Usomi wa Rais Magufuli na Kasumba ya Kiingereza

Bado najiuliza kama Phd yake ni ya kughushi. Je alitoa hongo kwa uongozi wa UDSM au nini kilitokea ?
na alikuwa na ushawishi gani wa kuweza kutunukiwa shahada ya 3 bila kufuata taratibu sahihi ?

Na je malengo yake ni yapi yaliyopelekea aghushi Phd yake kama kweli alighushi ?
 
Lugha ni njia ya mawasiliano, ni chombo kinachotumika katika kuwasilisha ile hali ya kuelimika kwa jamii fulani. Wasomi wengi wa Tanzania wamepata elimu katika mataifa kama China, Russia, France, Germany na zile nchi za Scandinavia. Wengi wa wasomi hawa, mwaka wao wa kwanza ulitumika katika kujifunza lugha ya wenyeji, halafu miaka inayofuata ndipo huanza kusomea fani mbalimbali za kitaaluma.

Wale maprofesa ambao wanafunzi wa kitanzania wanalazimika kujifunza mwaka wa lugha ili waweze kufundishwa nao yale masomo ya fani, mara nyingi hawajui kabisa lugha ya kingereza.

Lakini kwa sababu kujua kingereza sio kuelimika, maprofesa hao wala hawaoni aibu kutokuijua lugha ya kingereza. Wameshaelimika kiasi cha kuigawa elimu yao kwa wanafunzi wa kigeni kutoka Tanzania, bila ya wao kulazimika kuwa watumwa wa lugha ya kingereza.

Kuna wale ambao wanamkejeli rais Magufuli, wakisema kwamba hapandi ndege kwenda Ulaya kwa sababu ya tatizo la lugha ya kingereza, wanasema kuwa anashindwa kuongea na wageni wa kimataifa kwa sababu hajui vizuri kingereza. Huyu anayekejeliwa ni msomi wa ngazi ya PHD, ambaye baadhi ya watu wanamkejeli kwa sababu ya kasumba ya kupenda vituu vya kigeni.

Maprofesa wa mataifa yasiyozungumza lugha ya kingereza, waliowafundisha wasomi wetu ambao ndio "vichwa" vya taifa hili, ni watu walioelimika bila hata ya kulazimika kuwa watumwa wa lugha ya kigeni kwao yaani kingereza.

Sisi tuliotawaliwa tunaona fahari kukifahamu kingereza!. Wakati hatuna maendeleo yoyote ambayo yanahusiana na kingereza, ambayo tunaweza kujivunia kwamba yametokana na sisi.

Tunamkejeli rais wetu tukisema kwamba hayuko vizuri kwenye kingereza, wakati hicho kiswahili chenyewe hatukijui!!. Hicho kiswahili ambacho ni lugha ya taifa kinaishia kutamkwa midomoni peke yake, hakuna maendeleo yoyote yale ya kiteknolojia ambayo yanahusishwa na lugha ya kiswahili kwa asilimia mia moja.

Miaka ya nyuma huko migodini wazungu ambao huko Uingereza na Australia walikuwa ni wafungwa, walipewa kazi na kulipwa mishahara mikubwa kwa sababu tu ya kuongea kwao lugha ya kingereza!.

Hawakuwa na utaalamu kuwazidi wataalamu wazalendo waliosomea VETA na vyuo vingine vya ufundi hapa hapa Tanzania. Ulimbukeni wetu ukawapa maisha bora wageni, kwa sababu akili zetu zilinasa kwenye mtego wa kubabaikia kingereza.

Watanzania tuachane na huu ushamba wa kuiona lugha ya kingereza kama vile ndio kila kitu maishani.
Kha !ndo atuambie font fegi n phd juu.msitetee ujinga lazima ajue zote il kurahisisha mawasiliano
 
Tulimuona hapa rais wa china akiwa na mkaliman hata kingereza hajuu
Tofauti yetu na China ni kwamba kwetu ili uwe msomi lazima ujue kiingereza
Masomo kuanzia sekondari hufundishwa kwa kiingereza hivyo kama hukijui hapa kwetu hujasoma,period
Ama kuhusu vyeti hata Mrema ana digrii ingawa aliishia la kumi,kama ambavyo Bashite anavyo japo alifeli kuanzia darasa la nne. Ukitafuta kwa ujanja utavipata tuu
watch it!!
 
Lugha ni njia ya mawasiliano, ni chombo kinachotumika katika kuwasilisha ile hali ya kuelimika kwa jamii fulani. Wasomi wengi wa Tanzania wamepata elimu katika mataifa kama China, Russia, France, Germany na zile nchi za Scandinavia. Wengi wa wasomi hawa, mwaka wao wa kwanza ulitumika katika kujifunza lugha ya wenyeji, halafu miaka inayofuata ndipo huanza kusomea fani mbalimbali za kitaaluma.

Wale maprofesa ambao wanafunzi wa kitanzania wanalazimika kujifunza mwaka wa lugha ili waweze kufundishwa nao yale masomo ya fani, mara nyingi hawajui kabisa lugha ya kingereza.

Lakini kwa sababu kujua kingereza sio kuelimika, maprofesa hao wala hawaoni aibu kutokuijua lugha ya kingereza. Wameshaelimika kiasi cha kuigawa elimu yao kwa wanafunzi wa kigeni kutoka Tanzania, bila ya wao kulazimika kuwa watumwa wa lugha ya kingereza.

Kuna wale ambao wanamkejeli rais Magufuli, wakisema kwamba hapandi ndege kwenda Ulaya kwa sababu ya tatizo la lugha ya kingereza, wanasema kuwa anashindwa kuongea na wageni wa kimataifa kwa sababu hajui vizuri kingereza. Huyu anayekejeliwa ni msomi wa ngazi ya PHD, ambaye baadhi ya watu wanamkejeli kwa sababu ya kasumba ya kupenda vituu vya kigeni.

Maprofesa wa mataifa yasiyozungumza lugha ya kingereza, waliowafundisha wasomi wetu ambao ndio "vichwa" vya taifa hili, ni watu walioelimika bila hata ya kulazimika kuwa watumwa wa lugha ya kigeni kwao yaani kingereza.

Sisi tuliotawaliwa tunaona fahari kukifahamu kingereza!. Wakati hatuna maendeleo yoyote ambayo yanahusiana na kingereza, ambayo tunaweza kujivunia kwamba yametokana na sisi.

Tunamkejeli rais wetu tukisema kwamba hayuko vizuri kwenye kingereza, wakati hicho kiswahili chenyewe hatukijui!!. Hicho kiswahili ambacho ni lugha ya taifa kinaishia kutamkwa midomoni peke yake, hakuna maendeleo yoyote yale ya kiteknolojia ambayo yanahusishwa na lugha ya kiswahili kwa asilimia mia moja.

Miaka ya nyuma huko migodini wazungu ambao huko Uingereza na Australia walikuwa ni wafungwa, walipewa kazi na kulipwa mishahara mikubwa kwa sababu tu ya kuongea kwao lugha ya kingereza!.

Hawakuwa na utaalamu kuwazidi wataalamu wazalendo waliosomea VETA na vyuo vingine vya ufundi hapa hapa Tanzania. Ulimbukeni wetu ukawapa maisha bora wageni, kwa sababu akili zetu zilinasa kwenye mtego wa kubabaikia kingereza.

Watanzania tuachane na huu ushamba wa kuiona lugha ya kingereza kama vile ndio kila kitu maishani.
Aliyetaka kufatilia phd ya mkulu aliuawa na mwili wake kutupwa kwenye mto ruvu
 
Elimu ya huyo Rais wa China kaipata kwa Kiingereza? Huu mjadala mngeucha tuu maana ni kuzidi kumuanika Rais wetu bure hata hiyo mifano mnayotoa haiendani.
Swali ni kwa nini yeye amesoma mpaka level ya Phd kwa kiingereza na bado kinampa shida?
Yeah...!! Wanaruka ruka huku wanatoa mifano icyoendana wanaacha mada wanaenda ushabiki..!! Rais wa china kasoma kwa kichina so kujua kingereza co lazima kama huyu wetu ambaye amesoma mpaka hapo kwa kiingereza
 
