Hongera na pole pia kwa muziki mnene wa TRA Mkuu.Mi niliacha kazi kiwanda kikubwa cha bia kwa ukiritimba mwingi, majungu, kutiana presha. Siku naacha kazi kwa mshahara ule hakuna alie amini.
Niliingia kitaa na kamtaji kangu na kuanza kupiga ruti za Nairobi kupeleka mali na kurudi na mali.
Mambo yakaenda sawiaaa.
Japo sasa mziki wa magufuli nausoma vzr, nishapigika sana na TRA. Nafikiria kutafuta kazi tena, sasa sijui nitapata ya mshahara ule?
Mhhhh muulize kama alishaenda Law School na Kufaulu? Kama bado mwambie akajiunge huko akishapata muhuri wake mshauri akapige michongo nje ya Dar ni rahisi sana kutoboa maana kama ujuavyo wasomi wengi wanakimbilia Dar wakati kwa kipindi hiki fursa zipo mikoani. Hakika hatojutia kabisa.Mkuu hongera ila ulipata bahati ya mtu kukushika,kuna jamaa yangu kamaliza sheria yupo tu mtaani ikabidi ajishikize tu kwenye ualimu.Ukiwa na mtu ni rahisi sana kutoboa kwanza tayari huyo jamaa yako alikuwa na Law firm anajulikana michongo ipo na ndio maana nawe ukatoboa kiurahisi.
Exactly brother. Mtu inabidi unafanya uamuzi mgumu ili kuleta maendeleo. Huu siyo muda wa kuanza kulalamika ooh mshahara hautoshi mara nafanya kazi ktk mazingira magumu. Fanya uamuzi sahihi.Mkuu kwanza hongera saana kwa kupata wa kukushika mkono!! Umenipa nguvu ya kusonga mbele na maamuzi ninayotaka kuyafanya!! Inabidi tufike wakati tujitathimini: hivi kazi ninayofanya naifurahiaa?? Nafikia malengo yangu?? Au ni ili mradi tuu mateso kwenda mbele!! Watu wengi tunaogopa mabadiliko ( get rid of the fear of the unknown!!)
Hujasoma sheria Mkuu. Kwa uandishi wako huu nimekupinga kwa nguvu. utamu wa kuwa wakili ni kwamba ni fani ambayo haina kustaafu wala nini. Hivyo ukijenga jina utafaidi mpaka unaingia kaburini ni tofauti na ualimu. Ndicho kilichonishawishi kwa nguvu.Ingawa hii stori inahamasisha sana lakini kwa tuliosoma sheria tunajua huyu bwana amefanya advertiaing..kwa namna moja au ingine