Utabiri: Kuna Mawaziri wa serikali hii wataanza kujiengua wenyewe kwenye nafasi zao

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,970
Kwa mwendo wa kubana matumizi, kuepuka ulevi na kuzuiwa safari za nje zisizo na tija kwa taifa binafsi naona kuna mawaziri mwendo huu ni ngumu mno kwao! Kwa sasa wanataabika sana, exposure kwao imekua adimu kwa mambo yao binafsi. Nikionacho tuendako mbeleni kuna watu watazikimbia ofisi, wataomba wenyewe kuachia ngazi.

Kwa utawala uliopita kuna mawaziri walikua wakitumia muda mfupi sana ndani ya nchi, wengine walihamishia ofisi zao hotelini! Wengine walijitaftia hata pesa za kugombea urais kwa exposure walizokua nazo nje ya nchi. Sasa kwa mwendo huu wa kuwalazimisha wale mihogo waliozoea Pizza ni mtihani mgumu mno kwao. Ofisi kwa sasa zinaonekana ni kama za moto hivi.

Kwa hili nisiwe mnafki au mchoyo wa fadhila kumpongeza Mh Rais, acha waliozoea Pizza nao waonje uchngu na utamu wa mihogo!Asiyetaka akae pembeni awapishe waliozoea mihogo.
 
Mkuu hili naliona pia, ila sio mawaziri tuu, kuna makatibu na watu wengine nyeti " the untouchables " wataachia ngazi
 
Waondoke tujenge nchi yetu..ningeruhusiwa ningeshauri wepi waondoke....kule Pwani samaki mmoja akioza..huozesha wote.
 
Mkuu kumbe wewe ni mtabiri?, kuna mtabiri mwingine kule Arusha amepata matatizo
 
Wengine wataachia ngazi kulinda heshima zao dhidi ya udhalilishaji.....heshima kitu cha muhimu hata kama wewe ni bosi.

Yaan unitukane kisa uwaziri hehehehee
 
UKAWA wanawatukana sana mawaziri huu ni udhalilishaji
 
Mkuu hili naliona pia, ila sio mawaziri tuu, kuna makatibu na watu wengine nyeti " the untouchables " wataachia ngazi
Hawawezi achia maana watakuwa hawana pa kwenda/ shika, sana sana wapo wanaombea Mungu awasaidie wasije wakashindwa kasi.
 
Kwa mwendo wa kubana matumizi, kuepuka ulevi na kuzuiwa safari za nje zisizo na tija kwa taifa binafsi naona kuna mawaziri mwendo huu ni ngumu mno kwao! Kwa sasa wanataabika sana, exposure kwao imekua adimu kwa mambo yao binafsi. Nikionacho tuendako mbeleni kuna watu watazikimbia ofisi, wataomba wenyewe kuachia ngazi.

Kwa utawala uliopita kuna mawaziri walikua wakitumia muda mfupi sana ndani ya nchi, wengine walihamishia ofisi zao hotelini! Wengine walijitaftia hata pesa za kugombea urais kwa exposure walizokua nazo nje ya nchi. Sasa kwa mwendo huu wa kuwalazimisha wale mihogo waliozoea Pizza ni mtihani mgumu mno kwao. Ofisi kwa sasa zinaonekana ni kama za moto hivi.

Kwa hili nisiwe mnafki au mchoyo wa fadhila kumpongeza Mh Rais, acha waliozoea Pizza nao waonje uchngu na utamu wa mihogo!Asiyetaka akae pembeni awapishe waliozoea mihogo.
Umenikumbusha mbanano kati ya Nape na Mwigulu, Mwigulu alikuwa akijipangia kazi za uenezi wakati akijipigia chepuo kugombea Urais, makamba naye kaja na sera za kuwapa kipaumbele vijana huku akijingangia safari nyingi nje na ndani ili aweze kushawishi vijana wampigie kura akiteuliwa kuwa mgombea, sasa hapo vioja vya Nyarandu siwezi kuvitaja ilikuwa balaa
 
Kwa sasa hizo fujo hatuzioni tena.
 
Kwa mwendo wa kubana matumizi, kuepuka ulevi na kuzuiwa safari za nje zisizo na tija kwa taifa binafsi naona kuna mawaziri mwendo huu ni ngumu mno kwao! Kwa sasa wanataabika sana, exposure kwao imekua adimu kwa mambo yao binafsi. Nikionacho tuendako mbeleni kuna watu watazikimbia ofisi, wataomba wenyewe kuachia ngazi.

Kwa utawala uliopita kuna mawaziri walikua wakitumia muda mfupi sana ndani ya nchi, wengine walihamishia ofisi zao hotelini! Wengine walijitaftia hata pesa za kugombea urais kwa exposure walizokua nazo nje ya nchi. Sasa kwa mwendo huu wa kuwalazimisha wale mihogo waliozoea Pizza ni mtihani mgumu mno kwao. Ofisi kwa sasa zinaonekana ni kama za moto hivi.

Kwa hili nisiwe mnafki au mchoyo wa fadhila kumpongeza Mh Rais, acha waliozoea Pizza nao waonje uchngu na utamu wa mihogo!Asiyetaka akae pembeni awapishe waliozoea mihogo.

Yawezekana kweli lakini hao watakaoamua kuachia nyadhifa zao kwa sababu kama ulizozitaja hapa ni dhahiri bin shayiri watakuwa ni majipu yanayojaribu kukimbia vivuli vgao, hatutawaacha, tutawafuatilia undani wao na kuwatumbua ikibidi hukohuko waliko! No stone will be left unturned.
 
Hajielewi ndugu !eti Mimi sio mtabiri ila ni maoni tu, huku kichwa Chake cha habari kinaandikwa utabiri! Ni Shiida ni kama anakurupuka vile!
Ni bora ukatumia akili kufikiri! Kutabiri kitu siku moja ndio utakua mtabiri? Sioni hoja yako kiufupi.
 
Kwa mwendo wa kubana matumizi, kuepuka ulevi na kuzuiwa safari za nje zisizo na tija kwa taifa binafsi naona kuna mawaziri mwendo huu ni ngumu mno kwao! Kwa sasa wanataabika sana, exposure kwao imekua adimu kwa mambo yao binafsi. Nikionacho tuendako mbeleni kuna watu watazikimbia ofisi, wataomba wenyewe kuachia ngazi.

Kwa utawala uliopita kuna mawaziri walikua wakitumia muda mfupi sana ndani ya nchi, wengine walihamishia ofisi zao hotelini! Wengine walijitaftia hata pesa za kugombea urais kwa exposure walizokua nazo nje ya nchi. Sasa kwa mwendo huu wa kuwalazimisha wale mihogo waliozoea Pizza ni mtihani mgumu mno kwao. Ofisi kwa sasa zinaonekana ni kama za moto hivi.

Kwa hili nisiwe mnafki au mchoyo wa fadhila kumpongeza Mh Rais, acha waliozoea Pizza nao waonje uchngu na utamu wa mihogo!Asiyetaka akae pembeni awapishe waliozoea mihogo.
Mkuu mda c mref na mim ntaachia uwazir Wang maana daah yn nmezoea kwenda kula Bata Johannesburg kila wkend lakn sa iv nina mwez wa saba cjatok ndan ya nchi
 
Back
Top Bottom