ACHANA NA WAJINGA WENGI WA KITANZANIA AMABAO WAMESOMA ILA HAWAJAELIMIKA. KUHUSUDU MAMBO YA KIINGEREZA YANASABABISHA WAGENI WANATUMIA MWANYA HUU KUTUNYIMA AJIRA.OVERALL MAGUFURI ANAJUA KIINGEREZA VIZURI TU.NDO MAAANA ALIKUWA MWALIMU WA SEKONDARI LAKINI PIA KAFANYA PhD yake UDSM kwa kiingereza. Lakini zaidi Msc yake ameifanyia UK na akafaulu sana.
Una hoja nzuri tu. Lakini kuniambia kuwa kuwa mwalimu wa sekondari ndio kigezo cha kujua kingereza vizuri: hilo si kweli kabisa. Nilifundishwa na walimu kadhaa sekondari ambao kingereza ilikuwa shida sana. (Note - sina maana Mh. hajui kiinglishi, kuwa mwalimu wa sekondari si kigezo)
 
Lugha ni njia ya mawasiliano, ni chombo kinachotumika katika kuwasilisha ile hali ya kuelimika kwa jamii fulani. Wasomi wengi wa Tanzania wamepata elimu katika mataifa kama China, Russia, France, Germany na zile nchi za Scandinavia. Wengi wa wasomi hawa, mwaka wao wa kwanza ulitumika katika kujifunza lugha ya wenyeji, halafu miaka inayofuata ndipo huanza kusomea fani mbalimbali za kitaaluma.

Wale maprofesa ambao wanafunzi wa kitanzania wanalazimika kujifunza mwaka wa lugha ili waweze kufundishwa nao yale masomo ya fani, mara nyingi hawajui kabisa lugha ya kingereza.

Lakini kwa sababu kujua kingereza sio kuelimika, maprofesa hao wala hawaoni aibu kutokuijua lugha ya kingereza. Wameshaelimika kiasi cha kuigawa elimu yao kwa wanafunzi wa kigeni kutoka Tanzania, bila ya wao kulazimika kuwa watumwa wa lugha ya kingereza.

Kuna wale ambao wanamkejeli rais Magufuli, wakisema kwamba hapandi ndege kwenda Ulaya kwa sababu ya tatizo la lugha ya kingereza, wanasema kuwa anashindwa kuongea na wageni wa kimataifa kwa sababu hajui vizuri kingereza. Huyu anayekejeliwa ni msomi wa ngazi ya PHD, ambaye baadhi ya watu wanamkejeli kwa sababu ya kasumba ya kupenda vituu vya kigeni.

Maprofesa wa mataifa yasiyozungumza lugha ya kingereza, waliowafundisha wasomi wetu ambao ndio "vichwa" vya taifa hili, ni watu walioelimika bila hata ya kulazimika kuwa watumwa wa lugha ya kigeni kwao yaani kingereza.

Sisi tuliotawaliwa tunaona fahari kukifahamu kingereza!. Wakati hatuna maendeleo yoyote ambayo yanahusiana na kingereza, ambayo tunaweza kujivunia kwamba yametokana na sisi.

Tunamkejeli rais wetu tukisema kwamba hayuko vizuri kwenye kingereza, wakati hicho kiswahili chenyewe hatukijui!!. Hicho kiswahili ambacho ni lugha ya taifa kinaishia kutamkwa midomoni peke yake, hakuna maendeleo yoyote yale ya kiteknolojia ambayo yanahusishwa na lugha ya kiswahili kwa asilimia mia moja.

Miaka ya nyuma huko migodini wazungu ambao huko Uingereza na Australia walikuwa ni wafungwa, walipewa kazi na kulipwa mishahara mikubwa kwa sababu tu ya kuongea kwao lugha ya kingereza!.

Hawakuwa na utaalamu kuwazidi wataalamu wazalendo waliosomea VETA na vyuo vingine vya ufundi hapa hapa Tanzania. Ulimbukeni wetu ukawapa maisha bora wageni, kwa sababu akili zetu zilinasa kwenye mtego wa kubabaikia kingereza.

Watanzania tuachane na huu ushamba wa kuiona lugha ya kingereza kama vile ndio kila kitu maishani.

Wakulaumiwa hapa ni Magufuli mwenyewe. Ni yeye ndio hupenda kuchomekea tuvingereza katika hotuba au mazungumzo yake ya papo kwa papo. Mimi najua na Watanzania wengi wanajua kwamba rais wetu hajui Kingereza. Lakini, hiyo sio kesi na wala sio aibu. Anachotakiwa kufanya yeye ni kujikita kwenye Kiswahili tu na wanapokuja wageni wasiojua kiswahili basi atumie Kiswahili kitupu na wakalimani wamsaidie kutafsiri. Tatizo rais huyu hata akitumia wakalimani bado tu atajitutumua kuchomekea maneno au sentesi za Kingereza, na hapo ndio naona anajichoresha na kujiaibisha. Mfano mzuri ni ile siku aliyokuja rais Lungu wa Zambia.
 
I see no problem as long as the message is sent. Nani miongoni mwetu anaweza kusema anajua kiingereza?
Hakuna...mtanzania typical akianza kuongea kingereza na mkenya au mnigeria, ni vichekesho vitupu, sentensi zake mbili tu za kwanza, baada ya hapo kinaanza kigugumizi cha ukubwani.
 
Wakulaumiwa hapa ni Magufuli mwenyewe. Ni yeye ndio hupenda kuchomekea tuvingereza katika hotuba au mazungumzo yake ya papo kwa papo. Mimi najua na Watanzania wengi wanajua kwamba rais wetu hajui Kingereza. Lakini, hiyo sio kesi na wala sio aibu. Anachotakiwa kufanya yeye ni kujikita kwenye Kiswahili tu na wanapokuja wageni wasiojua kiswahili basi atumie Kiswahili kitupu na wakalimani wamsaidie kutafsiri. Tatizo rais huyu hata akitumia wakalimani bado tu atajitutumua kuchomekea maneno au sentesi za Kingereza, na hapo ndio naona anajichoresha na kujiaibisha. Mfano mzuri ni ile siku aliyokuja rais Lungu wa Zambia.
Tatizo lenu nyinyi mnakuwa na chuki za kipuuzi, mnaona kama vile kuongea kingereza ndio ujanja wa dunia hii.

Ugumu wa maisha unapowatandika ipasavyo hasira zenu mnamalizia kwenye kumkejeli rais, haiwasaidii na haitawasaidia.

JK anachomekea maneno ya kingereza, unataka kuniambia kuwa anakifahamu kingereza kuliko mama Theresa May?.
 
Kha !ndo atuambie font fegi n phd juu.msitetee ujinga lazima ajue zote il kurahisisha mawasiliano
Nyinyi mnakijua kingereza?. Mnafanana sana na wale watu ambao wakimwona mzungu wanaanza kumtetemekea, kumbe kwao Ulaya ni mchovu fulani tu.

Acheni ushamba, jifunzeni kuthamini kilicho chenu, jifunzeni kuwa ni uhalisia wa kwenu wenyewe. Unadhani kwanini Mwalimu Nyerere anaheshimiwa mpaka kesho?, alitengeneza uhalisia wa kwake mwenyewe.

Kwa taarifa yako JPM kwa sasa anaheshimika kila kona ya dunia hii, ila nyinyi wachache msiojielewa ndio mnaongea pumba humu JF.
 
