Usitoe nguo zako ulizozivaa kwa kituo cha yatima

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
21,079
Reaction score
43,471
Kila mtu anapaswa kujua kwamba ili Mungu akubariki ni lazima utoe kilicho bora zaidi na sio kitu ambacho hata hukihitaji tena.

Hata Mungu alimtoa mwanae wa pekee kama tunavyoamini sisi wakristo. Angeweza kumtoa mmoja wa malaika wake lakini alitoa kilicho bora zaidi.

Ikiwa unataka kuwapa watoto yatima nguo, nenda dukani, nunua nguo mpya na uwape. Au uza nguo zako ulizotumia na utoe hizo pesa wakajinunulie.

Nguo ulizozitumia hazina tofauti na makombo ya chakula.
 
Mwenyewe navaa zilizotumika Ulaya halafu niende dukani nikanunue mpya kuwapa yatima!.
Waweza kuwa na nguo nzuri lkn huzitumii kwaiyo unashauri bora zitupwe kuliko kuwapa yatima.
Halafu ni akili mbovu kutoa misaada kwa mategemeo ya kupata thawabu au baraka.
 
Kila mtu anapaswa kujua kwamba ili Mungu akubariki ni lazima utoe kilicho bora zaidi na sio kitu ambacho hata hukihitaji tena.

Hata Mungu alimtoa mwanae wa pekee kama tunavyoamini sisi wakristo. Angeweza kumtoa mmoja wa malaika wake lakini alitoa kilicho bora zaidi.

Ikiwa unataka kuwapa watoto yatima nguo, nenda dukani, nunua nguo mpya na uwape. Au uza nguo zako ulizotumia na utoe hizo pesa wakajinunulie.

Nguo ulizozitumia hazina tofauti na makombo ya chakula.
umeongea vyema ila jina lako linakusaliti.

vipi na mungu atakubariki kama ukiwaongoza binadamu wenzako kwa haki, bila kuwaumiza au kuwaibia stahili zao za kura

#NoReformsNoElection
 
Kuna kale ka wimbo kana sema

"Toa ndugu ,toa ndugu uulicho nachoo wewe .
Bwana atakuona mpaka moyoni mwako "
 
umeongea vyema ila jina lako linakusaliti.

vipi na mungu atakubariki kama ukiwaongoza binadamu wenzako kwa haki, bila kuwaumiza au kuwaibia stahili zao za kura

#NoReformsNoElection
Huu sio uzi wa siasa
 
Back
Top Bottom