Usindikaji wa pilipili na nyanya

napenda

JF-Expert Member
Jul 14, 2015
485
90
Habari wana jf, naomba mwenye ufaham wa namna ya kusindika nyanya kuwa tomato souce na pilipili kuwa chillsouce, pia vifaa kama mashine na vichanganywa pia gharama zake, nataka nii-ingize ktk baget
nawakilisha
===============

masalu isidori, post:
KUSINDIKA NYANYA
Nyanya ni zao ambalo haliwezi kuifadhika kwa muda mrefu lisipozindikwa zao hili ni zao la bustani ambalo linalimwa na wakulima na linahitajika katika shughuli za jikoni kama kiungo cha kuungi mboga, wakulima wemgi wamekuwa wakipata hasara kwa kulima zao la nyanya na kukata tamaa ya kulima zao hili tena ni kwanini kwa sababu bei ya zao hushuka pale ambapo zao hilo linapatikana kwa wingi sokoni na kumfanya mkulima ashidwe kupata faida kwa sababu zao linapokuwa lipo kwa wingi sokoni na uhitaji wa watu ni mdogo bei hushuka lakini kunakipindi ambacho zao halipatikani kwa wingi sokoni na kuwa na bei kubwa kipindi hiki ni kipindi ambacho mkulima ambaye ni mbunifu anatengeneza pesa lakini atatengenezaje pesa ni kwa kuchakata zao hilo na kulihifadhi na kuuzwa kwa bei ya juu.

Zao la nyanya ni zao ambalo hisindikwa na kupata bidhaa mbalimbali kuepuka uhalibifu wa zao hilo, kuongeza ubora na thamani, na kuwezesha upatikanaji wakati wote, zao hili huzidhikwa kuwa nyanya za kukausha,juice,lahamu na sosi au rojo.

KUKAUSHA NYANYA
Nyanya zinazotakiwa ni zile zilizokomaa na kuiva vizuri. Aina ya nyanya zinazotakiwa ni zile zenye nyama nyingi kama roma, Tanya na tengeru 97.

Vifaa
  • Visu vikali visivyoshika kutu
  • Ungo
  • Sufuria
  • Jiko
  • Kaushio bora
  • Mifuko ya plastiki
  • Beseni
Jinsi ya kukausha
  • Chagua nyanya zilizokomaa na kuiva vizuri
  • Osha kwa maji safi na salama
  • Kata nyanya kwenye vipande visivyozidi muilimita tano
  • Panga kwenye kaushio safi ili zikauke
  • Fungasha vipande vya nyanya vilivyokauka kwenye mifuko safi ya plastiki isiyopitisha unyevu
  • Weka lebo inayoonyesha muda wa kuisha matumizi kwa mwaka mmoja kutoka siku ya kutengenezwa
  • Hifadhi sehemu yenye ubaridi na kavu.
  • Hutumika kama viungo kwenye vyakula mbalimbali
KUSINDIKA NYANYA KUPATA JUISI
  • Chukua nyanya zilizoiva na kukomaa vizuri
  • Osha kwa maji safi na salama
  • Katakata nyanya katika vipande vidogo
  • Pima uzito wa nyanya
  • Kwa kilomoja ya nyanya ongeza maji lita moja
  • Chemsha kwemye moto kwa muda wa dakika 5 moto uwe na nyuzi joto 85
  • Saga nyanya kwa kutumia mashine ya mkono au umeme
  • Chuja rojo ili kupata juisi
  • Ongeza sukari gram 20 na chumvi gram 10 kwa kila lita moja ya rojo
  • Chemsha tena kwa muda wa dakika 20
  • Jaza juisi ikiwa ya moto kwenye chupa safi
  • Zipange chupa hizo kwenye sufuria
  • Weka maji kwenye sufuria yafii nusu ya chupa
  • Chemsha tena ili kuondoa hewa iliyoupo ndani ya chuapa
  • Ipua acha zipoe kisha weka lebo
  • Hifadhi kwenye ubaridi

Juisi hii huifadhiwa kwa muda wa miezi sita, hutumika kama kiburudisho
 
Mkuu leo mapumziko wengi wako busy na familia zao. Hiyo issue ikunbushie week days...
 
Unaweza kufanya manually jikoni kwako.
Uwe na nyanya na pilipili za kutosha, uwe na brenda ya kusagia, chujio la kuchujia, maji safi na salama ya kutosha, vyombo vikubwa na vya kutosha.

Endelea kufuata hizo video

Last edited by a moderator:
Habari wana jf, naomba mwenye ufaham wa namna ya kusindika nyanya kuwa tomato souce na pilipili kuwa chillsouce, pia vifaa kama mashine na vichanganywa pia gharama zake, nataka nii-ingize ktk baget
nawakilisha
MKUU fafanua
1. Unataka kuzalisha nyingi za kuuza? Au kutumia nyumbani?
2. Kama za kuuza je unaplan ni tani ngapi kwa siku unataka kuprocess??
 
Attachments

  • cat_3_tomatobased-chart.png
    cat_3_tomatobased-chart.png
    106.3 KB · Views: 527
  • S-gulliver manual tomato machine.JPG
    S-gulliver manual tomato machine.JPG
    3.7 KB · Views: 780
  • products_93663_433e63a7bb89b4320a762a016b3aac07.jpeg
    products_93663_433e63a7bb89b4320a762a016b3aac07.jpeg
    17.9 KB · Views: 517
  • 1777e7492bb857a83f39490430b43681.jpg
    1777e7492bb857a83f39490430b43681.jpg
    10 KB · Views: 606
Chipukizi
Nashukuru sana kwa msaada, lengo ni kuuza lakini nilitaka kuanza kutengeneza kwanza angalau chupa 10-hadi 50 kwa siku kwa lengo la kutafuta wateja kwanza then napanua uzalishaji , nitafurahi angalau kwa ufupi nikieleweshwa packing inafanyikaje ili product isichache na bei ya vifaa, nilitaka gharama ya vifaa isizidi 2M Kama vitapatikana
 
Last edited by a moderator:
Chipukizi
Pia hiyo attachment ya kwanza tomatobased chart ni ya kusindikia au?
 
Last edited by a moderator:
Unaweza kufanya manually jikoni kwako.
Uwe na nyanya na pilipili za kutosha, uwe na brenda ya kusagia, chujio la kuchujia, maji safi na salama ya kutosha, vyombo vikubwa na vya kutosha.

Endelea kufuata hizo video

Natumia cm haifungui youtube, nitaangalia baadae,pia nina toshiba nayo huwa inasumbua kuangalia youtube
 
Last edited by a moderator:
Chipukizi
Pia hiyo attachment ya kwanza tomatobased chart ni ya kusindikia au?
Yap hii ni factory kubwa let say 1000 tonnes per day.
1.Sajiri kampuni BRELA
2.Tengeneza na Sajiri nembo ya biashara yako e.g King tomato souce
3.Sajiri bar code ya product yako
4.From world known tomato souce formulation (ipo amabayo ndo wote wametengeneza zao tokana na hiyo)come up with your taste ( make it differ from other brand or just make it normal one and send sample to TBS
Once TBS wamekupa 100% Go ahead ndo uanze kutengeneza..
Design ya chupa ni muhimu pamoja na labeling yake kuwa na mvuto pia ni muhimu.
2 millions zinaweza kukupatia mashine za kuanzia,ila unahitaji pesa zaidi za usajiri,packing materials design and production)
Eneo la kuzalishia hiyo product usafi wake ni muhimu.
Iwapo ningepata muda wa kuonana na wewe ningeweza kukusaidia mpaka ukaanza uzalishaji,unaweza ni PM tu check na mida kwani at this time sipo Sana mjini nna kaproject kananiweka Sana maporini mpaka imalizike September ila all the best
 
Nilazima asajiri kampuni? au hata jina
 
Nilazima asajiri kampuni? au hata jina
Ndio ni lazima asajiri .hii inamanufaa kwake
1.kujulikana kitaifa
2.Benk kuweza kumapatia mikopo hapo baadae
3.itamlahishishia kupata masoko kiraisi,
Unaweza anza na business name Brela kwa 12,000 Tzs
 
Ndio ni lazima asajiri .hii inamanufaa kwake
1.kujulikana kitaifa
2.Benk kuweza kumapatia mikopo hapo baadae
3.itamlahishishia kupata masoko kiraisi,
Unaweza anza na business name Brela kwa 12,000 Tzs

Nimekupata, hivi hiki tutakiita kiwanda au? na business name inaruhusiwa kuzalisha product kama hizi za mleta mada?
 
