Usiogope wanavyomshangilia

"The challenge of leadership is to be strong, but not rude; be kind, but not weak; be bold, but not bully; be thoughtful, but not lazy; be humble, but not timid; be proud, but not arrogant; have humor, but without folly." - Jim Rohn
 
Tuombe Mungu tusifike huko........maana visa vya Iddi Amin jamani sikieni tu, msiombe kuona.
 
Nikweli sikuwahi kuongea privately na Major General Silas Mayunga ingawa nilimfahamu mara tu alipoteuliwa kua katibu wa CCM mkoa wa Kilimanjaro na mimi nilikua mkoani humo tukafamiana kwa kawaida tu. Ni kweli pia alikua 'mtata' ( yaani mtamaduni hasaa, nadhani naeleweka).
Lakini hapa sasa tukubaliane kutokukubaliana. Inawezekana uliongea nae privately akakwambia alivokwambia na inawezekana pia ikawa ni kweli, lakini kwa namna hiyo watu tumeambiwa meengi sana kuhusu viongozi wetu. Kuna kiongozi mmoja aliwahi kunambia privately kua kiongozi mmoja hapa nchini alisaini hati chache sana za watu waliohukumiwa kunyongwa ili hukumu hiyo itekelezwe juu yao. Kwamba alikua haipendi hukumu ya kifo! Lakini jamaa akanambia kiongozi huyo alipoteza na kauwa watu wengi sana kimyakimya na akatoa maelezo meengi sana! Mimi mpaka leo sijamuamini na siwezi kumuamini sababu sikuweza wala sikua na namna ya kuthibitisha, niliona ni porojo tu
Nakubaliana na wewe pia vitani kuna ukatili wa ajabu sana na wakinyama hasa! Lakini hiyo ndio vita, ukishasema vitani basi hakuna ubinaadamu na uongo pia unakua mwingi kwakweli na Mungu Atuepushe na vita, ila sasa propaganda zinazoendeshwa ni mbinu za kummaliza adui
 
wewe bwana mwongo nchi za magharibi hazikumchukia Amin mana zilimwona ndiye haswaa angeweza kupambana na Nyerere mcomunisti na ndo maana Uingereza ilimsaidia pia wakati wa vita ya Kagera
Nchi za Magharibi hazikumchukia Amini!? U need to read and research more. Support gani Uingereza ilitoa kwa Uganda wakati ule? Kama ni msaada labda waliwauzia silaha kama mabeberu wafanyavyo popote kwenye vita, pande zote zinazopigana zinaweza kuuziwa silaha na kampuni moja. Kwa taarifa yako pamoja na tofauti za kiitikadi kati ya Tanzania ya Nyerere na nchi za Magharibi walikua wakimheshimu sana sana Mwalimu na hawakujiunga na Amini kuipiga Tanzania
 
mkuu...wacha watu waendelee kumkenulia meno ngedere.

yatakapoanza kuwasibu ndipo wataelewa, lakini by then itakuwa too little too late!
 
Yule alianza kutumia mitama na kupiga roba enzi za JK akapewa tabasamu na cheo cha ukuu wa wilaya. Walimchekea bila kumuonya walipendezwa na kitendo.

Ameshika bunduki ananyemelea kuwa waziri wa mambo ya ndani. Ndio njia zake maana vyeti hana.
....maana yake watawala tulionao ndio style wanazopenda kututawala kihalifu
 
...wewe unaamini huyu anakemea wasaidizi wake?/ anachofanya nikukemea asiowapenda
 

Serikali hii ya JK Ni dhaifu, nchi inahitaji Raisi dikteta ili isonge mbele - Mnyika
- Kwa hiyo hii inasonga mbele au inarudi nyuma?
  • Bei ya sukari ikoje,
  • biashara na uwekezaji umeongezeka au unapungua? Uwekezaji kutoka nje umepungua kwa zaidi ya asilimia 9;
  • kasi ya kufunga maduka hapa nchini haijawahi kutokea tangu Tanzania kuwepo;
  • Udhaifu wa sarafu yetu umeendelea kuwepo; Malory zaidi ya asilimia 35 hayana kazi baada ya kukosa mizigo ya kusafirisha,

2. Nchi inahitaji Raisi anayeweza kufanya maamuzi magumu bila woga- Mbowe
- Ila hayo maamuzi yafanyike baada ya tafakuri ya kina ili yalete tija. Unaweza vipi kuanzisha miradi lukuki ya fedha nyingi ambazo huna na wakati huo huo unawadanganya wananchi kuwa miradi hiyo inagharamiwa kwa fedha za ndani?

3. Tunamuhitaji rais mwenye uwezo wa kukemea wasaidizi wake Na wakamtii- Lema
- Amemkemea nani? Kudhalilisha viongozi mbele ya wananchi ni kuwakemea? Vitendo vya DAB vinalalamikiwa na wengi amefanya nini?

Tumuunge rais kwa yale mazuri anayofanya lakn siyo kila kitu anafanya sawa. Anataka kuleta chembechembe za ubaguzi kwa wananchi wake, hili tulipinge kwa kulipigia kelele. Atafakari kabla ya kusema, aache kuongea uwongo, afuate katiba, miongozo, sheria na taratibu ili nchi isonge mbele

Pia akubali kukosolewa, kukosea sio dhambi wala kukosolewa sio dhambi.
 
Nimekuelewa
 
Hata mimi nilikuwepo!
Kama ulikuwepo basi lazima utafahamu kuwa makala imejaa uzushi na uongo wa kibavicha. Mimi wakati huo nilikuwa kidato cha nne kwa hiyo nilikuwa tayari najifahamu kiakili. Iddi Amin hakuwa na "kazi kubwa kueneza propaganda kwa wananchi wa Uganda ili wampende". Tangu siku ya kwanza ya mapinduzi watu walimwagika mtaani kushangilia kwa sababu Obote tayari alishapoteza imani ya wananchi. Mambo yalikuja kuharibika baadaye. Kama na wewe ulikuwepo nipo tayari hapa. Sida ganywi na uongo wa kitoto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…