hydroxo
JF-Expert Member
- Oct 19, 2015
- 3,251
- 6,790
1.Pweza wote wana kichwa kinachoitwa mantle kilichozungukwa na mikono nane inayoitwa tentacles.
ogani zote muhimu za pweza kama vile ubongo na moyo hupatikana kichwani.
2.Sehemu ngumu kuliko zote katika mwili wa pweza ni mdomo anaoutumia katika kulia.
3.Damu ya pweza ni ya rangi ya bluu.
4.Pweza wote wana mioyo mitatu.
5.Watu wengi hudhani ya kwamba,pweza ni samaki wakati katika uhalisia pweza si samaki.
6.Mikono ya pweza ni viungo vyenye akili zake zenyewe,2/3 ya nyuroni zote za pweza hupatikana katika mikono na ufanyaji kazi wake hautogemei amri kutoka kwenye ubongo.
7.Pweza wote wana sumu inayoweza kumuua mwanadamu lakini mwenye sumu hatari zaidi ni blue ringed octopus anayeweza kuua zaidi ya mwanadamu mmoja kwa mda mfupi ikiwa atachokozwa.
8.Pweza ni mnyama mwenye akili kuliko wanyama wote wasio na uti wa mgongo,anaweza kujifunza baadhi ya mambo kama kufunua na kufunika jagi la maji,kutatua baadhi ya mafumbo na hata kutofautisha maumbo ya vitu.