Usipitie barabara ya Mandela Dar sasa hivi

Ndugu wana jf. sasa hivi barabara ya mandela kipande cha tazara kuelekea buguruni mpaka ubungo magari hayatembei nimasaa mawili sasa,inasemekana kuna kiongozi anataraiwa kupita nyerere road akitokea airport. tahadhari kwa waliobado kuingia kwenye barabara hii watafute njia mbadala.mchana mwema wadau.
Hakika mie nilipata taarifa mapema nimezungukia magomeni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Barabara zenyewe hazizidi hata 5 pia ni mbovu hata ukipewa taarifa bado hakuna alternative za kuchepuka therefore ni non sense.
Wahenga walisema "Mwanzo wa ngoma ni lele".

Hata kama barabara ni moja tu, kama habari hii itasaidia watu, ina maana.

Mitandao ya kijamii inatakiwa kutumika kuboresha maisha.

Tunaweza kukusanya uzoefu utakaosaidia hata kwenye mipango ya kuboresha barabara za miji.

Kama unaona jambo hili halina manufaa si lazima kushiriki. Ila usiwakatishe tamaa wanaoanza hata kwa kuzungumza tu.

Kuna mtu anaweza kuwa anataka kwenda airport kutoka Tabata akawa na uchaguzi wa kupitia Segerea au kupitia Mandela Road. Na Mandela Road kuna foleni itakayoweza kumchelewesha kupanda ndege yake. Mtu huyu ukimwambia Mandela Road ina foleni atajua kupitia Segerea na kuwahi ndege.

Hapo utasemaje barabara zenyewe hazizidi 5?

Mji mkubwa, si kila mtu anauangalia kama unavyouangalia wewe.

Zaidi, huu ni utamaduni wa kuboresha mambo kwa kushirikiana kijamii.

Hao viongozi wenyewe huenda wakuona watu wanazungumza haya mambo wataona umuhimu wa kubadilisha mambo.

Unakataa kitu hata kabla hakijaonekana kama kinafanya kazi au vipi kwa sababu isiyo na msingi, unajionyesha uko negative tu.

Sent from my Kimulimuli
 
Ni wakati muafaka sasa viongozi wakapokelewa na kupanda helcopter mpaka ikulu kuliko kuzuia shughuli zingine namna hiyo. Wachumi vip mbona hamuishauri serikali kwa hilo?
 
Wahenga walisema "Mwanzo wa ngoma ni lele".

Hata kama barabara ni moja tu, kama habari hii itasaidia watu, ina maana.

Mitandao ya kijamii inatakiwa kutumika kuboresha maisha.

Tunaweza kukusanya uzoefu utakaosaidia hata kwenye mipango ya kuboresha barabara za miji.

Kama unaona jambo hili halina manufaa si lazima kushiriki. Ila usiwakatishe tamaa wanaoanza hata kwa kuzungumza tu.

Sent from my Kimulimuli
Sina uwezo wa kumkatisha tamaa mtu alieamua jambo flan ukikata tamaa kisa flan kasema unaonekana ulikurupuka af Roads hazijengwi mitandaoni mainjinia wa barabaraba ndio wanadizain na kujenga roads mfano wengi wenu hizi rapid transit mmezionea hapa ndio mnakengeuka uko buguruni wataka enda airport unapita wapi kwenda huko zaid ya boda boda huoni mmechelewa kama Nchi kujenga Mji mkuu mnabaki mnaishi kwa Imani rais wenu anasema tumwombee sasa tumekuja kujenga nchi au kusali rais aendlee kutawala.?? Reality n kua ni aibu kwa nchi ya Tz kua hivi na bado mpo mpo tu hamna hata dira kama Taifa mfanye lipi na lipi kwa muda upi.?
 
MIMI NASHAURI IKULU IHAMIE DOM, NA MARAIS WATUE HUKO DOM NA NDEGE ZAO. DAR IBAK KUWA MJI WA BIASHARA
 
Sina uwezo wa kumkatisha tamaa mtu alieamua jambo flan ukikata tamaa kisa flan kasema unaonekana ulikurupuka af Roads hazijengwi mitandaoni mainjinia wa barabaraba ndio wanadizain na kujenga roads mfano wengi wenu hizi rapid transit mmezionea hapa ndio mnakengeuka uko buguruni wataka enda airport unapita wapi kwenda huko zaid ya boda boda huoni mmechelewa kama Nchi kujenga Mji mkuu mnabaki mnaishi kwa Imani rais wenu anasema tumwombee sasa tumekuja kujenga nchi au kusali rais aendlee kutawala.?? Reality n kua ni aibu kwa nchi ya Tz kua hivi na bado mpo mpo tu hamna hata dira kama Taifa mfanye lipi na lipi kwa muda upi.?

1. Huelewi kwamba maneno yanaumba na kuumbua.

2. Unajichanganya kwa kusema mainjinia wana design wakati hujui kwamba kila design inataka feedback kutoka kwa watumiaji ili kuboresha design itakayofuata na mitandao ya jamii ni sehemu moja ya kutoa feedback kwa designers.

3.Umejikita sana kuongea habari za transit "mmezionea hapa Buguruni" "rais wenu" "bado mpo mpo tu" wewe umejitenga. Sasa kama umejitenga hivyo, kwa nini unachangia habari hizi? Kwa nini usifie huko uliko kimya kimya?

4. Unaniambia nimeona haya mambo Buguruni wakati hunijui, hujui nakaa wapi, hujui nimetembea miji mingapi duniani na hujui hapo Minazi Mirefu na Buguruni sijakanyaga miaka mingapi.

Unajionyesha ujinga wako wa ulimbukeni wako ku assume tu kwamba kwa sababu kijijini kwenu wewe peke yako ndiye uliyeona vitu vilivyozidi Buguruni, basi kila mtu yupo Buguruni.

Wakati wengine tupo at the center of the galaxy huku.

Acha ulimbukeni.

Usifikiri kila mtu yuko kwenye pango kama ndugu zako kijijini kwenu huko.

Acha kusema mambo kwa chuki tu bila kutumia akili.

Watu wakianzisha thread ya kuhabarishana barabara gani ina foleni wewe utapungukiwa nini?

Sent from my Kimulimuli
 
Hakika mie nilipata taarifa mapema nimezungukia magomeni

Sent using Jamii Forums mobile app
Nilikua maeneo ya kurasini. Ile natoka kufika Serengeti,nikakuta lori kama sisimizi. Nikasema kwa kuwa naenda Tabata,basi ngoja nipite hata ya kigogo kwa kupitia Kawawa maana ile ya Tazara ilikua haiwezekani. Ile naenda Keko,nikakuta haitembei kuanzia Bora. Likanijia wazo la kupitia route ndefu ya Yombo-Buza,na kwa kweli hiyo imenisaidia sana. Vinginevyo,hata kama msafara wa Waheshimiwa utakua umeshapita,lakini itachukua muda sana kuimaliza foleni ya leo kwa njia kuu za Mandela na Nyerere Road. Kwa wakaz waishio aina yoyote ya Tabata kama uko TMK basi pita njia ya Buza au Mchicha. Kwa walioko mjini wapite ya Kigogo kwenda Dampo au kwenda Xternal,angalau unaweza kuokoa muda wa foleni.
 
1. Huelewi kwamba maneno yanaumba na kuumbua.

2. Unajichanganya kwa kusema mainjinia wana design wakati hujui kwamba kila design inataka feednack kutoka kwa watumiaji ili kuboresha design itakayofuata na mitandao ya jamii ni sehemu moja ya kutoa feedback kwa designers.

3.Umejikita sana kuongea habari za transit "mmezionea hapa Buguruni" "rais wenu" "bado mpo mpo tu" wewe umejitenga. Sasa kama umejitenga hivyo, kwa nini unachangia habari hizi? Kwa nini usifie huko uliko kimya kimya?

4. Unaniambia nimeona haya mambo Buguruni wakati hunijui, hujui nakaa wapi, hujui nimetembea miji mingapi duniani na hujui hapo Minazi Mirefu na Buguruni sijakanyaga miaka mingapi.

Unajionyesha ujinga wako wa ulimbukeni wako ku assume tu kwamba kwa sababu kijijini kwenu wewe peke yako ndiye uliyeona vitu vilivyozidi Buguruni, basi kila mtu yupo Buguruni.

Wakati wengine tupo at the center of the galaxy huku.

Acha ulimbukeni.

Usifikiri kila mtu yuko kwenye pango kama ndugu zako kijijini kwenu huko.

Acha kusema mambo kwa chuki tu bila kutumia akili.

Watu wakianzisha thread ya kuhabarishana barabara gani ina foleni wewe utapungukiwa nini?

