Utabiri: Inakuja CCM iliyokosa utulivu.

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,970
Kuna uwezekano Mkubwa kabisa kukosekana kwa CCM iliyotulia baada ya muda mfupi ujao, ni bora hata CCM ya awamu zilizo pita. Itakua ya leo ni afadhili ya jana.

Awamu zilizopita CCM ilikua ikilalamikiwa kuendekeza makundi, lakini sasa kuna uwezekano wa kuibuka kwa makundi mengi mapya ndani ya Chama hicho hali ambayo watu watafikia kukiri kua ni bora CCM iliyopita.

Kuna kila dalili ya kuibuka makundi yatakayojiona kua ndio bora kilimo mengine na kuna makundi yatakayoibuka ndani ya chama yakilalamikia kusahauliwa katika ufalme uliopo na mengine yatakokua yanapinga jinsi uendeshwaji wa Chama ulivyo na mifumo yake mipya na yatafikia hata kutishia kujiunga na upinzani.

Ndivyo ilivyo na ndivyo inavyoweza kua.Kuna watu hua hampendi kuambiwa ukweli lakini wakati zaidi ndio huzungumza.
 
Hawa watu kampeni itakuwa ngumu mno. Hatari ni kwamba Magufuli ataenda kwenye uchaguzi kama Rais na si mgombea. Atatumia kauli za kero na za kibabe. Kisha kimya kimya atakumbushwa kila mtu abebe mzigo wake mwenyewe.
Hii ni fursa ya pekee kwa vyama kujipanga. Hii nafasi haitapatikana tena. Ile Kagera inatakiwa iwe ngome. Upinzani hamieni kule.
 
Hawa watu kampeni itakuwa ngumu mno. Hatari ni kwamba Magufuli ataenda kwenye uchaguzi kama Rais na si mgombea. Atatumia kauli za kero na za kibabe. Kisha kimya kimya atakumbushwa kila mtu abebe mzigo wake mwenyewe.
Mkuu unataka kusema ile kauli naomba mniombee intakuwa imekufa, au itaendelea lakini watu hawataomba.
 
Mkuu unataka kusema ile kauli naomba mniombee intakuwa imekufa, au itaendelea lakini watu hawataomba.
Mh Magufuli anaongoza kama alichaguliwa nchi nyingine akaletwa bongo au km watu waliomba akashuka toka mbinguni hivyo wanatakiwa wazidi kumuombea ili awepo.
Ipo haja ya kujiuliza, watu hufanikiwa kwa sababu wazazi na walezi wao ni wababe au ni wasikivu na wenye huruma. Inawezekana yote yakawa sahihi lakini Mh Rais huenda anaamini kuwa Rais ni kuwa na ufahamu uliopitiliza na wengine hawaelewi lolote kama yeye anavyotambua njaa.
Angejikumbusha kuhusu sukari na mangwangala, angejifunza.
 
Kwani yy na ww nani mwenyejukumu la kuhakikisha watz hawafi njaa? acha mambo ya jf, bro uliwahi hata siku moja kushuhudia njaa?
 
Kwani yy na ww nani mwenyejukumu la kuhakikisha watz hawafi njaa? acha mambo ya jf, bro uliwahi hata siku moja kushuhudia njaa?
Inategemea umezaliwa Lini ndugu? Hizi tarumbeta za msiuze mahindi ya kuchomwa, msitumie kwa pombe, msiuze nje nk zinasababishwa na nini kama si hofu ya njaa? Hivi ni sahihi uzalishe bidhaa kwa mtaji wako kisha upangiwe matumizi?
Kwa kumalizia, ni kweli njaa naifaham na chakula cha msaada ninakifaham
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom