Usiyoyajua kuhusu Taifa la Uholanzi (Netherland)

Usiyoyajua kuhusu Taifa la Uholanzi (Netherland)

God Made Dutch and Dutch Made Holland!!!!

1. Ni nchi ya kwanza kugeuza eneo la bahari kuwa eneo la makazi (Land Reclamation)

2. Nchi Inayoongoza kwa kuwa na watu warefu zaidi duniani, wastani wa urefu wa wanaume ni sm 184 (karibu mita 2) ilihali wanawake ni sm 170

3. Nchi ya Kwanza Duniani Kuhalalisha Ushoga Mnamo Mwaka 2001

4. Nchi Yenye Idadi Kubwa ya Baiskeli Kuliko Hata Idadi ya watu, sensa ya mwisho inaonesha nchi hiyo ina Baiskeli milioni 18 sawa na zaidi ya baiskeli moja kwa kila raia

5. Nchi ambayo imehalalisha haramu nyingi kiasi cha kuwafanya watu wawe huru sana na hivyo kupunguza kama si kuondoa wafungwa kabisa. Hii ni nchi pekee ambayo imelazimika kuazima wafunwa toka mataifa mengine maana jela zao zipo tupu

6. Nchi ambayo wanawake hufurahia maisha kuliko nchi nyingine yoyote duniani kwa kupewa kipaumbele cha kwanza, wakifuatiwa na mtoto, Mbwa, Baiskeli na Mwanaume kipaumbele cha mwisho

7. Nchi yenye maduka ya ngono (sex shops) na vioski huru vya kuvutia bangi (maarufu kama coffee shops) ambapo unaingia na kuvuta bangi utakavyo kisha unarudi kitaa...yaani ukiingia coffee shop unakutana na menu za bangi tu

8. Miongoni mwa nchi maarufu kwa starehe duniani kwani licha ya kuongozwa kwa unywaji wa pombe yao maarufu ya Heineken pia inachagizwa na kauli mbiu ya S 3 (SAND, SUN AND SEX)

9. Nchi inayoongoza kwa unywaji wa kahawa duniani (wastani wa vikombe 3 kwa siku kwa mtu) sababu ni kwamba licha ya baridi kahawa inawafanya wasilale ili waendelee na starehe
View attachment 327437
10. Likizo ya uzazi ni siku 57 na inaweza kuchukuliwa muda wowote hadi mtoto anapofikisha miaka 8!!
Kuhusu nchi hii uko sahihi, Red Light District Amsterdam
ni hatariiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii!
 
Uchumi wa nchi yenyewe ukoje? Ni ya ngapi kwa uchumi duniani? Uchumi wake hasa unategemea nini? Wastani wa pato LA kila RAIA ukoje, naona umeelezea mambo ya starehe tu bila kueleza hela za starehe wazipata wapi
 
ngoja nifanye mpango wa visa niende zangu huko uholanzi nikatulie mpaka 2020 nakuja kuchungulia kama bado naenda zangu eritrea nikajitwalie vimwana wazuri mpaka 2025 narudi tena bongo!!!! Ccm wakiingia tena madarakani nahama kabisa na uraia!!!
 
Wako vizuri sana wanatupa hadi misaada. Wanategemea sana Bandali, uwanja wa ndege na pia wanazalisha sana mboga na matunda
 
Wako vizuri sana wanatupa hadi misaada. Wanategemea sana Bandali, uwanja wa ndege na pia wanazalisha sana mboga na matunda
Hiyo nchi ina idadi ya watu wangapi? Idadi yao sasa na sisi, mbona mi naona sources yao ya mapato ni ndogo kuliko sisi na bado wanatupa misaada, yaani bandari, airport na ukulima wa mbogamboga? Sisi tumelogwa nani? Kwa sababu sisi tuna vitu lukuki MF utalii,, madini, bandari, nk na bado maskini?
 
ngoja nifanye mpango wa visa niende zangu huko uholanzi nikatulie mpaka 2020 nakuja kuchungulia kama bado naenda zangu eritrea nikajitwalie vimwana wazuri mpaka 2025 narudi tena bongo!!!! Ccm wakiingia tena madarakani nahama kabisa na uraia!!!
Weee ni soo
 
Wako vizuri sana wanatupa hadi misaada. Wanategemea sana Bandali, uwanja wa ndege na pia wanazalisha sana mboga na matunda
Bila kusahau diary industry wako so advanced..
 
