Utabiri wa Bibi Titi: Historia ya Uhuru wa Tanganyika Itaandikwa

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,921
30,264
UTABIRI WA BIBI TITI MOHAMED: HISTORIA YA UHURU ITAANDIKWA NA WATU AMBAO HATA HAMTAWATEGEMEA

Bibi Titi alipata kumwambia mjukuu wake Omari Mzee Kitenge kuwa historia yake itakuja kuandikwa hata kama yeye atakuwa hayuko duniani.

Baada ya kumaliza ratiba ya mchana leo siku ya tano ya Bibi Titi Festival tukatangaziwa kuwa tusiondoke hapo uwanjani tusubiri chakula na kwa hakika nilipokuwa naangalia muda nikajua ni chakula cha jioni tunakaribishwa.

Jua lilikuwa linaanza kubadili rangi yake na kujiinamia kuamza kuzama.

Jicho langu likaenda kwenye ule umati wa watu walifurika katika Uwanja wa Ujamaa nikajiuliza umma huu wote kweli utaweza kupata chakula?

Wake kwa waume na watoto.

Kama vile Mshehereshaji kasikia shaka yangu akatangaza kuwa tusitie hofu tutulie chakula kipo cha kutosha pamoja na maji na juisi.

Nikashusha roho.

Naiuliza nafsi yangu huyu Bibi Titi ana nini jamani?

Shughuli yake imekuwa kula kwa Mfalme kulala kwa Mfalme?

Mwenyekiti wa UWT Mary Chatanda katika hotuba yake ametangaza kuwa itajengwa Maktaba ya Bibi Titi Dodoma ambayo itahifadhi historia yake na ya wanawake wengine walioigania uhuru wa Tanganyika.

Hii maana yake ni kuwa Bibi Titi historia yake itahifadhiwa na wenzake aliokuwanao: Tatu bint Mzee, Chiku bint Said Kisusa, Hawa Bint Mafatah, Halima Khamis, Shariffa bint Mzee, Fatma Matola, Halima Selengia, Amina KInabo, Lucy Lameck, Mama bint Mwalimu, Zarula bint Abdulrahman, Nyange bint Chande, Mama Boi, Biti Farahani, Biti Kaijage, Biti Sheikh, Biti Saliboko, orodha itakuwa ndefu maana kuna wengi hawafahamiki kwa sasa.

Hakika aliyepewa hapokonyeki.

Maktaba ya Bibi Titi itakayoweka kumbukumbu zake na za wanawake wengine waliopigania uhuru wa Tanganyika akili wakati mwingine hukataa kuamini masikio yake yenyewe.
Kwa vigezo vyote hili ni jambo kubwa na la kihistoria.

1701547561629.jpeg
 
Hili jambo jema sana kuwatambua na kuwaenzi wote walio jitolea hali na mali kwa kupigania uhuru wa nchi hii ambao leo tunaufaidi.
 
Miaka kadhaa iliyopita niliwahi kuwaza kutengeneza tisheti za bibi titi kama ilivyo za che guevara.Historia ya bibi titi huwa inahuzunisha namna alivyoishia. Lakini alikuwa mwanaharakati mwenye uthubutu haswa.

Niliwahi juwaza matukio kama haya kwa bibi Titi, nafurahi yanatokea japo tumechelewa. Bibi Titi alikuwa mwanamke wa shoka si kidogo.

Sent from my SM-A225F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom