Hili ni tukio ambalo limenitokea live hapa mtaani kwetu.
Hapa ninapoishi mtaani japo nina muda kidogo tangu nihamie, sijaweza kujichanganya sana kiasi cha kufahamiana na watu wengi kivile Ukizingatia mara nyingi niko busy sana, so nafahamiana na watu taratibu sana, japo wengi tunafahamiana japo kwa sura. Sasa kuna duka huwa naenda kuchukua baadhi ya mahitaji ila huwa nawakuta wauzaji wawili au watatu ambao wanapeana shift.
Sasa majuzi nilifika hapo kununua bidhaa, nikawakuta wawili kwa pamoja. Nikahitaji kununua bidhaa ambayo mimi nilijua bei ni 5000 tu kwa uzoefu wa maduka mengine. Nilipofika wakaniambia 5,500/-.Basi tukabishania bei, baadaye nikatumia kigezo cha kusema nina 5000 tu niuzie. Muuzaji alinitazama kwa jeuri flani akaniambia "kama unanunua sema bana la sivyo niendelee na ratiba zangu, mwanaume gani ww usiyetembea na hela ya ziada". Akaondoka akaingia mlango wa ndani, mara kidogo akatoka akiwa na sahani ya chakula (wali maharage). Akaanza kula. Mwenzake alikuwa ameshatangulia kuchukua chakula anatuangalia tunavyobishana tu anaendelea kula.
Ile kauli iliniudhi sana. Nikawaza nikiondoka nitakuwa nimekubali udhalilishaji mkubwa kiasi kile. Lakini pia sikutaka kumjibu neno lolote, maana nilihisi ana stress zake tu ambazo hata sijui ana shida gani. Nakumbuka kwenye mfuko wa shati nilikuwa na hela ndogo ndogo zinazofikia elf 12, mchanganyiko wa buku 1, 2 na 5. Mfuko mmoja wa suruali nilikuwa na silver za 500 kama tatu hivi, na mfuko mwingine nilikuwa na Tsh laki 5 ambazo ndo nilikuwa natoka benk kuzidraw. Zile laki 5 zilikuwa noti za elf 5 tuu, mpya kabisa zimefungwa na ile karatasi special ya benk. noti zimenyooka utadhani zimepigwa pasi.
Nikaamua kulipiza kisasi cha kumsambaratisha yule dada kisaikolojia. sikutaka hata kutoa noti ndogo ndogo ambazo ni chenji kamili maana ingetosha. Nikazamisha mkono mfukoni, nikatoa zile laki 5, nikawa navuta noti taratiiiiiiibu, nikachomoa elfu 5 ya kwanza baadaye ya pili, nikazishika mkononi huku nikimuagiza anipatie bidhaa husika. Huwezi kuamini alishindwa kabisa kuniangalia usoni, akawa anaangalia chini tuu na pembeni. Mwenzake akawa anamcheka akamwambia leo umepatikana siyo kwa kunyooshwa huko. Kwa kweli alishindwa kuja kunihudumia ikabidi yule rafiki yake ndo aje anihudumie. Aliyenihudumia akawa anacheka huku ananisemesha semesha, sikuwa na time kabisa. Niliporudishiwa chenji nikatoka, nikaingia duka la pili wanauza soda nnikalipia soda mbili, nikamwambia mhudumu apeleke kwa wale wadada, nikasepa zangu nisijue yaliyoendelea nyuma ya pazia.
Baada ya wiki hivi nikiwa nakatiza chochoro flani za uswazi, nikasikia mtu ananiita nyuma yangu, "kaka samahani", kugeuka nikaona ni yule ambaye alinihudumia (huyu wa pili). Nilikuwa sijamkariri vizuri sura na hata jina simjui, kaikabidi kuulizana na kufahamiana, ndo akanikumbushia lile tukio. Kwa kuwa tulikuwa tunaenda mwelekeo mmoja, tukapiga story mbili tatu, tukapeana namba kabla hatujaachana.
Baada ya kupeana namba mnajua kilichoendelea?
Subiri part 2