Usiombee kutendwa

Pole. Ilishanitokeaga had chakula hakipand. Ila JF ilinisaidia kusoma mikasa ya wengne..bada ya muda mchache tu maisha yakarud normal...ni ngumu ila inaishaga..
 
Haya maandiko yako yamenifunza sanaa,kila kitu fanya kwa kiasi,nikitendwa mm ambaye nishasoma mchezo maumivu n tofaut na ww uliye deep down.hawa viumbe c wa kwenda mzma mzmw,wakishajua unawapenda bac ndo huanza visa wakidhan utaomba msamaha tu.
Noma sana
 
Fanya maisha yako kwani huyo sio mzazi wako useme huwezi muacha
 
Wengi wenu mnapata tabu kwa vile mlikuwa na expectations kuubwa,hii hutokea hasa kwa vijana kwa vile awali hukuwahi kujua saikolojia hasa ya mwanamke
Binafsi nilichojifunza kwa miaka hii nimeishi duniani ni kwamba usiwe na matarajio chanya tuu kwa kitu chochote kwenye maisha wewe jua tu kwamba Jambo lolite unalolifanya kwa malengo chanya Basi jua Kuna hasi yake pia.Hii itakusaidia kujiandaa kisaikolojia kuhimili pindi hasi ikitokea ili usipotee kwenye reli yaani uwe na huzuni inayohimilika na kuganga yajayo,ukizaa watoto kwa mfano jua pia wanaweza wakafariki au wakaugua au ukabahatika wakawa vizuri
Ukioa wewe jua inaweza tokea ukawa cheated nk so jiandae kisaikolojia kwa Jambo lolote hasi kwenye maisha ,kuishi kwenye nadharia ya perfection,rightness na positive response mda wote ni mbaya lazima utatoka kwenye reli,utakata tamaa na inaweza pata stroke kwa heart attack
 
Ni kweli mkuu kitu kikubwa cha kukilinda kwa sala,maarifa na juhudi zingine za kibinadamu ni afya ya mwili na akili,hayo mengine yanahimilika hata upoteze kila kitu kuanzia watoto,mali au kazi utapambana lakini pia omba hayo yasikufike uzeeni hasa la kupoteza Mali kwenye umri ambao mwili hauna tena nguvu na maarifa ya kutafuta ,utalia Zaid ya maombolezo ya Daudi wa kwenye Bible.
 
Nimeona hakuna aliyekushauri uchukue dose, hayo maumivu unayopata ni Moto na dawa yake ni moto. Ruhusu macho yakupe mwenza mwingine (hata kama awe rafiki wa muda, tumia bima ya afya ya mwili), kila ukimkumbuka aliyekutosa, waza kupata dose, omba dose, siku so nyingi, upo huru. Akiba ni muhimu, usiitupe hiyo dose.
 
Kiufupi nitalia kwa mengine sio mapenzi, niliwah umia na kutetemeka mwili kwa mapenzi back in 2010s huko kuanzia hapo nilijifunza kupenda kwa kutumia akili na sio moyo tena Hadi Leo nimeoa mwendo ni huo huo.
Angalizo na tahadhari,kupenda kwa kutumia akili kutakufanya uone makosa zaidi kwa mwenzio na unaweza kuwa mkatili so jitahidi ku balance na hakikisha mwanamke unaempata ni yule anaeweza vumilia Hali hiyo,usijesema sijakutambua Ila hii njia haitakuja kukumiiza maana umeshajenga saikolojia ya lolote laweza kutokea na uko tayari.Faida ya njia hii ni kufocus kwenye mambo ya msingi ya familia kuliko kuwaza kuridhishana kwa kusimamia kucha kwenye mapenzi
 
Ukiona Giza limeongezeka usiku,ujue ni karibu na mapambazuko.Mungu ni wa rehema na hajawahi kukuacha Wala kukusahau kamwe,hivo jiandae kupata kilicho bora zaidi kuliko ulichokipoteza, pole sana ndg.
 
Mkuu kwani ulimsomesha?Kama ulimsomesha imekula kwako maana mchumba hatugharamii siku hizi...labda awe mke tu
 
Point
 
Mkuu kwani ulimsomesha?Kama ulimsomesha imekula kwako maana mchumba hatugharamii siku hizi...labda awe mke tu
Sijamsomesha hata, nilikuwa nae katika mahusiano ila nilijifunza kumuamini , nikamuamini sana kwamba atakuwa wangu!! Daah kilichotokea kumbe akiwa na mimi kuna jamaa walikuwa wanafaidi kijanja bila mimi kujua . Ila kutokana na kumwamini sikufahamu hilo , badae nikaamua kufanya mambo ya (BLACK MAGIC )
Kwenye kasimu kake loooooh nilichoka sana.

Watu wanalipa mpaka kodi ya nyumba , na mambo mengine ukicheki nilikuwa na malengo nae sana ila kwasasa nimebakia mtazamaji tu , japo ukweli naujua ila sijamwambia nimeamua kunyamaza , nayeye ananichora tu anajua sifahamu kitu
 
Pole Sana mkuu...ilishanitokea....ila muda ni mwamuzi mkubwa Sana nilishamsahau
 
Nothing sucks forever in life, be strong bro.

Nalo litapita tu.
 
Acha kulialia wewe mtoto wa kiume bwana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…