Usiri wa Kamati za Rais kupendekeza uwazi wa Mikataba

Ni sahihi kwa mh rais kufanya hivyo kwa sababu baadhi yetu tunatafuta points za kupandia jukwaani kuanza kuyumbisha mchakato wa majadiliano. Ameona dalili za mamluki waliojidhihirisha tangu tume ya kwanza kutoa ripoti yake wakitafuta namna ya kuwasaidia Acacia waende mahakamani ili wao wapate political gain. Mh rais anaona mbali zaidi.
Sasa kama hivyo ndicho tofauti ya kamati hizi za jpm na wale maraisi waliotangulia ni nn?
Kwasababu hata wao walifanya siri hivi hivi anavyofanya yeye.
Ndio maana watu wanasema hakuna jipya hapo ni yaleyale tu!!!!!!
 
Mkuu hata marais waliopitisha hii mikataba leo tunayoambiwa ni ya wizi walisifiwa kwamba wanaona mbali. Na sifa kubwa ilikuwa ni huo unaoitwa usiri. Jiongeze jomba.
Nope. Usiishi kwa mazoea. Kwanza turejeshe uzalendo. Hivi Unaweza amini hata kwa hizi juhudi anazochukua mh rais wako waliojipambanua kusaidia wanyonyaji?
 
Nope. Usiishi kwa mazoea. Kwanza turejeshe uzalendo. Hivi Unaweza amini hata kwa hizi juhudi anazochukua mh rais wako waliojipambanua kusaidia wanyonyaji?

Mkuu kuishi kwa mazoea ndio huo usiri. Ilitakiwa kwenye hizi zama mpya tuachane na huo usiri maana ndio tulipoingizwa chaka.
 
Micha
Ni sahihi kwa mh rais kufanya hivyo kwa sababu baadhi yetu tunatafuta points za kupandia jukwaani kuanza kuyumbisha mchakato wa majadiliano. Ameona dalili za mamluki waliojidhihirisha tangu tume ya kwanza kutoa ripoti yake wakitafuta namna ya kuwasaidia Acacia waende mahakamani ili wao wapate political gain. Mh rais anaona mbali zaidi.[/
Mficha uchi hazai
 
Wakati ripoti zikisisitiza uwazi wa mikataba, Mikataba kupelekwa Bungeni na mengineyo, Wazalendo wamezuia ripoti yao kuwa wazi na kupelekwa bungeni. Hili linatia shaka juu ya uwazi wa Serikali na dhamira katika kuhakikisha Taifa linanufaika na rasilimali zake. Yaani kilichopelekea mabadiliko ya sheria hakifahamiki kwa kina kwa watunga Sheria
Ni utashi wa Rais kukufanya wewe uione hiyo ripoti
Rais ameridhia mapendekezo yote,unapatwa na wasiwasi wa nini
 
Watanzania! Ni kipi bora. Kupata sheria bora zinazoepuka aina zote za kuibia taifa ama bora ni kumlinda mtu. Mbona tunashindwa kujenga hoja kea ajili ya unafiki mwingi?
 
Sasa nimekubali kuwa Tundu Lissu was right alipowachana Serikali Bungeni kuwa ripoti zote 2 za Maparofesa Mruma na Osoro zilikuwa ni Professional RUBBISH!!!
Maneno hayo yana ukweli kwa 99.99% ndiyo maana Prof. Kabudi kasema hizo ripoti ni mali ya Magufuli tu na haziwezi kupelekwa Bungeni asilan maana ni TAKATAKA kwa kweeri!!!
 
Pale giza linapomlaumu nuru, usanii ni moja ya kipaumbele cha chama cha makinikia
 
Mkuu kuishi kwa mazoea ndio huo usiri. Ilitakiwa kwenye hizi zama mpya tuachane na huo usiri maana ndio tulipoingizwa chaka.
Mkuu uko sahihi kabisa. Tatizo wako wanasiasa wameonesha nia mbaya tangu mwanzo wa mchakato huu.
 
Mkuu uko sahihi kabisa. Tatizo wako wanasiasa wameonesha nia mbaya tangu mwanzo wa mchakato huu.

Kwa hiyo huo usiri unafanywa ili kuwanyima hao wanasiasa wenye nia mbaya hiyo ripoti? Huoni huko ni kama kuogopa kivuli chako?
 
Habari wadau, Nimeshtushwa sana na kitendo cha Waziri wa
Sheria na Katiba kudai kwamba Ripoti za Makinikia ni kwa ajili ya Rais, na hazitaweza kutolewa kwa kamati Ya Bunge, wala kwa Wawakilishi wa Wananchi. Suala la kungangania ripoti hizi kuwa siri ya Rais, wakati tayari umma ulishasomewa matokeo na mapendekezo ni jambo linalotia mashaka juu ya uhalali /ukweli wa kilichomo ndani yake.

Acacia ( Watuhumiwa Wezi) mara kadhaa wametilia shaka juu ya taarifa husika, na kuomba nakala za ripoti husika ili waweze kupitia details zilizopo na kutoa majibu lakini hawakupatiwa.

Wakati ripoti zikisisitiza uwazi wa mikataba, Mikataba kupelekwa Bungeni na mengineyo, Wazalendo wamezuia ripoti yao kuwa wazi na kupelekwa bungeni. Hili linatia shaka juu ya uwazi wa Serikali na dhamira katika kuhakikisha Taifa linanufaika na rasilimali zake. Yaani kilichopelekea mabadiliko ya sheria hakifahamiki kwa kina kwa watunga Sheria
Hata mimi nimestuka,kidogo,ila sio wazo baya.Of course kama reports zitakuwa released sasa ita-jeorpadize our negotiating strength and position wakati wa negotiations utakapo wadia kwa kuwa watajua nondo zetu.Hii itawafanya watujue,na kwa hiyo kuweza kujiandaa vizuri zaidi.Infact, hata negotiating team yetu inapaswa kuwa siri kubwa.Wasiijue kabisa.
 
Hao wananchi "wa Chadema" kama wanataka uwazi wapeleke hoja bungeni waunde kamati yao itakayopeleka majibu waziwazi bungeni bila kuacha kitu.
.... Dah Lumumba bwanaa hata Ndugai hamumuamini na yeye kumpa hizo ripoti? Kwani rais amewekwa madarakani na nani? Hizo ripoti ni kwa faida ya nani?
 
Habari wadau, Nimeshtushwa sana na kitendo cha Waziri wa Sheria na Katiba kudai kwamba Ripoti za Makinikia ni kwa ajili ya Rais, na hazitaweza kutolewa kwa kamati Ya Bunge, wala kwa Wawakilishi wa Wananchi. Suala la kungangania ripoti hizi kuwa siri ya Rais, wakati tayari umma ulishasomewa matokeo na mapendekezo ni jambo linalotia mashaka juu ya uhalali /ukweli wa kilichomo ndani yake.

Acacia ( Watuhumiwa Wezi) mara kadhaa wametilia shaka juu ya taarifa husika, na kuomba nakala za ripoti husika ili waweze kupitia details zilizopo na kutoa majibu lakini hawakupatiwa.

Wakati ripoti zikisisitiza uwazi wa mikataba, Mikataba kupelekwa Bungeni na mengineyo, Wazalendo wamezuia ripoti yao kuwa wazi na kupelekwa bungeni. Hili linatia shaka juu ya uwazi wa Serikali na dhamira katika kuhakikisha Taifa linanufaika na rasilimali zake. Yaani kilichopelekea mabadiliko ya sheria hakifahamiki kwa kina kwa watunga Sheria
Wewe mwenyewe hujitambui
 
Back
Top Bottom