Mimi nitafurahi siku Magufuli akitembelewa na mzungu au hata mtu asiejua Kiswahili aweke mkalimani yeye Akomae na Kiswahili mwanzo mwisho.
hapo zamani za kale mara baada ya uhuru watanganyika wengi walienda kusoma shule wakitokea mashambani kwa wakulima. lugha yao kubwa ilikuwa ulimi wa mama. wakakutana na kiingereza shuleni wakifundishwa na waalimu walioiva kufundisha kwa lugha ya kiingereza. wakajifunza sarufi na fasihi bora kabisa ya kiingereza. kwa huo msingi waliojengewa na waalimu wakaelimika vizuri sana kwa kiingereza. hawakuwahi kusema kiingereza hakieleweki. Elimu waliyopata kwa kiingereza kama udaktari,URUBANI,Kuongoza ndege, Ukulima, ualimu, ujenzi, mawasiliano, afya, dini, wakaitumia vizuri wakatibu wagonjwa wakapona, wakafundisha wanafunzi wakawa pro, drs, wanasheria, na taaluma zingine nyingi, wakajenga barabara, nyumba, ofisi, miundombinu ya maji, simu, radio na kadhalika. Kila mtu wa enzi zetu za miaka ya 60, 70, 80, 90 alipenda kujifunza kwa kiingereza na aliemika tulipendelea kusoma Novel za wazungu kama vile James Hadley Chase na nyinginezo tukazielewa. library service zilikuwa mobile kwa Gari special, unaazima kitabu baada ya wiki unarudisha. Shule zilikuwa na Library zilizosheheni viatbu vya kila maarifa kuanzia ukulima wa kisasa na elimu ya kujitegemea. Muda wa kwenda library ulikuwepo. Muda wa kujiandaa kwa kwaya, maaigizo, ngonjera, mashairi, gwaride, utamaduni(ngoma) kwa ajili ya sherehe za UHURU, MAPINDUZI, SABASABA, NANENANE, AZIMIO LA ARUSHA, MUUNGANO tulikuwa nao.Shuleni tulikuwa na club za midahalo ya kiingereza, drama, na music. Tulifurahia shule, tulijifunza kuandika barua kwa kiingereza ya urafiki na ya kuomba kazi tumeapply kwenye real life tumefanikiwa.
Ikaja miaka ya 2000 ya Dot.com.,miaka ya uwazi na utandawazi wanafunzi wanaona kila kitu mtandaoni kusoma vitabu hawataki wanasema hawaelewi kwa kiingereza. Itabidi tuanze kutafsiri physics, chemistry, biology, mathematics kwa kiswahili ambacho hata maneno ya kutosha yanayozungumzwa katika maongezi ya kawaida hakuna. kwa mfano neno umbijani, kinakilishi,baobonye. Mimi naona Kiswahili cha kuongea kuwasiliana kinatosha. Waalimu wafundishwe Kiingereza vizuri kama waalimu wetu ili waweze kufundisha wanafunzi. Ikiwezekana tuImport/tuombe msaada wa Waalimu kutoka nje kama ilivyokuwa zamani. Waalimu na wanafunzi wa English Medium wako vizuri sana kuanzia vidudu. Tuseme tuu kugharamia Elimu hatuwezi. Niko tayari kukosolewa!
 
Tatizo lenu nyinyi mnakuwa na chuki za kipuuzi, mnaona kama vile kuongea kingereza ndio ujanja wa dunia hii.

Ugumu wa maisha unapowatandika ipasavyo hasira zenu mnamalizia kwenye kumkejeli rais, haiwasaidii na haitawasaidia.

JK anachomekea maneno ya kingereza, unataka kuniambia kuwa anakifahamu kingereza kuliko mama Theresa May?.

Wewe bila shaka hukusoma nilichoandika au kukuelewa. Ungeelewa, usingeandika huu upuuzi. Tatizo la "Kiswakinge" sio la rais wetu tu, bali ni la wabunge na jamii ya "wasomi" nchini kwetu. Ukisikiliza Bunge, matatizo ni hayohayo ya kuchomekea sentesi za Kingereza. Lakini, wengi wao ukiwaambia tuongee Kingereza kitupu, hawewezi. Sasa kwanini tuendelee kujidhalilisha na lugha za watu? Kwanini tusiongee Kiswahili kitupu, tena fasaha? Najua Kiswahili bado hakina tafsiri ya maneno kadhaa ya kitaaluma, lakini wakati tunaendelea kutumia baadhi ya maneno hayo katika sentesi zetu za kiswahili (sio Kingereza), ni jukumu letu kubuni au kutafuta tafsiri ya maneno hayo kwa Kiswahili ili kuikuza lugha yetu.
 
Nyinyi mnakijua kingereza?. Mnafanana sana na wale watu ambao wakimwona mzungu wanaanza kumtetemekea, kumbe kwao Ulaya ni mchovu fulani tu.

Acheni ushamba, jifunzeni kuthamini kilicho chenu, jifunzeni kuwa ni uhalisia wa kwenu wenyewe. Unadhani kwanini Mwalimu Nyerere anaheshimiwa mpaka kesho?, alitengeneza uhalisia wa kwake mwenyewe.

