Usiombe hivi vitu viwili (2) vikutokee katika maisha yako

Usiombe hivi vitu viwili (2) vikutokee katika maisha yako

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
40,710
Reaction score
63,393
Usiombe hivi vitu viwili (2) vikutokee katika maisha yako;-
  • Maradhi ya muda mrefu
  • Kesi mahakamani
Hivyo vyote viwili, vinamaliza pesa na vinapoteza muda; vinaweza vikakubadilisha ndani ya muda mfupi ukawa masikini/fukara.

Na ni mazingira ambayo yatakutambulisha rafiki wa kweli ni yupi, pamoja na mkulungwa ni yupi? Ingawa wakulungwa ni wengi zaidi.

Ule muda wa kufanya uzalishaji unakuwa haupo, na kidogo ulichokikusanya kinaishia huko kwenye kupambana na kesi au maradhi.

Wengi wanaoyapitia haya wanakuwa kama wamechanganyikiwa, na wakati mwingine jamii inawatelekeza.
 
Kweli kabisa usemayo......yaani ni bora ukose pesa ubaki na afya yako......Ila yote kwa yote Mwenyezi Mungu ndio wakuombwa tu katika majambo yote katika maisha yetu
Vinatesa sana
 
Nilikuwa Gerezani toka mwezi wa 12/2020 na nilitoka 9/2021 nakuelewa ulichosema. Bibilia imeamdika Dini Safi ni kutazama wagonjwa na wafungwa/mahabusu magerezani inamaana yake.

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
Ni kweli mkuu, na kama unataka ujifunze kuwa na utu, tembelea; wafungwa, yatima, na wagonjwa
 
Back
Top Bottom