Usiombe yakukute jamani, daah!!!

Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote, una ugonjwa wa kufisha; nani awezaye kuujua?

Ufunuo wa yohana : Mlango 2:22 Tazama, nitamtupa juu ya kitanda, na hao wazinio pamoja naye, wapate dhiki kubwa wasipotubia matendo yake.

Mithali : Mlango 6:32 Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa;Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake.

Awali ni awali hakuna awali hakuna awali mbovu.. hapa ndipo nilipogundua wanaume wengi kwanini tunakufa mapema.. kwenye hii issue mkuu nimegundua yafuatayo..

Ni Mvivu wa kufikiri ama kukishughulisha kichwa cha juu ambacho ndicho chenye ufahamu na utashi.. kichwa hiki kama ungekishirikisha vzr naamini kabisa leo tusingekuwa tunazungumza haya mambo kwa ukubwa huu..

Pia hakikisha siku zote unapoanzisha mahusiano na mtu umejitafakari vya kutosha? Na je upo tayari kwa changamoto za mbeleni.. jipime mzee baba usiache tamaa zikuendeshe kwenye maamuzi ya msingi.. hapa kumbuka moyo huwa mdanganyifu kama nilivyosema hapo awali.

Tatu unapokuwa kwenye miji ya watu acha papara mzee baba.. fanya fisibilty study then yazoe mazingira kwanza..

Kumbuka kwa maelezo yako hujatueleza ubaya wowote wa mwanamke wako wa singida isipokuwa nafsi yako inakiri kumtenda vibaya mzazi mwenzio..

Moyo wako umefungwa kwenye zinaa, umeiuza nafsi yako mwenyewe!.

Then mimi naona hata kama utaharmonize hiyo situation, maswali ya msingi na ya kujiuliza ni haya..

Kwanini amwage damu kwa kujikata?
Damu hii ina maana gani?
Nini tafsiri ya damu tena ya mtu?

Anza kutafuta njia mapema ya kuiponya nafsi yako hao wa kumwaga damu hata ukiachana naye ujue haupo salama mana kiwanja ulichoingia sicho mkuu..
Huyo akijiua ujue ndugu zake watajua umemfanyia chezo ukoo utakukalia kikao..
 
Mkuu umenigusa sana,sana sanaaa!!!
Moyo wangu umesononeka sana,na tafakuri ya suluhu inazidi kuwa complex sana!
 
Jamani,naomba kuleta mrejesho wa maswahibu yangu!

Baada ya co-worker kujikata mkono kama jaribio la kujitoa uhai wake,nilisitisha safari ya Singida.
Lakini baada ya wiki moja niliamua kutengeneza dharura ya uongo kwa kumpanga rafiki yangu anipigie simu kunipa taarifa kuwa nahitajika kwetu haraka sana!(kwetu ni mkoani)

Basi jioni moja tukiwa tunaongea (huku nikiwa na hasira sana,japo sikutaka ajue),jamaa yangu akanipigia simu,akijifanya kaka yangu,akanambia nijitahidi ndani ya siku mbili nifike nyumbani kuna mambo muhimu yanahitaji uwepo wangu.

Baada ya kumaliza mazungumzo ya simu nikamwambia huyu mpnz wangu kuwa ninahitajika nyumbani haraka,inabidi kesho nipande gari kuelekea nyumbani,hakutia shaka!

Asubuhi ya siku iliyofuata nikapanda gari kuelekea Singida kwa mama watoto wangu.

Nimefika Singida,nikakuta familia yangu ikiwa poa kabisa,nikajisemea moyoni,huyu mwanamke (wa Tanga) anataka kuniharibia familia yangu hakika,kila nikiwaangalia wanangu wanavyofurahia uwepo wangu,na vizawadi kidogo nilivyowabebea nikajisemea hakika sitakubali kuiharibu familia yangu!

Usiku wa saa tano hivi nimelala na mke wangu,sijui shetani gani alinituma kushika simu ya mke wangu,nikaichukua nikaenda sebuleni,(yeye akiwa amelala baada ya game),kufungua inbox yake,loooh!nakuta SMS za wanaume kama 4 hivi,wote wanaonyesha wame-date naye,kwa sababu kila mmoja anasifia kuhusiana na mapenzi aliyopewa!
Mmoja ameandika," Bby una K ya moto sio mchezo,natamani iwe kila siku"

Mwingine,"Kwa ulivyokuwa mtamu,ungekuwa hauna mume ningekuoa kabisa"

Baada ya hapo nikajikuta najawa na hasira mbaya,ukizingatia si mtu niliyempenda ila nililazimika kuweka maslahi yangu kando ili kulinda maslahi ya watoto wetu,(maana bila watoto kiukweli tusingekuwa pamoja mpaka sasa)

Nimeendelea kuwepo mpaka sasa,na Alhamis natarajia kurejea Tanga,ila nina hasira moyoni isiyokifani,mbaya zaidi,kila nikisoma sent items zake kwa hao jamaa,naona anaonyesha ushirikiano chanya kwao!

Kimoyo moyo nawaza nikiondoka nimpotezee moja kwa moja,maana hata hamasa ya kusex naye sina kabisa!!

Nafikiria kuachana na wote nianze upya,(maana wa Tanga nampenda lakini kwa kiasi fulani naona hanifai kuwa mke) japo najiuliza ni mwanamke gani atakayenielewa kuwa nina watoto 3 na aishi nami na kuwapenda hao watoto wangu!!!???
Ushauri zaidi jamani,vijana wenzangu epuka sana kuanzisha mahusiano na mfanyakazi mwenzako,hasa kama hauna mpango wa kumuoa,ni hatari!!
 
Hakika tunaendelea kupata funzo la kutosha humu JF

Ila mkuu hujatuambia baada y kumzalisha huyu demu wa Tanga vp khs yule wa singida alijua hili? na alilipokea vp maana alikuwa anajua ni rafk yako tu wkt anakuja pale Tanga
 
Hakika tunaendelea kupata funzo la kutosha humu JF

Ila mkuu hujatuambia baada y kumzalisha huyu demu wa Tanga vp khs yule wa singida alijua hili? na alilipokea vp maana alikuwa anajua ni rafk yako tu wkt anakuja pale Tanga
Nilipoenda hii juzi ndo nilipanga kuongea naye kwa utulivu sana,lakini baada ya kuona usaliti niliouelezea hapo juu hakika sijaweza kumwambia chochote!
 
Kama amethubutu kujichinja mwenyewe basi jua wazi kuwa ana uwezo pia wa kukufanyia hilo jambo muda wowote akitaka. Na siku ukisema umuache, kwake kujiua ni zoezi la dakika sifuri tu. Upande wa ushauri, sijui hata nikushaurije mana hata nikikushauri uhame unaweza ukasikia ameshajiua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…