Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,034
- 144,388
Napenda kumshauri na kumsihi naibu katibu mkuu wa CCM bara,mh.Mwigulu Nchemba,kuwa awe makini na aina ya siasa anazoziendesha.Anapaswa kutokujisahau,kutokulewa madaraka na kusoma alama za nyakati.
Jambo analopawsa kutambua kuwa CCM ni chama cha kisiasa na yeye kapewa nafasi hiyo wakiamini atakisaidia chama kukabiliana na siasa za ushindani.Anapaswa pia kutambua hali mbaya inayokikabili chama chake na kujiuliza endapo atafanya siasa za kukigharimu chama nani ataendelea kumvumilia?Nina uhakika si wote ndani ya CCM wanaridhika na siasa za sasa za Mwigulu Nchemba.
Kitu anachotakiwa kutambua kuwa CCM siku zote huangalia upepo wa kisiasa unakwendaje na kuweza kuchukua maamuzi yoyote ikiwa ni pamoja na kumtoa mtu kafara.Yeye mwenyewe teyari ameshaonyesha hali hii kwa kumgeuka waziri wa maliasili na utalii,mh kagasheki,baada ya kuona hali ya kisiasa kwa CCM ni mbaya huko Loliondo.Wamempinga Kagasheki wazi wazi kama vile sio mwenzao.Hata wale waliotakiwa kujivua gamba nao chama kiliamua kuwageuka tu ili kujisafisha mbele ya umma.kilichowaokoa kila mtu anakijua.
Huko Loliondo analaumiwa kufukuza waandishi wa habari,kesi ya Lwakatare anatajwa yeye,mikutano ya vurugu,mauji n.k jina lake lipo! Vurugu bungeni yeye na mambo mengine mengine.Yote haya ni hatari kwa chama chake.
Mwigulu Nchemba,pamoja na kusifiwa na mwenyekiti wako,bado hao hao wanaokusifu wanaweza wakakugeuka.Hawakawii kukwambia mwenzetu naona utupishe kwani mwenendo wako unaharibu jina la chama.Kama nilivyokwambia hapo awali,waliotakiwa kuvuliwa magamba ni mfano mzuri kwani baada ya kuonekana wao ndio wanaharibu "image" ya chama wakawataka wajiuuzulu nafasi zao ili kukinusuru chama.Unapaswa ujiulize, kama wale jamaa walitakiwa kujiuzulu,wewe je itashindikana nini?
Leo wanaweza wakakutuma,kesho wakakugeuka!