Usiombee kukosa hela

Bora sisi wanaume. Wanawake wanakuwa mara mbili yetu.Ngoja waje kusimulia yao.

Kuna kipindi Unakuta mwanamke mzuri hatongozwi wala kupewa salamu miezi.Hapo unakuta kila kitu ndani kwake kimeisha nywele zimeoteana tumbo la period linamsumbua.Hana hata mia madeni kibao.
 
Bora wewe mtoto unamsomesha huku ukimwandaa kuwa jeshi la akiba! maisha hayatamgonga sana kwa kuwa kwa kiasi fulani anauzoefu wa kujitegemea! kwa shule hiyo lazima aende na kuni, ufagio, na hela ya mihogo!
hivyo hata akiwa na familia atajua lazima nirudi nyumbani nikiwa na kitu na hata akienda kusalimia atajua mikono mitupu hailambwi
 
Aisee mkuu Mungu yupo anaweza asikujibu kwa wakati ila tusikate tamaa, naonaga nina shida sana na niko kibachela sasa nikiwa na family sijui itakuaje anyway naomba ujana wangu upite salama niendelee kujipanga, Mungu yupo bwana..
 
Kuna siku nimeingia mwendokasi nikadondosha sarafu ya 200 ikiwa inaondoka jamaa mmoja na mama mmoja waliigombania 200 utadhan milioni.

Jamani maisha magumu.
Yaani ni vile moyo wa mtu kichaka hatujui lililopo laiti kama ingekuwa unaona moyo wa mwenzio maswaibu anayopitia katika maisha haya tungekuwa watu wa uzuni sana
 
tena hao wafanyakazi ndio wakuonewa huruma, mimi huku nilipofikia kwenye utafutaji, kuna brother nilikutana nae yeye ni mwalimu wa primary akawa anasema dogo mimi naacha kazi kumuuliza anasema toka aanze kazi ajapandishwa daraja wala mshahara ni mtu wa madeni, anaachukua deni la huku anaamisha kule mshahara laki nusu ameoa na ana watoto wawili, plus kapanga aiseee alikuwa mtu wa kulalama muda wote mwezi mzima mtu anasubiria 150k dah na yuko na family bado kwao waombe hela maana wao wanajua mtoto ameajiriwa bado ukweni yaani taabu!
 
Umenikumbusha kipindi flani ivi bado dogo sikumbuki ni mwaka gani ila nilikuwa bado shule ya msingi.nilizinguana na mshua nikasepa nyumbani kimbilio lilikuwa ni kwenda kwa bibi.kwa bibi ni mbali kidogo ni zaidi ya km 10 kwa wale wanaoishi kijijini watakubaliana na mimi km 10 kutembea ni kawaida sana.nimefika kwa bibi jioni na haikuwa kawaida mimi kwenda ule muda tena bila kutumwa.huwezi amini bibi alinifukuza nirudi home kipindi hicho vijijini cm ni adimu so kulikuwa hamna hata njia ya kumpigia aidha baba au mama kujua kulikoni.nilizuridi nyumbani ndani siwezi kuingia nikaenda nyuma ya choo nikajiegesha nikalala asubuhi nimewahi kuamka nina njaa ya hatari natamani kula hata udogo wakati nawaza huku naenda nisipo pajua gafla kwa mbele nikaona not ya elfu 2 .kwanza niliiokota ile hela afu nikapiga magoti pale pale bara barani nikasali na kumshukuru mungu.nikaenda dukani nikanunua mandazi na mbege chibuku moja mimi ni mchaga nikasingizia nimetumwa na mama ya kwenda nayo shambani.wachaga wataelewa hapa.nikala mandazi na mbege yangu nikashiba afu ndo nikaenda home kupokea kipigo kwa mshua sasa.hapo ni jioni ndo nilienda home
 
"Waziri Mkuu ameliomba Bunge liidhinishe TZS bilioni 116.8 kwa ajili ya Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zilizo chini yake kwa matumizi ya mwaka 2021/2022. Kati ya fedha hizo TZS bilioni 93.3 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na TZS bilioni 23.5 ni kwa ajili ya maendeleo", Mwisho wa kunukuu.

Mchawi wa maendeleo yenu ni CCM, siku mkipata akili ya KUWAFURUSHA madarakani mambo yatakuwa sawa.
 
Kwahyo unaamini tunaishi kwa migongo ya wanaume ..kwamba usipitongozwa wewe ndo basi .duh...sikia ..kati ya wanawake na wanaume sisi sifa yetu kuu tuna uthubutu kuwashinda nyie...nyie mnakufa na tai ..sisi hatuna aibu..yes wako wenye aibu lakini njaa ikikushika hata beki 3 unafanya maisha yasonge
 
nakubaliana na wewe 100% na nyie mkiamua kuweka aibu pembeni ni balaa mnatusua chap kwa haraka pia kusaidika kwa upande wenu ni rahisi mno maana mu wapole na hamna tabia mbaya, nilishawahi kukosa kazi Mwanza kwa ajiri tu ya kuwa mimi ni mwanaume yaani kazi ya professional yangu kabisa ila walinikataa wakasema wanaume hamuamiki mnakula rushwa sana mtaichoma taasisi, nikitamani niwe mdada shida hizi dah
 

Alipoingia Hayati wa Africa ike sekeseke la vyeti bas mume wangu akasimamishwa kazi...ikaonekama cheti cha form 4 jina la kati kati likawa tofaut na cheti cha chuo...wakamsimamisha bila payment kwa 3mths..alidata..mie skudata...bas nikajikuta naenda mawenzi nikanunua matunda meengi embe ng'ong'o zile nilinunua kama za 9000.nikazitengeneza juic...asbh nikaenda nayo juic job...bas haikukaa hata masaa ikaisha..bas ikawa ndo kaz yangu jaman Mungu alinishika mkono niliuza juic bila aibu..yaan nikawa napata shiling kwa shiling ..yaan hom narudi na faida nene...wakawa wanaishobokea balaa😅! Lakin mwenzang alijikunyataaa....nilimtoa balaa....ila nyir mna aibuu..sijui tu
 
Linauhusiano gani na maada

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
 
mzee shida ya kupika mwenyewe huwa ni gharama kushinda hata kwenda kula mgahawani ugali wa buku jelo
 
Hongera zake amepata mke anajitambua, sisi bhanha aibu sana haswa ile nitaonekanaje na nini.. ila kwa upande wangu yaani kazi yoyote halali nafanya bila hiyana kikubwa iwe halali tu hata kubeba mizigo yaani nimeamua liwalo na liwe vyeti viko home tu dar mimi nipo napambana huku Moro
 
Hee....kumbe tuko mji mmoja...kaza mkuu..so una mishe gan
 
Kuepukana na hayo, fanya urafiki na makampuni ya Simu, haswa TIGO NA AIRTEL hawa ukienda nao vizuri hupati tabu, ukichacha laki 3, 5 wanakukopesha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…