Uswahili asili yake ni Uhindi ama uarabu?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
18,301
33,920
Aina ya maisha (Life style) ya watu wa pwani na baadhi ya watu wa bara ambayo yanaitwa maisha ya Kiswahili ni maisha yanayoaksi aidha Uhindi ama Uarabu.

Lakini "uswahili" asili yake ni kuiga mambo mengi ya watu toka India ama toka Uarabuni? Watu wa pwani kuitwa "Sahel" ndiyo tiketi ya kusemwa kwamba uswahili asili yake ni Uarabu?

Tukiangalia biashara, kuoana, ujenzi,na Lugha za watu wa pwani wanavyowasiliana jee tunaweza kufikia hitimisho gani kuhusu asili ya uswahili? Jee ni kuiga maisha ya waarabu waliokuja pwani ya Afrika Mashariki na kufika hadi ndani kabisa Bara ama Wahindi walioishia kwenye pwani hizi za Afrika Mashariki?
 
Acha kuchanganya madensa uswahili asili yake ni kibantu
Kwa mfano jinsi waswahili tunavyofanya sherehe za harusi zetu kunafanana na wabantu wote? Yaani mambo ya kupeleka sanduku Upande wa kikeni na mambo ya kula solo ni ubantu?
 
Mkuu huwezi kutenganisha uswahili, uislamu na waarabu
Sitaki kutenganisha bali nauliza tu. Kuna mambo mengi sana waswahili wanafanana na wahindi kuliko waarabu. Angalia aina ya mavazi yanayovaliwa na wanawake wa Pwani kwa rangi na urembo wake zinaaksi zaidi uhindi kuliko uarabu!!
 
waswahili wengi hupenda kutumia au kunogeshea uswahili wao na maneno ya kiarabu.
wahindi wengi washambawashamba tu
 
Mkuu hoja ni mavazi au lugha..?

Mbona wanaume wa kiswahili sasa hivi wanavaa sana majeans kutoka huko ulaya ina maana tuseme waswahili asili yao huko ulaya au..?
 
waswahili wengi hupenda kutumia au kunogeshea uswahili wao na maneno ya kiarabu.
wahindi wengi washambawashamba tu
Unadhani vyakula vinavyopendelewa zaidi na waswahili asili yake ni India ama Uarabuni. Kwa mfano pale Darajani Zanzibar kati ya vyakula vyenye asili ya Kihindi amaKiarabu vingi ni vipi?
 
Unadhani vyakula vinavyopendelewa zaidi na waswahili asili yake ni India ama Uarabuni. Kwa mfano pale Darajani Zanzibar kati ya vyakula vyenye asili ya Kihindi amaKiarabu vingi ni vipi?
Wahindi wamekaa sana zanzibar ambapo walikuwepo waarabu,hivyo kuiga baadhi ya tamaduni hasa za vyakula sio ajabu.

Kwani wewe unazungumzia lugha au life style ya mvazi na vyakula,mana naona waenda huku nakule mkuu.

Tulia kwenye jambo moja kwanza
 
Mkuu hoja ni mavazi au lugha..?

Mbona wanaume wa kiswahili sasa hivi wanavaa sana majeans kutoka huko ulaya ina maana tuseme waswahili asili yao huko ulaya au..?
Kati ya vitu vinavyojenga tamaduni ya jamii fulani mavazi hayana nafasi. Hivi ni kwa nini ni rahisi kuwatambua wamasai kama si kwa uvaaji wao?
 
Sasa wewe unazungumzia kuitambua tamaduni katika nyanja la lugha au mavazi..?
Kati ya vitu vinavyojenga tamaduni ya jamii fulani mavazi hayana nafasi. Hivi ni kwa nini ni rahisi kuwatambua wamasai kama si kwa uvaaji wao?
 
Back
Top Bottom