Usisahau ulipotoka na nadhiri ulizoweka

LOVINTAH GYM

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
459
643
Kila mtu kabla hajapata kitu flani ambacho anakitamani kukipata huweka ahadi nyingi sana, na hata akiona mtu mwengine anacho basi humuona anakifanya vibaya.

Mara nyingi tunapenda kushinda, kiasi ya kwamba tunasahau malengo sio ushindi tu na kuna vitu muhimu zaidi ya ushindi.

Mfano:

Ukiwa unapanga bado huna uwezo wa kujenga, utakuwa unakereka labla mwenye nyumba wako anavyo ku treat, na kukunyanyasa.

Mara nyingi watu huweka ahadi kuwa Mungu akimjalia uwezo atakuwa baba mwenye nyumba poa sana.

Mungu hujibu maombi, ila wengi husahau na kujikuta wanarudia makosa yale yale.

Kwahiyo umeshinda kwamba na wewe umekuwa baba mwenye nyumba ila umesahau goal yako ilikuwa uwe baba mwenye nyumba bora.

Same thing, kabla hujapata kazi unaweka promise nyingi kuwa ukipata kazi basi utaifanya kiuaminifu, utakuwa unawai, utarizika na kidogo unachokipata na una focus kujifunza.

Ila ukishinda kupata kazi basi baada ya miezi michache unabweteka na kuanza kuchelewa kwenda officini, kuwa mlalamishi nk

Kuna msemo unasema ukisahau ulipotoka basi utapotea unapokwenda.

Winning is a fantastic feeling but never forget the goal, if you wanted to win an election and your goal was to create justice.. do that... do not forget the goal.

Una malengo ya kufungua shule nzuri, watoto wasome vizuri, kwasababu wewe uliteseka katika maisha yako ya shule.

Sasa baada ya kufanikiwa kufungua shule, unajikuta wewe ndio mnyonyaji, huwalipi walimu, wanafunzi unawalisha vibaya, unakataa kuchukua watoto ambao hawana uwezo a hutaki kuwapa nafasi, una focus kwenye ku maximize profit.

Ni kitu kizuri ila sadaka ni muhimu, chukua hata watoto 5 ambao ni yatima waweke kwenye shule yako wapate elimu.

Ukishinda usisahau malengo yako, ni rahisi kupotea na kupoteza vyote.

Kabla hujapata kazi, ulikuwa unaenda kanisani, unaenda kutembelea ndugu na kuomba baraka zao.

Baada ya kupata kazi uko busy, huna mda hata wakuwapigia simu , uliwaahidi utawajengea, ila umepata pesa yako imekuwa na ya Bar tu.

Hatumaanishi usijipende sema tu kama uliweka nadhiri jitahisi utimize.
 
Back
Top Bottom