Usiyoyajua kuhusu pweza

Usiyoyajua kuhusu pweza

Nashangaa kuna watu wanaweza kula pweza lkn wanahisi kinyaa kula konokono. Miili yao iko sawa tu. Wakati unakula konokono wewe vuta picha kwamba nI pweza. Mambo yanakwenda fresh tu. Zambia kuna watu wanakula konokono
 
Huko ZNZ kijana au mwanaume kabla hajakwenda kufunga ndoa anapikiwa supu ya pweza wiki anakunywa. Inatokana na imani husika lakini issue ya potency ni protein ya mnyama huyo ilivyo nyingi. Anaweza akaingia katika mwili au fuvu la mnyama mwingine wa bahari kujilinda akawa anatembea yumo humo. Mjanja sana. Pamoja na ujanja wake binadamu anamuua au kumvua na inabidi upige mikono yake hiyo uibonde ndio ilainike uweze kuchemsha. Misuli yake ni kabambe sana. Symbiotically watu ndio wanafananisha na urijali. Kumbe ni dishi ule zuri sio kutegemea pweza pekee-atakapopatikana unamla mtaani bila ya kuogopa kipindupindu. Poleni!
 
1.Pweza wote wana kichwa kinachoitwa mantle kilichozungukwa na mikono nane inayoitwa tentacles.
ogani zote muhimu za pweza kama vile ubongo na moyo hupatikana kichwani.

2.Sehemu ngumu kuliko zote katika mwili wa pweza ni mdomo anaoutumia katika kulia.

3.Damu ya pweza ni ya rangi ya bluu.

4.Pweza wote wana mioyo mitatu.

5.Watu wengi hudhani ya kwamba,pweza ni samaki wakati katika uhalisia pweza si samaki.

6.Mikono ya pweza ni viungo vyenye akili zake zenyewe,2/3 ya nyuroni zote za pweza hupatikana katika mikono na ufanyaji kazi wake hautogemei amri kutoka kwenye ubongo.

7.Pweza wote wana sumu inayoweza kumuua mwanadamu lakini mwenye sumu hatari zaidi ni blue ringed octopus anayeweza kuua zaidi ya mwanadamu mmoja kwa mda mfupi ikiwa atachokozwa.

8.Pweza ni mnyama mwenye akili kuliko wanyama wote wasio na uti wa mgongo,anaweza kujifunza baadhi ya mambo kama kufunua na kufunika jagi la maji,kutatua baadhi ya mafumbo na hata kutofautisha maumbo ya vitu.
Kwa hizo sifa zote alizonazo ndio maana anaongeza nguvu kwenye kale kamchezo
It has unique characteristics
 
Nimeamka asubuhi nimekuta mke wangu kaniandalia supu ya pweza, si kawaida yake, wacha niinywe tu tuone
 
Back
Top Bottom