CCM tumshauri Rais Samia asigombee 2025

Prof Koboko

JF-Expert Member
Aug 15, 2020
350
2,549
Nawasalimia kwa jina la JMT wanajukwaa.

Ndugu zangu hasa Makada wa CCM mliopo humu msinihukumu kua natumikia kundi au mlengo flani ndani ya chama. Niwe muwazi ni kwamba kwa sasa binafsi naridhika sana na utendaji wa Mama kwa miaka 5 tu aliyeachiwa na hayati JPM. Angeishia miaka hii 5 tu.

Sisemi kuwa haziwezi siasa lakini kwa hali ninayoitazama mbele ya safari inaweza kuwa ngumu zaidi, wapinzani wetu wapo kimya lakini hatujui wanawaza nini na mshindani wa Mama atakuwa nani. Kwanza CCM imeshaanza kugawanyika makundi ambayo binafsi sioni mtu wa kuyaweka pamoja kwa sasa, haya makundi kuna yapo yanayougulia maumivu makali sana na kuna yapo yanayopooza maumivu makali. Shida kubwa ni kwamba hayupo wa kuyaweka haya makundi pamoja, tofauti ya mitizamo ni kubwa mno.

Tunaweza kujifariji kwa kuzuia suala la katiba mpya itakayoondoa uwezekano wa Makada wenzetu kusimamia uchaguzi, lakini kuna wakati unaweza kufanya hujuma kubwa mpaka ukaaibika, huenda tunaweza kuelekea mahali ambapo mtu akishinda wananchi hawatakubali aporwe ushindi wake. Tusijifariji kuja kutegemea Dola itusaidie, tunaweza kuja kuaibika vibaya mno. Dola kuna wakati inachoka kutumiwa itakapobidi. Tumshauri Mama asimame kwa miaka mitano aliyorithi toka kwa JPM.

Gharama za maisha zinapanda kimya kimya, Miamala ya simu na vifurushi vya internet zinapandishwa kimya kimya, gharama mafuta ya kula,sukari, petroli,diesel,mafuta ya taa, vifaa vya ujenzi usiseme, Luku makato bila ya watu kuridhia, vurugu kwa wamachinga. Kiukweli watanzania siyo wajinga tusubiri tuadhibiwe ili tupate adabu miaka mitano watakayobeba wapinzani.

Tunaweza kufika mahali wapinzani wetu wakalazimisha katiba mpya wakatoka barabarani nchi nzima kuiomba, hivi polisi wanaweza kukamata kwa mfano wanachama wa CHADEMA million 6 nchi nzima? Watawaweka mahabusu zipi? Hata wakitoka milion 3 watawaweka wapi? Kuna mambo tunayafanyia mzaha lakini CCM mbele yetu hali ni tete.

Tungeruhusu katiba mpya tupambane kwa huo mfumo mpya badala ya mazoea na kuwapa kiki wapinzani. Hawa wapinzani tumewapa pumzi ya kua nje ya bunge miaka 5, hatujui wanarudi vipi na nguvu mpya.

Ni mawazo ya kada huru, hulazimishwa kuyachukua au kuyasoma.

Weekend njema!
 
Furaha ya CHADEMA ni SSH kugombea. Kama 2020 alipanikishwa na watu wa Mbeya akiwa mgombea mwenzao, 2025 akiwa mgombea si litakuwa shamba laini kulimwa na Lissu au Mbowe?

Tumwache aendelee kuingizwa kingi na establishment ya mwendazake kwa issue za hovyo kama Ugaidi.

Wana CCM wakiridhika kwamba ushawishi wa mama umeshuka sana, atakubali tu kupisha ki nyume na matakwa ya upinzani
 
Tunaweza kufika mahali wapinzani wetu wakalazimisha katiba mpya wakatoka barabarani nchi nzima kuiomba, hivi polisi wanaweza kukamata kwa mfano wanachama wa CHADEMA million 6 nchi nzima
Yaani kisa Chadema wanataka katiba mpya, ndiyo nchi ishindwe kufuata taratibu zake za kujiendesha. Chadema si wanauhubiri utawala wa sheria, inakuwaje wasitumie sheria hizo hizo zilizopo kudai katiba bila kulazimisha watu kuingia barabarani?

