Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,746
- 25,662
Hata hi Leo wapo ila sasa kuna mbinu mpya na za kileo mapigano ya waasi Wa congo yanafadhiliwa, Sudan kusini Na kwengineko kwa mbinu mbadala na huo alotumia Che Guevara Wa kupigana bega kwa bega na anaowasaidia, na ya sasa hivi ni mabaya zaidiDuuh zamani kulikuwa kuna watu wanaojua kujitolea kutoka moyoni
shukran mkuuMkuu ongezea na hili,
Jina alilotumia Che kuingia Congo kwa mara hiyo ya pili lilikuwa Ramon Benetiz.
Baada ya Che kujifunza Kiswahili kidogo, alijipa yeye mwenyewe na wenzake hao wawili majina ambayo ingekuwa rahisi kwa Wacongo kuwaita. Dreke, aliyekuwa wa pili baada ya Che, akaitwa Moja, Papi akaitwa Mbili na Che akajiita Tatu.
Aprili 20, siku moja tu baada ya kuwasili, Che na watu wengine 14 wakaondoka Dar es Salaam kwa gari kuelekea Kigoma. Barabara ilikuwa mbaya wakati huo na safari yenyewe ilichukua siku mbili. Kwa mujibu wa maelezo ya kwenye Pasajes, Che na wenzake walipanda boti kupitia Ziwa Tanganyika na kwenda Congo.
Che alikaa katika mapambano ya kumsaidia Kabila dhidi ya majeshi ya Joseph Kasavubu na baadaye Mobutu Sese Seko kwa muda wa miezi saba. Wacuba waliokuwa na Che hawakufanikiwa katika azma yao.
Katika kitabu cha Anderson kuhusu Che nilichokieleza kabla, yaliandikwa mengi kuhusu namna Che alivyoshindwa kutimiza azma yake. Mosi, ni aina ya viongozi ambao aliwakuta Congo ambao hawakuwa wakifanana kitabia na mtu kama Castro.
Wakati akina Castro walipambana katika eneo la milima la Sierra Maestra kila siku bila kutoka, Kabila alionekana kwenye uwanja wa mapambano mara moja tu katika wakati wote ambapo Che alikuwa vitani.
Mara zote Kabila na wenzake walikuwa na udhuru wa kutokuwepo vitani. Wanamapinduzi wa aina ya Kabila walikuwa wakifanya siasa zao kwenye viwanja vya ndege, hoteli za kitalii na majiji makubwa duniani.
Che aliporudi Dar kutoka Congo alilalamika kuhusu wapiganaji wa Kabila. Alisema alivunjika moyo nao kwa vile hawakuwa na maana na kwamba mara nyingi wakivuta bangi tu.
Kama walivyo wanamapinduzi wengine mahiri, Che Guevara pia alikiri makosa yake binafsi kwenye vita hiyo ya Congo ambayo ilishindwa kupata matokeo yaliyotarajiwa.Akiandika katika kitabu chake hicho cha Pasajes de la Guerra Revolucionaria (Congo), Che aliandika.
“Kuna mambo kadhaa ambayo pengine sikuyafanya vizuri kwenye mapambano yale. Labda nilikuwa mkali sana kwa askari wangu. Nilikuwa nikitumia mbinu za adhabu ambazo wakati mwingine si za kawaida kwa askari kama vile kuwashindisha njaa.
“Pili, nilikuwa na uhusiano mzuri na wananchi masikini na askari wa chini kuliko wale wa ngazi za juu. Kasoro ninayoijutia ni kwamba sikujifunza vya kutosha lugha ya Kiswahili na hili lilininyima fursa ya kuwasiliana vizuri na watu wengi zaidi.
“Nimejifunza mengi Congo; yakiwamo makosa ambayo sitaraji kuyarudia. Labda yatakuwepo mengine ambayo nitayarudia na mengine mapya nitakayoyafanya. Sasa nimeamini zaidi kuhusu mapambano haya ya msituni dhidi ya ubeberu kuliko ilivyokuwa kabla.Sitasahau kuhusu kushindwa kwangu huku na mafunzo haya niliyojifunza Congo.
mkuu samahan hivi che alihusika mapinduzi ya zanzibarMkuu ongezea na hili,

Tuko mkuu sema wakina Sizonje na Bashite wana turudisha nyumasiku hizi watu tumekuwa wa kujipenda wenyewe wenye roho kama huyu jamaa wamebaki wachache sana