Sent from my Kimulimuli

Nakujibu mwishoni hapo we ku reply hii comment angu umepungukiwa au kuongezewa nin..???? kule juu sikujibu maana ujaelewa nilichoandika na ukajibu kwa povu kuni attack personal mara kwetu mara sijui umetembea
Miji mingapi mara sijui kijijin Dont panic Mr. Vijimambo tu hivi. Be cool.
 
Wewe nenda elimu ya ngumbaru ujue kuandikaKiswahili ujue kwamba "ujaelewa" si neno sahihi la Kiswahili, neno sahihi ni "hujaelewa".

Ukiweza kuandika Kiswahili sahihi, labda tutaelewana.

Kujibu comment yako nimeongezea jamii watu wanaopinga ujinga.

Wewe unakumbatia ujinga.

Kuna tatizo. Tatizoni foleni za barabarani. Tatizo hili linaletwa na ujinga wa kutojua vipi tuepuke foleni za barabarani.

Mtu katoa wazo la kuanzia tu, kwamba tuwe na thread ya kuhabarishana wapi kuna foleni ili tupaepuke.

Wewe unapinga wazo litakaloondoa ujinga wa kutojua wapi kuna foleni ili watu wapaepuke.

Unapinga wazo la kuondoa ujinga.

Unakumbatia ujinga.

Wewe ni mjinga.

Na mimi napinga ujinga wako.

Naendeleza utamaduni wa kupinga ujinga.

Ndicho nilichoongeza.

Sitaki ujinga.

Sema jingine.
 
Nilikua maeneo ya kurasini. Ile natoka kufika Serengeti,nikakuta lori kama sisimizi. Nikasema kwa kuwa naenda Tabata,basi ngoja nipite hata ya kigogo kwa kupitia Kawawa maana ile ya Tazara ilikua haiwezekani. Ile naenda Keko,nikakuta haitembei kuanzia Bora. Likanijia wazo la kupitia route ndefu ya Yombo-Buza,na kwa kweli hiyo imenisaidia sana. Vinginevyo,hata kama msafara wa Waheshimiwa utakua umeshapita,lakini itachukua muda sana kuimaliza foleni ya leo kwa njia kuu za Mandela na Nyerere Road. Kwa wakaz waishio aina yoyote ya Tabata kama uko TMK basi pita njia ya Buza au Mchicha. Kwa walioko mjini wapite ya Kigogo kwenda Dampo au kwenda Xternal,angalau unaweza kuokoa muda wa foleni.
Halafu kuna mjinga mmoja Jestkilla atakwambia "barabara zenyewe tano tu mnataka kuhabarishana ili iweje?".

Watu wana ulimbukeni fulani hivi wakishatoka nje ya Tanzania tu wanajiona kamawamefika mbinguni wanaleta post za chuki ya kuchukia kwao wenyewe bila hata ya kuwa na kiasi.

Watu tumekaa viwanja vikubwa barabara zina lane nane nane na kupandiana kama meanders za Mekong, lakini ikija kwenye kutoa mchango wa mawazo kuhusu kuboresha mambo nyumbani hatuwezi kuendeleza ulimbukeni wa chuki za kijinga.

Jamaa ameonyesha ulimbukeni wa hali ya juu.
 
Ndugu wana jf. sasa hivi barabara ya mandela kipande cha tazara kuelekea buguruni mpaka ubungo magari hayatembei nimasaa mawili sasa,inasemekana kuna kiongozi anataraiwa kupita nyerere road akitokea airport. tahadhari kwa waliobado kuingia kwenye barabara hii watafute njia mbadala.mchana mwema wadau.
Siyo kiongozi anapita mvua ikinyesha traffic waliondoka kwenye mkutano ya barabarani ndivyo inavyokuwa, hata ma driver wa Dar wanaogopa sana mvua.
 
Ukiweka sticky watu wengi huwa hawasomi mfano ni mimi mwenyewe hapa, ni mara chache sana kusoma sticky kwa mwaka mzima
Sijasema sticky. Nimesema thread.

Thread ikiwa nzuri na ina crowd participation itapaa yenyewe tu.

Kuweka sticky ni kama kuipaisha thread kwa nguvu. Vitu vya kupaishwa kwa nguvu huwa sivishabikii.
 
Barabara zenyewe ni;
1. Mandela
2. Morogoro
3. Nyerere
4. Uhuru
5. Ali Hassan Mwinyi
6. Kawawa
7. Bagamoyo

Kuwe na thread ya kuhabarishana hizi foleni manake leo hali ni mbaya sana.
 
16 Reactions
Reply
Back
Top Bottom