usitake mwili ukutawale utawale wewe

usitake mwili ukutawale utawale wewe

ladyfurahia

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2011
Posts
14,758
Reaction score
9,592
Habari zenu wanachitchat wenzangu

naona mko ifit kimtindo leo nimeingia kwa gia namba 4 ambayo haiwezekani kabisa kushika njia za matopeni kwani itakwama yenyewe ni lami kwa kwenda mbele jamani waungwana wenzangu acha leo niwaase kwa mada hii inayosema kuwa usitake mwili ukutawale bali uutawale, wako watu wengi ambao wameshindwa kuutawala miili yao wameacha miili yao iwatawale na mwishoe wanajuta kwa yale mwili uliyoyachagua kuyatenda, wengine wetu wamediliki kusema mwili unataka kwanini niuzuie usitake kile kiutamanicho, Tamaa ya mwili mara nyiingi hupelekea mauti na mwisho ni kifo bila hata kukitaraijia. Wewe mwenzangu ambaye wahuruhusu mwili wako kutenda maovu mfano kuvuta sigara, kunywa pombe, kutamani mali ya mwenzako, kufanya uzinzi, kutukana na kusema uongo na mambo mengine yanayofanana na hayo ni upuuzi mbele za Mungu na ni chukizo kabisa Mungu hapendi watu wake aliowaumba wafanye yaisiyompendeza yeye kwani aliwaumba kwa mfano wake na aliwaumba kwa utukufu wake iweje wewe ndugu yangu unauachia mwili wako ufanye maovu na sio kuleta baraka kwa Mungu. iweje uhuruhusu mwili wako ukutawale na sio wewe kuutawala kwa mambo mema yanayompendeza Mungu. Hebu jichunguze na jithaminishe mbele za Mungu umemtenda dhambi mara ngapi na mara ngapi umemfanyia Mungu yaliyo mema. JICHUNGUZE MOYONI MWAKO kuwa umeruhusu MWILI kufanya yenye machukizo. hebu soma hapa: Warumi 12:1-2, Ni heri ufanye maamuzi sasa kwamba UNAUTAWALA MWILI WAKO NA SIO MWILI UKUTAWALE
 
Maneno kuntu
Btw in real life wewe ndo mama lwakatare?
 
Nisaidieni kutofautisha,mwili,nafsi,roho na akili nini tofauti yake na ni kipi haswa ukiache kikitawale?
 
Daaah asante kwa ujumbe lady furahia!
 
Last edited by a moderator:
Kumbe kuvuta cigara,kunywa pombe! Nazo ni dhambi!!
 
Mimi ni nani na mwili ni upi? Au nafsi ndio tofauti ya mimi na mwili?
 
nimeshakuwekea hapo kwani huna macho wewe au huoni ndugu manoah
 
Last edited by a moderator:
mkaka nazungumzia huo mwili wako unaoonekana ambao umeshikishwa na nafsi yako ambayo inaupeleka kufanya yaisiyompendeza Mungu hebu soma mada kwa makini ndipo utanielewa kama ujanielewa mwambie Ruttashobolwa akuelezee kwa kina ili uelewe Slave
 
Last edited by a moderator:
kumbe ulikuwa ujui ndugu yangu ndio ni dhambi na Mungu hapendi Yegoo
 
Last edited by a moderator:
umenisahau mm ni mama paroko ndugu sio mama lwakatare Bishanga
 
Last edited by a moderator:
mwili ni ule body yako nzima iliyojaa moyo, nafsi, roho na akili, sasa kinachozungumziwa hapa ni huo mwili wako ulio na nafsi (UTASHI) Roho (MOYO) na akili (UFAHAMU) vitu hivyo vyote vikiungamanishwa vinaleta neno MWILI hivyo ninaposema usitake mwili wako ukutawale nazungumzia vitu vyote hapo juu nilivyovitaja kwani bila kuwa na ufahamu (mawazo) huwezi kuwa na nafsi (utashi) na bila kuwa na roho hutaweza kushinda tamaa za mwili wako kwani jambo zuri au baya huanzia katika mawazo yako (ufahamu) kisha uteremka mpaka katika moyo wako na ndipo kitu kinazaliwa na kuumbika juu ya mwili wako NADHANI MPAKA HAPO UMENIELEW WEWE NA NWENGINE WALIOKUWA HAWAJUI ZAIDI nivea Ruttashobolwa
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom