Ustaarabu wa Bongo

Ustaarabu wa Bongo

tajirijasiri

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Posts
2,863
Reaction score
3,854
Mara Kadhaa unaweza kukutana na ustaarabu huu wa Bongo:-

1. Kuulizwa "umeniletea zawadi gani?" hata kabla haujapewa pole ya safari kana kwamba alikupatia pesa umnunulie.

2. Kukutana na mtu dukani akakulazimisha umnunulie kitu au umtoe mkwanja, na usipomnunulia au kumpa linakuwa bifu.

3. Bidada kujihisi unamtaka kimapenzi kila umsalimiapo.

Je, ukiwa kama mdau, kuna ustaarabu mwingine wa Bongo umewahi kukutana nao?

Changia....
 
4. Tumekutana kwa bahati mbaya cafeteria, canteen au restaurant, unaniomba nikununulie chakula au kinywaji, kwani pale umetekwa?
 
Mara Kadhaa unaweza kukutana na ustaarabu huu wa Bongo:-

2. Kukutana na mtu dukani akakulazimisha umnunulie kitu au umtoe mkwanja, na usipomnunulia au kumpa linakuwa bifu.

Hiyo kitu imenikuta jana tu!, yaani wanaboa sana aisee
 
Unakutana na mtu baa anakulazimisha umnunulie pombe
 
Hii nimeikuta Kinondoni, Binti/mama akinyanyuka kwenda ext.ziro (chooni) utakuta anafuatwa na wanawake wenzie wakimuomba akawaombee bia alipokaa, mimi hujiuliza ni lazima wanywe bia? tena za kuomba? basi aombe mmoja kila mmoja kwa wakati wake hata watatu, cha kushangaza wanakuomba wewe ambaye pale hunywi hiyo bia umefata story na marafiki zako. Aiiibu Aibu zao hata wao!!!!!.
 
Back
Top Bottom