Ustaarabu ndani ya mabasi ya abiria ni muhimu sana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ustaarabu ndani ya mabasi ya abiria ni muhimu sana

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Sipo, May 8, 2009.

 1. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #1
  May 8, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  jana nikiwa kwenye basi la kwenda tegeta nilishuhudia uchafu mmoja uliokuwa ukifanywa na KIJANA na BINTI mmoja. Hawa walikuwa wamekaa siti ya nyuma kabisa halafu yule kijana alikuwa ANAMSHIKASHIKA yule binti MATITI uku yule binti akiwa amemuegemea. Kumbuka watu wamesimama kwenye basi kutokana na tabu ya usafiri, kuna watu wazima na wadogo, wanafunzi n.k
  Naamini hii ni tabia ya kukemea hasa kwa vijana ambao wanatakiwa kuleta mabadiliko. Huu sio UZUNGU ila UPUNGUANI
   
 2. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #2
  May 8, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Sipo wacha vijana wajiachie, kama mmeshindwa (serikali) kucontrol circulation ya vigazeti vyakipuuzi vya shigongo vinavyochapisha picha na habari za ngono mpaka kwenye front page bila kujali ethics za jamii yetu. Vijana wanasoma na kuangalia hizo picha na KUONA PENGINE SIE WAZAZI WAO NA SERIKALI TUMERIDHIA UCHAFU HUO. Therefore this is an end result of our failure to control and up hold our culture na lazima wote tujilaumu kwa hili. By the way sio kwamba nasapoti hii khali ila najaribu kuelezea jinsi gani na sisi kama walezi tumechangiaa ktk mmomonyoko wa maadili.

  Alaaniwe Shigongo na magazeti yake!!!
   
 3. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #3
  May 8, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Sasa mbona wewe haujawashtua waache kushikana?
   
 4. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #4
  May 8, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Senior, ingekuwa ngumu kutokana na mazingira, ningeweza kukosa msaada kama jamaa ange-react. Si unajua kuwa abiria huwa tuna mitizamo tofauti, inawezekana wengine walikuwa wana-enjoy
   
 5. Andindile

  Andindile JF-Expert Member

  #5
  May 8, 2009
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Ungeweza kutumia njia ambayo jamaa asingejihisi kuwa unataka kumdharirisha mbele za watu. Mfano, kuongea na jamaa wa kiume peke yake kwa kumnong'oneza kuwa kitendo anachofanya angesubiri wafike sehemu ambayo haina kadamnasi badala ya kumpayukia ndani ya basi. Kwa njia hiyo hata yeye angeona umemstahi pamoja na makosa yake yote.

  Mara nyingi watanzania huwa tunakosa uthubutu wa kusema jambo pale muhusika anapokuwepo. Akiondoka tu, tunakuwa hodari wa kuipamba story. oh hata mimi nilimwona akifanya ...............
   
 6. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #6
  May 8, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Shigongo is just a drop of water in the sea!

  Kuna mambo kadhaa mengi sana ya kimaadili ambayo yameachiliwa na aidha wazazi au serikali. Mojawapo ni:

  1. Vibanda vya kuonyeshea sinema vya mitaani- hizi ni sehemu za hatari sana. Kila mzazi na ahakikishe mwanae hapiti jirani na maeneo hayo hatari.

  2.Magazeti hayo jamii ya akina Shigongo sielewi kwanini hayafuatiliwi. Ni upuuzi kupiga marufuku vile vijitabu vya mapenzi vilivyokuwa vinauzwa kwa wauzamagazeti, huku ukiacha magazeti ya Shigongo yakichukua nafasi ya vijitabu vile.

  3.Vipindi vyetu vya TVs navyo vinasaidia sana kupandisha mihemko miongoni mwa vijana wanaokua. Mliopo kwenye taaluma hii ya broadcasting na regulatory bodies saidieni kurekebisha hali hii.

  4.Simu hizi za kisasa nazo ni balaa, maana zimebadilisha kabisa mwelekeo wa maadili yetu. Wanafunzi wanakuwa na simu za bei mbaya zikiwa zimejaa picha za ngono na wanatumiana na kuangalia masaa yote.

  5.Pia kuna hizi sinema za kibongo za akina Ray, mfano live ni picha iitwayo OPRAH. Ile picha ni nzuri sana, lakini imekuja kuvurugwa kwenye scene moja ambapo inaonyesha live watu wakitupana kitandani, na hatimaye kutoa miguno ambayo, hata mtoto asiyejua masuala hayo atapatwa na udadisi kutaka kuona kinachoendelea huko chumbani.

  6. Pia sasa hivi, sijui ni taasisi gani inahusika moja kwa moja na hili, lakini kuna kasi kubwa mno ya importation ya mikanda ya picha chafu mitaani.Nani asiyejua kwamba pale kati ya round about ya Uhuru na Msimbazi, na junction ya mtaa wa Congo ndo center ya mauzo ya kanda hizo- tena mchana kweupe?

  Kwahiyo wadau, nadhani hao vijana waliokuwa wanapeana vionjo vya uzinzi kwenye Daladala wanakabiliwa na Pressure za kila aina toka kwenye jamii yetu, ambapo zooote zinawaonyesha kuwa uzinzi ni kitu cha kawaida.

  Lakini, ndugu SIPO, kama alivyosema mdau mwingine hapo juu, did you take any initiative to stop them, au ndo yale ya ....mtoto wa mwenzio ni mkubwa mwenzio!!
  Cheers!!
   
  Last edited: May 8, 2009
 7. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #7
  May 8, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Mzalendo,
  vijana kama hawa ambao hawajistahi mbele za watu, unakuta wameshindikana kwao au wazazi wao wameshindwa kuwalea.Wewe mtu baki ukiwakoromea unataka kugeuka ze comedy kwenye basi maana wanaweza kukuporomoshea matusi ukabaki na aibu.
  Kuna mama mmoja tena mzee aliwahi kumwambia binti mmoja kwamba alivyovyaa siyo vizuri na ni chukizo kwa mwenyezi Mungu( alikuwa amevaa kata k. huku nguo ya ndani thong ikiwa imebaki nje nje) .Yule mdada aliishia kumtukana yule mama mbele za watu bila aibu, huku akimwambia huyo Mungu basi anibeep nimpigie...........mengine makubwa yalifuatia baada ya hapo.
  Kwa kifupi hailipi kuanza kukaripia vijana/watoto walioshindikana.
  Shigongo atalaumiwa kwa magazeti lakini tatizo siyo Shigongo.
   
Loading...