Nimekupata, hivi hiki tutakiita kiwanda au? na business name inaruhusiwa kuzalisha product kama hizi za mleta mada?
Yap anafungua non limited company. Kwanza hii itamwezesha Ku apply vibali mbalimbali pamoja na TBS,TDFA,Leseni ya biashara n.k.
Pia kufungua ACC benk.
 
Chipukizi
Asante sana kwa ushauri wako, kwa kua imelazim kupitia usajiri wa kampuni kwanza non-limited, naomba wataaram wa mambo haya ya kusajiri wanipe ushauri hapa, naomba Busiminate na ANJOA CPN pitieni hapa mnishauri baada ya kusoma thread hii, sababu itanilazimu niombe likizo october ili niende dar kusajiri
 
Una haja ya kuja Dar kusajiri Brela.Siku hizi unamàlizana na Brela kidigital kila kitu online.temberea tovuti ya Brela leo
 
Last edited by a moderator:
nimepitia toka mwanzo wa mtoa hoja na kugundua kuwa hana utaalamu upande wa food processing na hata hivyo bado michango miingi imekuwa katika kutegeneza common tomato au chill ambazo tunazitumia majumbani ndani ya siku moja ikizidi siku mbili kwa mtu mwenye regrigerator, nafikiri mdau huyu alitaka kujua mtililiko mzima hivyo kwa kumpaka asali kidogo kwenye mdomo bado hatujamsaidia sana,nimeona you tube pics zoote hizi ni kutegeneza just home use tomato source na sio commercial chill au tomato kama yeye anavyotaka. ningependa kumshahuri mdau huyu mwenye mtazamo wa mbali kwenda Brela sijui kupata barcode, kupata usajili wa TBS ni mapema sana ktk hatua aliyonayo kwa sasa bado ni premature huyu hawezi kurupushani kwa hatua aliyonayo unless otherwise kwani alipo kwa sasa sijui tumuite nani hayupo kwenye hatua yeyote bado yupo kwenye info collection na mbaya zaidi inaonekana hana hizi ABCD za ujasiliamali.

kwa mtazamo wangu ili kupata practical experience sijui mdau huyu yuko wapi kwa sasa lakini pale Ferry soko la samaki , Magogoni kuna mzee mmoja mtaalamu sana kutegeneza chill na tomato source na daima naona anategeneza kidogo volume kubwa kwa uzoefu wangu mara nyingi naona anategeneza kila siku na kuuza ujazo wa 60 lts kila siku, anategeneza na kuuza chachandu na pia local tomato source nenda pale pata practical experience. jamani kutegeneza tomato source na chill ambazo zinakuwa packed katika mikebe au chupa sio simple kama unavyooona hapo kwenye you tube otherwise zitakuwa fermented na kutegeneza sumu, ndugu yangu mdau sio kuwa nakupa hofu hapana ningependa uweze kujua mtililiko wa kutegeneza na uweze kwenda hatua kwa hatua, kama upo Iringa sio mbaya kuomba pale Dabaga ukaenda kuona jinsi wanvyotegeneza tomato source sidhani pia kama wanategeneza chill.

otherwise mimi nianze na ushahuri huo na kama kuna other members wanaweza kuchangia kumsaidia mdau huyu kutimiza ndoto yake kitu ambacho kila kukicha tunaomba vijana wa kitanzania waweze kuwa na fikara za ujasiliamali kama huu.

aksante karibuni

Habari wana jf, naomba mwenye ufaham wa namna ya kusindika nyanya kuwa tomato souce na pilipili kuwa chillsouce, pia vifaa kama mashine na vichanganywa pia gharama zake, nataka nii-ingize ktk baget
nawakilisha
 
muvimba
Umelenga kabisa ninacho taka, shida kubwa ni kuzifanyia parking zisi-fermant, au lazima nitafute semina au mafunzo ya dalasani kabisa kwaajili ya usindikaji?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom