Uso wangu unaharibika sana

Chief Lugina

JF-Expert Member
Jul 1, 2011
286
76
JD please kwa yeyote anayeweza kunisaidia mafuta au lotion ambayo inaweza kufanya uso wangu uwe soft bila chunusi wala makovu. Nimetumia mafuta na lotion ya kila aina lakini naona kama namaliza hela tu na imefikia sasa saona kama uso umekuwa sugu. Please kama kuna mtu yeyote anaye weza kunisaidia please niambie nitumie nini ili kufanya uso wangu kuwa soft.

NOTE: Siyo kunifanya kuwa mweupe(Kuni braech) nataka nibaki na color yangu but isiwe na mabaka na chunusi....
 
Try Vaseline. . .
Au ukamwone mtaalamu akushauri mafuta ya aina gani yataendana na ngozi yako (ya mafuta, kavu. . . ).
 
Una miaka mingapi? Isije ikawa ndiyo unaingia kwenye balehe? Au hiyo steji uliiruka bila kutokwa chunusi. Mimi siyo mtaalam wa hiyo fani ya udaktari ila nauliza tu.
 
1. tumia vitunguu saumu..chukua vitunguu saumu vimenye kisha vitwangetwange alafu chuja maji yake then osha uso wako kwa maji ya uvuguvugu kisha paka mchujo huo ktk sehemu zilizo athirika kaa kwa muda wa dk 15 then osha kwa maji ya uvuguvugu fanya kwa cku mara moja
2.chukua asali mbichi ya nyuki wadogo kijhko kimoja changanya na mdalasini vikijiko viwili kisha osha uso wako vizuri kwa maji ya uvuguvugu then paka mchanganyiko huo kaa kwa dk 15 then osha kwa maji ya uvuguvugu,tiba hii ni bora ikatumika usiku kabla ya kulala
3.chukua asali mbichi ya nyuki wadogo kijiko kimoja changanya na ndimu tatu then osha uso wako kwa maji ya uvuguvugu kisha paka mchanganxiko huo kaa kwa muda wa dk 15 then osha uso kwa maji ya uvuguvugu
4.nenda ktk maduka ya madawa nunua cream inaitwa perlsol fornte cream inasaidia sana ktk matatizo ngozi km chunusi na makovu..
 
Wewe ni she au He? Kama ni He cheza mechi sana kila siku unapiga bao mbili kwa mda wa mwezi hivi makovu na vichunusi vinaisha vyote ila zingatia,kunywa maji mengi,kula vizuri na pia chonde chonde usiuze mechi(tumia ndomu)
 
Matibabu hutegemea una ngozi ya aina gani na una umri gani na kama una allergies za aina gani. Ni bora umuone mtaalamu wa ngozi ili akupime na akupatie tiba husika.
 
1. tumia vitunguu saumu..chukua vitunguu saumu vimenye kisha vitwangetwange alafu chuja maji yake then osha uso wako kwa maji ya uvuguvugu kisha paka mchujo huo ktk sehemu zilizo athirika kaa kwa muda wa dk 15 then osha kwa maji ya uvuguvugu fanya kwa cku mara moja
2.chukua asali mbichi ya nyuki wadogo kijhko kimoja changanya na mdalasini vikijiko viwili kisha osha uso wako vizuri kwa maji ya uvuguvugu then paka mchanganyiko huo kaa kwa dk 15 then osha kwa maji ya uvuguvugu,tiba hii ni bora ikatumika usiku kabla ya kulala
3.chukua asali mbichi ya nyuki wadogo kijiko kimoja changanya na ndimu tatu then osha uso wako kwa maji ya uvuguvugu kisha paka mchanganxiko huo kaa kwa muda wa dk 15 then osha uso kwa maji ya uvuguvugu
4.nenda ktk maduka ya madawa nunua cream inaitwa perlsol fornte cream inasaidia sana ktk matatizo ngozi km chunusi na makovu..

Gozo, mwongozo wako unaonekana umemaliza form six. Asante sana. Ila sasa nashangaa kwa nini usianze kutumia wewe kwanza manake duuu kama kweli hiyo avator ndiyo picha yako halisi!!!
 
Kama ngozi ya uso ulishaichosha kwa madawa mengi (ma-lotions) au mamikorogo huko nyuma usitegemee kupata mabadiliko chanya. Pole sana
 
Gozo, mwongozo wako unaonekana umemaliza form six. Asante sana. Ila sasa nashangaa kwa nini usianze kutumia wewe kwanza manake duuu kama kweli hiyo avator ndiyo picha yako halisi!!!

Usiogope mkuu mi ndo hendisamu pekee duniani nisiyetumia scrub na facial ya aina yoyote ile lakini ngozi yangu inang'aa kama site mirror za bajaji sport new model 2012..
 
JD please kwa yeyote anayeweza kunisaidia mafuta au lotion ambayo inaweza kufanya uso wangu uwe soft bila chunusi wala makovu. Nimetumia mafuta na lotion ya kila aina lakini naona kama namaliza hela tu na imefikia sasa saona kama uso umekuwa sugu. Please kama kuna mtu yeyote anaye weza kunisaidia please niambie nitumie nini ili kufanya uso wangu kuwa soft.

NOTE: Siyo kunifanya kuwa mweupe(Kuni braech) nataka nibaki na color yangu but isiwe na mabaka na chunusi....

jipake goli, asubuh na kabla ya kulala kwa muda wa wiki mbili.
 
Jaribu kutumia hii kama utafanikiwa kuipata.

is-proactive-a-good-acne-scsar-removal-cream-300x264.jpg
 
Jitahidi usile vyakula vyenye mafuta mengi e.g chips, maandazi, chapati n.k mara kwa mara. Kula matunda na mboga mboga za kutosha, bila kusahau maji glass 6-8 kwa siku.
Upumzishe uso na hayo ma-cream, jaribu kunawa tu na maji ya vuguvugu mara mbili kwa siku (usitumia sabuni inakausha ngozi), tumia vitu vya asili zaidi mf. asali na limao kama alivyoshauri mdau hapo juu.
Kila la heri....
 
Back
Top Bottom