Usipuuze jambo, na usiahirishe kila kitu

uzeebusara

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2013
Posts
657
Reaction score
514
USIPUUZE KILA KITU NA USIAHIRISHE KILA KITU

Mgonjwa mmoja aliyelazwa hospitalini alitembelewa na ndugu zake. Alikuwa amewekwa kwenye mashine ya oksijeni na hivyo hakuweza kuongea.

Wakati wakiwa pembezoni mwa kitanda, mgonjwa huyo alichukua kalamu na kipande cha karatasi akaandika ujumbe na kumpatia mmoja wa ndugu hao ambaye alikiweka mfuko bila kukisoma huku wakiendelea na mazungumzo.

Baada ya dakika chache, mgonjwa alifariki dunia. Ndugu yule aliingiza mkono mfukoni mwake ili kujua marehemu aliandika nini. Wajua nini kilichotokea? Kwa masikitiko ujumbe ule ulisomeka hivi:

“Tafadhali sogea pembeni kidogo, umekanyaga mpira wa oksijeni. Siwezi kupumua tena, unaniua”.

FUNZO:

Je, unaahirisha kusoma ujumbe? Je, unapuuza kupokea simu kwa sababu anayekupigia tayari wamjua? Huwenda ujumbe unaochelewa kuupokea ni muhimu kwako au kwa mtu mwingine ambaye yuko katika wakati mgumu.

Tafadhali pokea simu na usome ujumbe unaotumiwa. USIAHIRISHE KILA KITU.
1474475484249.png
 
View attachment 404447
Sawa lakini mfano wako aisee una kauongo
1.,akachukua kalamu
2. Akachukua karatasi
3. Akaandika
Akashindwa kutoa ishara ya sogea umekanyaga mpira wa oxygen ,
Any way late him Rest in peace
Muda
 
Daa jamani kumbe nimekosea sana, leo asubuhi sijapokea simu kisa anaepiga nimemzoea,ngoja nimtafute.R.I.P mgonjwa
 
Back
Top Bottom