Watu wengi hawajui sana kuhusu taifa la Netherland au Uholanzi, Hii nchi ya Uholanzi pia ndio hufaamika kama Holland au Netherland au Dutchland, ndio nchi pekee duniani yenye majina matatu ambayo yote hutumika kumanisha nchi mmoja.

Nchi ya Uholanzi hufahamika kwa kauli mbiu ya taifa hilo isemayo "God Made Dutch and Dutch Made Holland!!!!"

Yafuatayo ni usiyoyajua kuhusu nchi hii ya Holland/Dutchland/Netherland

1. Ni nchi ya kwanza kugeuza eneo la bahari kuwa eneo la makazi (Land Reclamation) Yasemekana kwamba Uwanja wa Ndege wa Schipol uko Mita 4.5 chini ya usawa wa Bahari, ndio uwanja wa ndege ulio chini zaidi duniani.

2. Nchi Inayoongoza kwa kuwa na watu warefu zaidi duniani, wastani wa urefu wa wanaume ni sm 184 (karibu mita 2) ilihali wanawake ni sm 170. Inasadikika kwamba sababu kuu mchanganyiko wa vinasaba pamoja na unywaji wa maziwa kwa wingi tangu mwaka 400 AD.

3. Nchi ya Kwanza Duniani Kuhalalisha Ushoga Mnamo Mwaka 2001

4. Nchi Yenye Idadi Kubwa ya Baiskeli Kuliko Hata Idadi ya watu, sensa ya mwisho inaonesha nchi hiyo ina Baiskeli milioni 18 sawa na zaidi ya baiskeli moja kwa kila raia. Kwa wastani wadachi huendesha baiskeli umbali wa km 2.5 kila siku sawa na km 900 kwa mwaka

5. Nchi ambayo imehalalisha haramu nyingi kiasi cha kuwafanya watu wawe huru sana na hivyo kupunguza kama si kuondoa wafungwa kabisa. Hii ni nchi pekee ambayo imelazimika kuazima wafungwa toka mataifa mengine maana jela zao zipo tupu

6. Nchi ambayo wanawake hufurahia maisha kuliko nchi nyingine yoyote duniani kwa kupewa kipaumbele cha kwanza, wakifuatiwa na mtoto, Mbwa, Baiskeli na Mwanaume kuwa kipaumbele cha mwisho.

7. Nchi yenye maduka ya ngono (sex shops) na vioski huru vya kuvutia bangi (maarufu kama coffee shops) ambapo unaingia na kuvuta bangi utakavyo kisha unarudi kitaa...yaani ukiingia coffee shop unakutana na menu za bangi tu na watu wanavuta bila hata kupata mawenge.

8. Miongoni mwa nchi maarufu kwa starehe duniani kwani licha ya kuongozwa kwa unywaji wa pombe yao maarufu ya Heineken pia inachagizwa na kauli mbiu ya S 3 (SAND, SUN AND SEX)

9. Nchi inayoongoza kwa unywaji wa kahawa duniani (wastani wa vikombe 3 na zaidi kwa siku kwa mtu) sababu ni kwamba licha ya baridi kahawa inawafanya wasilale ili waendelee na starehe.

10. Likizo ya uzazi ni siku 57 kwa wote baba na mama na inaweza kuchukuliwa muda wowote hadi mtoto anapofikisha miaka 8!!

11. Ni moja ya nchi pekee duniani ambapo makaburi hukodishwa kwa kati ya miaka 5 hadi 10 kutegemea pochi lako na hii inatokana na uhaba wa maeneo ya kuzikia nchini humo

12. Ndio nchi ya asili ambayo Makaburu wanaoishi Afrika Kusini walitokea.

13. Ni moja ya nchi balani Ulaya ambayo inanasibishwa na taifa la Ujerumani, hii ni kutokana wote asili yao kuwa Dutch, kila mmoja hudai ndio asili (original) ya mwenzake.

14. Ndio nchi ya kwanza duniani kuanzisha shirika la ndege duniani (Air line) ambalo ndio shirika la ndege kongwe zaidi duniani linaloitwa KLM.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom