Usomi sana na kuwa 'anti-social'

Usomi sana na kuwa 'anti-social'

ong'wafaza

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2012
Posts
262
Reaction score
115
Swali:Je, kuna uhusiano wowote kati ya wasomi sana na socialization?
Kumekuwa na dhana kwamba watu wenye elimu kubwa mara nyingi wanaonekana kuwa ma anti-social.
Nakumbuka hata shuleni na vyuoni wengi wa wale wanafunzi waliokuwa na akili sana darasani walikuwa hawachezi hata mziki ukiwepo shuleni.
Aidha, hata kwenye taasisi mbalimbali za ajira, wale ambao ni wasomi sana hawashiriki sana kwenye shughuli za kijamii kama vile harusi na misiba zinapotokea makazini au hata kwa majirani zao.
Je, dhana hiyo ya kuhusisha elimu na u anti-social ni sahihi?
Hebu watafiti tufanyieni utafiti wa hiyo hypothesis .
Hii itasaidia katika kujenga jamii yenye ushirikiano na hata kuongeza mshikamano miongoni wa wananchi kwa kutungwa sera zitakazoondoa gap iliyopo kati ya haya makundi mawili.
Vilevile itasaidia kupunguza kama sio kuondoa kabisa dhana ya kwamba wasomi wazuri hawawezi kuwa wasanii au wanamichezo wazuri.
Naomba kuwasilisha.
 
Ni sahihi always intelligent people never talk frequently but they talk for purpose,hiyo ni kutokana na uumbaji wa MUNGU mwenyewe ko never change the fact
 
Huo ndo ukweli kabisa, na kwa hii awamu wanapata tabu sana

Unamaliza chuo, hujui mtu asie na ajira anaishije mtaani, hujasociolize na watu kupata connection za apa na pale
Unabaki wa kushinda ndani tu na simu,

Hii kitu inawakumba graduator kibao wa miaka hii
 
Huo ndo ukweli kabisa, na kwa hii awamu wanapata tabu sana

Unamaliza chuo, hujui mtu asie na ajira anaishije mtaani, hujasociolize na watu kupata connection za apa na pale
Unabaki wa kushinda ndani tu na simu,

Hii kitu inawakumba graduator kibao wa miaka hii
Na hawataki kujushugulishs
kisa wamesoma
hio mentality mm hata sielewi walikofundishiwa
 
Back
Top Bottom