Kwa taarifa yako JPM kwa sasa anaheshimika kila kona ya dunia hii, ila nyinyi wachache msiojielewa ndio mnaongea pumba humu JF.

Pole weye danganya bashite wenzio kwa heshima ya mdomoni
 
Wewe bila shaka hukusoma nilichoandika au kukuelewa. Ungeelewa, usingeandika huu upuuzi. Tatizo la "Kiswakinge" sio la rais wetu tu, bali ni la wabunge na jamii ya "wasomi" nchini kwetu. Ukisikiliza Bunge, matatizo ni hayohayo ya kuchomekea sentesi za Kingereza. Lakini, wengi wao ukiwaambia tuongee Kingereza kitupu, hawewezi. Sasa kwanini tuendelee kujidhalilisha na lugha za watu? Kwanini tusiongee Kiswahili kitupu, tena fasaha? Najua Kiswahili bado hakina tafsiri ya maneno kadhaa ya kitaaluma, lakini wakati tunaendelea kutumia baadhi ya maneno hayo katika sentesi zetu za kiswahili (sio Kingereza), ni jukumu letu kubuni au kutafuta tafsiri ya maneno hayo kwa Kiswahili ili kuikuza lugha yetu.
Hakuna dhambi yoyote kuchomekea maneno ya kingereza, kama vile isivyo dhambi kwa mtu kutokuweza kutiririka kingereza.

Usimdharau mtu kwa kutumia lugha za kejeli eti kwa sababu hawezi kutiririka kingereza, kwa muingereza na mzungu mwingine wewe na mimi ni vinyago tu, haipo haja ya kujikomba.
 
Bora wewe umesema utadhani hata wakipata Rais mzungu awe anaongea hicho kingereza WATAKIELEWA....watanzania bwana we are so fun.
 
Wewe bila shaka hukusoma nilichoandika au kukuelewa. Ungeelewa, usingeandika huu upuuzi. Tatizo la "Kiswakinge" sio la rais wetu tu, bali ni la wabunge na jamii ya "wasomi" nchini kwetu. Ukisikiliza Bunge, matatizo ni hayohayo ya kuchomekea sentesi za Kingereza. Lakini, wengi wao ukiwaambia tuongee Kingereza kitupu, hawewezi. Sasa kwanini tuendelee kujidhalilisha na lugha za watu? Kwanini tusiongee Kiswahili kitupu, tena fasaha? Najua Kiswahili bado hakina tafsiri ya maneno kadhaa ya kitaaluma, lakini wakati tunaendelea kutumia baadhi ya maneno hayo katika sentesi zetu za kiswahili (sio Kingereza), ni jukumu letu kubuni au kutafuta tafsiri ya maneno hayo kwa Kiswahili ili kuikuza lugha yetu.
Hakuna mtanzania asiyechanganya lugha., hata tunapoongea lugha za ulimi mama lazima tuweke kiswahili. Aliyesoma kwa Kiingereza huku anaongea kiswahili na venacular lazima wakati wa kujieleza aweke kiingereza. Napenda sana mtu anayemix lugha kama wakenya! huo ufasaha wa nini ikiwa mtu anaeleweka.
 
Hakuna dhambi yoyote kuchomekea maneno ya kingereza, kama vile isivyo dhambi kwa mtu kutokuweza kutiririka kingereza.

Usimdharau mtu kwa kutumia lugha za kejeli eti kwa sababu hawezi kutiririka kingereza, kwa muingereza na mzungu mwingine wewe na mimi ni vinyago tu, haipo haja ya kujikomba.

"Kinyago" ni wewe peke yako, na fikra zako za kitumwa. Mimi ni mtu mwenye heshma yangu binafsi na katika jamii. Tena ninao wazungu wanaonifanyia kazi (nimewaajiri) kwasababu na wao ni watu kama sisi tu. Hoja yangu inabaki palepale, unapochanganya Kiswahili na Kingereza, wengi wa Watanzania wanaokusikiliza wanashindwa kukuelewa. Ila kwa watu kama nyinyi, kichanganya lugha hizi mbili, ndio mnaona ufahari na usomi. Kazi ipo!
 
Back
Top Bottom