Bibi Titi: Mlango Alioufungua Wamepita Wanawake Hesabu Yake Haifahamiki

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,922
30,271
BIBI TITI FESTIVAL IKWIRIRI RUFIJI: MLANGO ALIOFUNGUA BIBI TITI UMEPITWA NA WANAWAKE IDADI YAO HAINA HESABU

Aliyepewa hapokonyeki.
Bibi Titi kawika alipokuwa hai.

Bibi Titi anawika akiwa kaburini.

Niko mbele basi dogo limewabeba vijana wa kike na wa kiume tunaelekea Ikwiriri, Rufiji kwenye Bibi Titi Festival 2023.

Namshukuru sana rafiki yangu Haruna Mbeyu yeye kwa kutambua mapenzi yangu ya historia ndiye aliyenileta mwaka jana katika Bibi Titi Festival.

Namshukuru sana.

Basi lilikuwa kimya hadi tulipolipa mgongo Jiji la Dar-es-Salaam hapo ndipo ile hali na "mood" ya Bibi Titi Festival ikaanza.

Nyimbo moja baada ya nyingine.
Kisha ghafla ikaambwa nyimbo ya Bibi Titi.

Nyimbo za siku hizi zote ni "Long Play," yaani nyimbo ndefu si zile za zamani za dakika mbili na tatu.

Mashairi ya nyimbo yana beti nyingi na ndefu.
Mwimbo huu ulikuwa wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Kwanza ndivyo nilivyosmini.

Ghafla 'melody" imebadilika halikadhalika na beti zimegeuka nasikia kibwagizo na mashairi yanamtaja Bibi Titi kwa sifa kubwa kubwa waimbaji wakipokezana kusifia kwa mashairi ya kupendeza.

Nyimbo ni historia nzima ya mwanamke wa aliyekuwa nyuma akiuangalia mgongo wa mwaname akimfuata mwanamme nyuma aliyemtangulia mbele.

Nyimbo hizi zina vionjo vya midundo ya asili lakini ala zinazopigwa ni pamoja "Moog Sythesizer," na "Electric Drums."

Vibwagizo vinavyoimbwa na ala zinavyopigwa kama vile wanahanikiza dunia nzima kwa hamaki na uchungu.

Muziki uko kati ya Rap na nini sijui.
"Nani aliyesema wanawake mahali pao jikoni na uani?"

"Bibi Titi kaonyesha njia sote tukaanza kupita na kupika hatakuacha wala kuteka maji kisimani."

Maneno mengi.
Huyu anaimba mwenzake anapokea kwa Rap.

Anaingizwa Mama Samia kwa shangwe.
Rais, Rais, Rais...

Nyimbo nzuri inasisimua.

Nimekaa kwenye kiti nawaza namna muziki ulivyobadilika.
Bibi Titi alikuwa mwimbaji katika ujana wake sana.

Akiimba na Egyptian kundi maarufu la taarab enzi hizo.
Muziki wa enzi zile ulikuwa baridi sana hakuna midundo.

Nimeinamisha kichwa changu namuwaza Bi. Titi akiimba na Egyptian na fidla za Egyptian zinazopigwa kwa utulivu na wasikilizaji wako juu ya viti wanatikisika.

Namuwaza na Nuru Bint Sudi na nyimbo yake, "UTP Wana Majambo TANU Wanaichukia."

Huu ni mwaka wa 1957.
Nikamkumbuka marehemu Leila Sheikh kipenzi cha Bibi Titi.

Siku moja alinihadithia Bibi Titi alivyoimba "duet," na Siti Bint Saad Zanzibar nyumbani kwa Said Soud.

Siku hiyo walikuwa nyumbani kwa Said Soud miaka ya mwanzo kabisa 1950.

Walioalikwa ni ni vijana "ehe" wa Kizanzibari.
Bibi Titi alikuwa kafuatana na mumuwe Humud ndiyo kwanza wameoana.

Leila kanihadithia anasema Bibi Titi akimtaja kwa mapenzi makubwa akisema alikuwa na sura jamil.

Siti bint Saada alikuwapo akitumbuiza.
Siti bint Saad akaimba nyimbo moja ikipendwa sana wakati huo.

Watu wametulia wanasikiliza.

Siti bint Saad akaimba alipofika kati anaingia beti za mwisho yeye, akimjua Titi ni mwimbaji mwenzake akampa ishara amalizie nyimbo ile beti za kumalizia.

Bibi Titi anamwambia Mwanleila kama mwenyewe alivyokuwa akipenda kumwita Leila Sheikh, "Mwanlela hukuwepo lakini malaika wako walikuwapo.

Nilimpokea Al Nisaa.''

Nawaza najiambia tofauti iliyopo baina ya muziki ule walioimba Siti bint Saad, Nuru Bint Sudi na huu ninaousikia leo vijana wanaimba kumtukuza Bibi Titi kwa yale makubwa aliyoyafanya katika maisha yake akipigania uhuru wa Tanganyika.

Nimezungumza na baadhi yao vijana hawa hakuna hata mmoja aliyepata kumuona Bibi Titi.

Wanaijua historia yake kijuujuu.

Bibi Titi kamwachia marehemu Leila Sheikh historia yake yote ya maisha yake kwa sauti yake na kwa picha za video.

Bibi Titi katuachia historia ya maisha yake kama vile alinyanyua kalamu kuandika.

Leila amefariki kabla ya hata kuanza kuandika maisha ya bibi yake.
Lakini kila kitu kipo.

Waandaaji wa Bibi Titi wa Festival waliangalie hili.

Bibi Titi katika uhai wake alikijenga chama cha TANU kwa kuwaleta watu kuwa wamoja wameungana kupigania uhuru wao.

Leo uwanja umepanuka zaidi jina la Bibi Titi linaweza likatumika kwa maslahi ya jamii yaliyo makubwa zaidi ya tunavyoweza kufikiri.

Kwa juma Zima hili Ikwiriri imefurika watu.
Kila mwenye biashara yake ikifika usiku anahesabu faida.

Lakini wanaonufaika zaidi ni wanasiasa.

Kwa hili wanasiasa wana deni kubwa kwa Bibi Titi mwenyewe na kwa Tanzania nzima.

Deni hili lazima lilipwe.
Tujenge umoja wa Watanzania wote kupitia hii Bibi Titi Festival.

1701472648443.jpeg

Mh. Mchengerwa kati akiwa na Omar kuliani kwake mjukuu wa Bibi Titi
1701472709050.jpeg

1701472842507.jpeg

1701472890472.jpeg
 
Mh Mchengerwa pia ni mjukuu wa Bibi Titi Mohamed.
 
Back
Top Bottom