Chadema kisiwe kigezo cha kupitisha ajenda zenu za kuvuruga utaratibu tuliojiwekea wa kuendesha nchi. Kwa sababu hata katiba ya chadema hakuna mahali imeasema kuwa wanachama watatumia nguvu dhidi ya serikali halali iliyoko madarakani ikiwa inafuata taratibu za kuendesha nchi.
 
Mleta maada watu watashindwa kuelewa hapa. Kiukweli mama ushawishi hana tena

Shida iliyopo ipinxani nap wameshimdwa kueleweka; sioni kama wana mtu wa kusimamisha. Hatutaki wakimbizi watuwekee mtu mpya tuifundisge CCM adabu.

Anyawsy miaka minne bado hivyo tusubiri maana hatujui lile kundi linalougulia lina mipango gani.
 
Miaka 10 yake anaianza 2025, kwa sasa anamalizia kiporo cha JPM! Vumilia tu, tupo naye mpaka 2035
 
Nawasalimia kwa jina la JMT wanajukwaa.

Ndugu zangu hasa Makada wa CCM mliopo humu msinihukumu kua natumikia kundi au mlengo flani ndani ya chama. Niwe muwazi ni kwamba kwa sasa binafsi naridhika sana na utendaji wa Mama kwa miaka 5 tu aliyeachiwa na hayati JPM. Angeishia miaka hii 5 tu.

Sisemi kua haziwezi siasa lakini kwa hali ninayoitazama mbele ya safari inaweza kua ngumu zaidi, wapinzani wetu wapo kimya lakini hatujui wanawaza nini na mshindani wa Mama atakua nani. Kwanza CCM imeshaanza kugawanyika makundi ambayo binafsi sioni mtu wa kuyaweka pamoja kwa sasa, haya makundi kuna yapo yanayougulia maumivu makali sana na kuna yapo yanayopooza maumivu makali. Shida kubwa ni kwamba hayupo wa kuyaweka haya makundi pamoja, tofauti ya mitizamo ni kubwa mno.

Tunaweza kujifariji kwa kuzuia suala la katiba mpya itakayoondoa uwezekano wa Makada wenzetu kusimamia uchaguzi, lakini kuna wakati unaweza kufanya hujuma kubwa mpaka ukaaibika, huenda tunaweza kuelekea mahali ambapo mtu akishinda wananchi hawatakubali aporwe ushindi wake. Tusijifariji kuja kutegemea Dola itusaidie, tunaweza kuja kuaibika vibaya mno. Dola kuna wakati inachoka kutumiwa itakapobidi.
Tumshauri Mama asimame kwa miaka mitano aliyorithi toka kwa JPM.

Gharama za maisha zinapanda kimya kimya, Miamala ya simu na vifurushi vya internet zinapandishwa kimya kimya, gharama mafuta ya kula,sukari, petroli,diesel,mafuta ya taa, vifaa vya ujenzi usiseme, Luku makato bila ya watu kuridhia, vurugu kwa wamachinga. Kiukweli watanzania siyo wajinga tusubiri tuadhibiwe ili tupate adabu miaka mitano watakayobeba wapinzani.

Tunaweza kufika mahali wapinzani wetu wakalazimisha katiba mpya wakatoka barabarani nchi nzima kuiomba, hivi polisi wanaweza kukamata kwa mfano wanachama wa CHADEMA million 6 nchi nzima? Watawaweka mahabusu zipi? Hata wakitoka milion 3 watawaweka wapi? Kuna mambo tunayafanyia mzaha lakini CCM mbele yetu hali ni tete. Tungeruhusu katiba mpya tupambane kwa huo mfumo mpya badala ya mazoea na kuwapa kiki wapinzani. Hawa wapinzani tumewapa pumzi ya kua nje ya bunge miaka 5, hatujui wanarudi vipi na nguvu mpya.

Ni mawazo ya kada huru, hulazimishwa kuyachukua au kuyasoma.

Weekend njema!
Hakuna mwanakijani mwenye uthubutu,kama watu wenyewe wanaogopa vivuli vyao. Wenyewe.
 
Back
Top Bottom