Usingizi ni ugonjwa?

Fidel80

JF-Expert Member
May 3, 2008
21,947
4,445
Wakuu ni wazi tumeshuhudia watu wakiwa wamelala/sinzia wengine wanalala kwa kukoloma iwe kwenye daladala au kitandani au kwenye kochi popote pale je ni ka ugonjwa? Unakuta mtu kaachama mdomo nzi wanaingia na kutoka kama huyu hapa chini

Ni nusu kifo,ni dawa ndio maana ukiamka unajisikia nguvu mpya.Na watu wasio na usingizi wanakuwa wagonjwa kabisa na akili zao zinakuwa hazijatulia na wanautafuta hata kwa madawa ya usingizi.
 
Unakuta mtu kaachama mdomo nzi wanaingia na kutoka kama huyu hapa chini

Mazoea nayo yanachangia mkuu, kama mtu akijijengea utaratibu wa kulala amefunga mdomo itafikia kipindi atakuwa analala hivyo bila kuufungua, labda awe na mafua yanayomzuia kupumua kwa pua!
 
Wakuu ni wazi tumeshuhudia watu wakiwa wamelala/sinzia wengine wanalala kwa kukoloma iwe kwenye daladala au kitandani au kwenye kochi popote pale je ni ka ugonjwa? Unakuta mtu kaachama mdomo nzi wanaingia na kutoka kama huyu hapa chini

Usingizi kama ni ugonjwa, basi watu wote ni wagonjwa. Jamaa akiamka na akigudua umetumia picha yake, huna baati maana atakutafuta na kukuwinda kwa mishale na manati. Ila mbona wapo wengi hapo, ni makonda wa malori au ni makuli maana inaelekea mzigo ulikuwa mzito. Nyoka anaweza kuingia mdomoni bila yeye kujitabua.
 
Sasa kwa usingizi huu kwa wanandoa inakuwaje? Maana akijitupa kitandani ni hadi asubuhi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom