais ,basi baada ya hapo hatawaheshimu na wala hatawasemea watanzania shida zao.
Ni kweli baada ya October 2025 Rais Samia anaonekana dhahiri hayuko upande wa watanzania hasa watanzania wanyonge! Wamachinga wanafukuzwa, bei za bidhaa na mafuta zinapanda hovyo hovyo lakini Rais Samia yuko kimya na hata akiongea anatetea hali hiyo bila kujali inavyoathiri maisha ya wananchi wake.
Rais Samia kukosa uhalali kisiasa
Balozi Polepole alionya mapema sana kuwa Rais Samia alitakiwa uongozi wake kuishia 2025 na kama atalazimisha kwenda zaidi ya hapo basi atakosa uhalali kisiasa kutoka ndani ya nchi na nje ya nchi.
Utabiri huu umetimia kwa haraka sana, Rais Samia hakubaliki nje ya nchi ndiyo maana hajafanya ziara yoyote Ulaya mpaka sasa. Kutoka ndani ya nchi Rais Samia utawala wake umepuuzwa kuanzia kijijini hadi mjini.