Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,014
- 144,371
Tangu sheria inayohusu maliasili za gesi na madini kufanyiwa marekebisho na serikali na kisha kupitishwa na Bunge,kumekuwa na madai mbalimbali yakiwemo malalamiko kutoka kwa wadau mbalimbali wa sekta hiyo yakiwemo makampuni ya utafutaji na uchimbaji wa madini na gesi.
Kuna madai pia kuwa baadhi ya makampuni yamesitisha shughuli zake ingawa pia ziko taarifa kuwa kuna makampuni mengine mapya yanaomba leseni za kufanya hizo zinazohusiana na uchimbaji na utafutai wa madini ama gesi.
Binafsi naona ni swala la muda tu kabla hatujalazimika kuirudisha tena Bungeni sheria husika ili ifanyiwe marekebisho kuondoa hii sintofahamu as long as madai/ taarifa hizi tunazosika na kuzisoma ni za kweli.
Sijui na siamini kama tumejianda na yatakayokuwa matokeo ya kubadili sheria hizi maana kila uamuzi una gharama zake.
Muda utaongea.