Utabiri: Huenda ya KANU nchini Kenya yakaikumba CCM

TumainiEl

JF-Expert Member
Jan 13, 2010
6,184
11,200
Kule Kenya kulikuwa na chama imara na kilicho tikisa taifa kilichoitwa Kanu.
Hakuna asie juwa vile Kanu chini ya Kenyata na Mzee Moi kilivyo watoa kamasi wakenya.

Kilikuwa na power full makachero na kilikuwa na majasusi hatari like never before sidhani hata cc wamefikia hizo level.

Chini ya Moi chama kilishika hatam chini ya kauli yake Tata ya Harambee.

Wakenya walilima kwa kucha na Taifa lilipita nyakati uwenda mpaka sasa bado haijawahi tutokea.

Vifo vya kutisha kama kile cha akina Auko na yule waziri wa Ulinzi havito sahaulika ktk historia ya Kenya.

Raila Odinga huyu Mtoto pamoja na baba yake wamepona chupuchupu kwenye matukio yakupotezwa kwa sababu yasiasa.

Ilifika mahali wakenya walisema inatosha na wazee wakuu wa Taifa wakaona ndani ya kanu vita ya masilahi inataka kuliacha taifa ktk mtanziko mkubwa na uwenda chama kama chama kikawa moja ya kitisho cha uhai wa taifa na amani baada ya makundi hatari ndani ya chama kuibuka nakuwa kitisho kikubwa kwa viongozi na chama yani umafya umafya.. u do me i do u.

Tetesi zinasema wenye akili wakasema twendeni na dira ya Baba wa Taifa ila sasa vyombo vya ulinzi vifanye kazi yake na wanasiasa wafanye kazi yao.

Wanasiasa fanyeni siasa walinzi tunalinda atakaye shinda na kuzuwia makundi hatari ya uharamia ndani ya chama.

Pili historia yakutisha ya Kanu ili fika hatuwa wakasema huu mzoga utatunukia sisi na vizazi vyetu hivyo bora tuachane nao.

Mwisho wa Yote Kanu ilikufa na ndipo kukaibuka vyama kama Orange na 🍌 na yote yaliendelea ni historia.

Haikuwa Rahisi ila Kenya leo wanapumua na yule alie nyanyasika kwa miaka mingi anaenda kuwa Rais.

Sina huwakika kama chama cha ccm kitavuka tena miaka 50 au 10 kama hakija jigawa ili kupisha mabadiliko.

Huko tuendako uwenda chama kitakuwa na wakati mgumu sana kutokana na madhila na matukio watanzania wameona chini ya CCM.

Nina tia shaka wakuu wa Taifa hili ipo siku watasema bora kuvunja chama kuliko kubaki wamoja wakati ktk mioyo hatupo wamoja.

Ni siku ngumu na chungu uwenda wengi wasingependa kuiona ila uwenda tupo karibu sana.
 
Umenikumbusha mbali sana mdogo wangu alisoma Gusii miaka hiyo ujinga uliokuwepo wa kumuimba Moi asubuhi parade alikua anaushangaa sana..

Na mara kupewa yale maziwa ya packet mchana.

Kuvaa beji ya Moi na kumuita mtukufu Rais .

Na Tanzania niliona inaelekea huko Jiwe alipotaka kuanzisha somo la historia ili wamsome yeye.

Hakuna marefu yasiyo na ncha.
 
Kule Kenya kulikuwa na chama imara na kilicho tikisa taifa kilichoitwa Kanu.
Hakuna asie juwa vile Kanu chini ya Kenyata na Mzee Moi kilivyo watoa kamasi wakenya...
Mama akina makamba na nape ndo watakoiua ccm .jpm polepole na bashiru alijitahidi kila namna kufanya chama kiwe cha watu waote leo bila aibu nape anasema eti CCM ina wenywe ..tusubiri hao wenyewe watakuwa akina nani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umenikumbusha mbali sana mdogo wangu alisoma Gusii miaka hiyo ujinga uliokuwepo wa kumuimba Moi asubuhi parade alikua anaushangaa sana..

Na mara kupewa yale maziwa ya packet mchana...
Maziwa ya nyayo nimekunywa sana pande hizo
 
Hata hivyo amna kilichobadilika, rushwa, ufisadi, nidhamu ndogo kazini nk vimeendelea kutamalaki hata baada ya KANU kuondoka.


Hata Tanzania tukibadili chama tawala, bado tutahitaji katiba mpya.
 
Salute mkuu tunakoelekea hiki chama ni kweli kitavunjika wacha waendelee kufukuzana wacha waendelee kusemana na kutosamehana wacha waendelee kuridhishana watu wachache ktk chama wache waendelee kubaguana ndani ya chama na wacha makundi yaendele kuzaliwa ndani ya chama.

Ni suala la mda mfupi kweli kilichotokea kwa Kanu ndicho kinaenda kutokea CCM na ikifa CCM tutakuwa na kipindi cha mpito maana siasa itapata ushindani sana lkn itakuwa siasa ya hovyo mpaka hapo baadaye siasa itatulia na tutasonga mbele
 
  • Thanks
Reactions: Ame
CCM ikifa na Tanzania inakufa. CCM ndiyo inalinda huo unaoitwa muungano kwa nguvu ya dola, CCM ikifa na muungano unakufa tena haraka sana.

Muungano ukifa hakuna tena Tanzania. Nyerere alikuwa ni genius. Aliwategea bomu la muungano, akawaachia lile bomu CCM. CCM ikifa, bomu linalipuka.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom