Utabiri: Huenda ya KANU nchini Kenya yakaikumba CCM

CCM ikifa na Tanzania inakufa. CCM ndiyo inalinda huo unaoitwa muungano kwa nguvu ya dola, CCM ikifa na muungano unakufa tena haraka sana. Muungano ukifa hakuna tena Tanzania. Nyerere alikuwa ni genius. Aliwategea bomu la muungano, akawaachia lile bomu CCM. CCM ikifa, bomu linalipuka.
Huo muungano we unakunufaisha nin?

Sent from my TECNO BC2c using JamiiForums mobile app
 
Sina huwakika kama chama cha ccm kitavuka tena miaka 50 au 10 .

Acha janja janja za utabiri. Ina maana in 10 to 50 years ccm ikifa utabiri wako utakuwa umetimia😂😂

Ukisema in 10 years ccm inakufa huo ni utabiri ambao ukitokea hata nyuma ya hapo utapata sifa. Ila 10 to 50???? Hiyo ni janja janja ili ikitokea usifiwe na isipotokea useme muda bado.

Miaka 50 ni mingi sana, kizazi ni kipya na ccm haiwezi kuishi milele ipo wazi kuna siku itafutika na huo si utabiri.

Nikuulize miaka 50 ijayo ndani ya ccm unawaona kina nani? Ww unajiona wapi in 50 years? 😂😂😂 we jamaa bana.
 
Kule Kenya kulikuwa na chama imara na kilicho tikisa taifa kilichoitwa Kanu.
Hakuna asie juwa vile Kanu chini ya Kenyata na Mzee Moi kilivyo watoa kamasi wakenya.

Kilikuwa na power full makachero na kilikuwa na majasusi hatari like never before sidhani hata cc wamefikia hizo level.

Chini ya Moi chama kilishika hatam chini ya kauli yake Tata ya Harambee.

Wakenya walilima kwa kucha na Taifa lilipita nyakati uwenda mpaka sasa bado haijawahi tutokea.

Vifo vya kutisha kama kile cha akina Auko na yule waziri wa Ulinzi havito sahaulika ktk historia ya Kenya.

Raila Odinga huyu Mtoto pamoja na baba yake wamepona chupuchupu kwenye matukio yakupotezwa kwa sababu yasiasa.

Ilifika mahali wakenya walisema inatosha na wazee wakuu wa Taifa wakaona ndani ya kanu vita ya masilahi inataka kuliacha taifa ktk mtanziko mkubwa na uwenda chama kama chama kikawa moja ya kitisho cha uhai wa taifa na amani baada ya makundi hatari ndani ya chama kuibuka nakuwa kitisho kikubwa kwa viongozi na chama yani umafya umafya.. u do me i do u.

Tetesi zinasema wenye akili wakasema twendeni na dira ya Baba wa Taifa ila sasa vyombo vya ulinzi vifanye kazi yake na wanasiasa wafanye kazi yao.

Wanasiasa fanyeni siasa walinzi tunalinda atakaye shinda na kuzuwia makundi hatari ya uharamia ndani ya chama.

Pili historia yakutisha ya Kanu ili fika hatuwa wakasema huu mzoga utatunukia sisi na vizazi vyetu hivyo bora tuachane nao.

Mwisho wa Yote Kanu ilikufa na ndipo kukaibuka vyama kama Orange na na yote yaliendelea ni historia.

Haikuwa Rahisi ila Kenya leo wanapumua na yule alie nyanyasika kwa miaka mingi anaenda kuwa Rais.

Sina huwakika kama chama cha ccm kitavuka tena miaka 50 au 10 kama hakija jigawa ili kupisha mabadiliko.

Huko tuendako uwenda chama kitakuwa na wakati mgumu sana kutokana na madhila na matukio watanzania wameona chini ya CCM.

Nina tia shaka wakuu wa Taifa hili ipo siku watasema bora kuvunja chama kuliko kubaki wamoja wakati ktk mioyo hatupo wamoja.

Ni siku ngumu na chungu uwenda wengi wasingependa kuiona ila uwenda tupo karibu sana.
Zingatia tu kuwa marais wote wa Kenya ni ndani ya chain.
JamiiForums2140070670.jpg
JamiiForums990200756.jpg
 
Mama Samia anakopa unafikiri ni akili za wanawake wenzake wanaokopa VICOBA. Amejisahau kuwa yeye ni Rais.
Hii ina uhusiano gani na mada iliyopo mezani? Acha hii tabia. Mimi na wewe tuna mama..hebu tuwaheshimu! Pia mheshimu Mkuu wa nchi.🙏🙏🙏
 
Ulichokiandika ni sahihi na ni suala la wakati tu . Chini ya Jua hakuna taasisi itakayodumu milele . NINA HAMU YA KUUSHUDIA HUO WAKATI ,HAWA WANAODHANI TAIFA HILI HALIWEZI KUENDA PASIPO WAO WAKATI UNAKUJÀ
 
Hata warumi hawakuwahi kufikiri utawala wao utafikia mwisho pamoja na kutawala dunia kwa miaka mia tano. Mabadiliko huwezi kuyaona kila wakati, yanaweza kutokea ghafla.
Siyo vifo vyote hutokea mpaka uugue kwanza No. CCM imevuruga maisha ya watu wengi sana.
CCM aliyoianzisha Nyerere, hata yeye mwenyewe angekuwa hai, angeikataa na pengine kujuta kwa kile alichokianzisha kuwa chombo cha mateso kwa watu wake.
Tuliyoyashuhudia wakati wa Magufuli, CCM waliona na walinyamaza kimya . Hii kumfunga Sabaya na kutaka kumkamata Makonda wamesubiri mpaka Magufuli amekufa, Magufuli kuwa mwenyekiti hakuwezi kuwa sababu ya CCM kunyamazia uovu,ndio maana wanna vikao vya ngazi mbalimbali. Mahakama zimemkamata na hatia Musiba kipindi hiki.
CCM ya Nyerere pamoja na mapungufu yake iliheshimu Sana uhuru wa mahakama. Mwalimu alikuwa na mapungufu Kama mwanadamu na alikiri upungufu wake, lakini kwenye chombo Cha utoaji haki hakuingilia kabisa hata hotuba yake alipokumbushia Vita ya rushwa kipindi Chao na ikatokea waziri wake Fundikira akapatikana na makosa ya rushwa alipelekwa mahakamani lakini kwa kuwa mahakama ilikuwa huru haikuamua kufuata Utashi wa kisiasa Kama ilivyo leo na tunamuona Jaji mkuu anahudhuria kwenye mialiko ambayo ajenda zake zitakwenda mahakamani au ziko mahakamani na yeye bila haya anachangia. Upo wapi Uhuru wa mahakama chini ya CCM ya leo!!!
CCM imara isingeruhusu hayo. CCM ilinyamaza kimya hata pale kulipokuwa na tetesi za kuongezewa muda Magufuli kinyume Cha katiba.
Salmin Amour Rais wa Zanzibar wakati wake alijaribu kutaka kujiongezea muda CCM iliyokuwa imara wakati huo hawakumuogopa.
Leo CCM uongozi wanapeana wao wanaojiita wenye CCM na watoto wao. CCM imara isingekubali kuvunjwa kwa katiba kwa kuzuia vyama vya upinzani kufanya mikutano. CCM ya Sasa ni waoga usipime. Hawana watu wa kuaminika tena. Watu waliawaamini wanasiasa wasomi enzi hizo, siyo Sasa. Nani angeaacha kufuatilia majadiliano kwenye Meza ya duara kutoka redio ya ujerumani kama ukisikia leo atakuwepo, Prof Haroub Othman au Prof. Chachage au Mzee Kigunge!! Lakini kipindi tumewaona kina Kitila,Kabudi, Bashiru wote ni mashahidi,mambo mengi yameharibika wakishuhudia na wako kimya. Mbunge anapigwa risasi mchana kweupe na mwisho anavuliwa ubunge wake hawa wako bungeni wanashangilia.
Wachache waliobaki CCM hawapewi heshima kwa sababu wanapenda kusema ukweli. Mzee Warioba,Butiku na hata Jenerali ulimwengu wanapuuzwa.
Hivyo anguko la CCM halitashangaza kwani tayari ilishaanguka kwenye mioyo ya watanzania wengi imebakiza nguvu za dola tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom