Mazoea hujenga tabia. Kuna mambo ambayo uzalendo hushindikana. Uaminifu unapofikia kikomo mambo yanaweza kubadilika. Mwanamke ni binadamu anayefikiri pia, tena kwa maswala hayo ni wajanja kuliko tunavyofikiri. Anaweza kutoka chumba jirani na usigundue ukawa nawe unajishughulisha na kumsifu kwa uaminifu wake, naye akakufanyia manjonjo kukupoteza ili uendelee kulala usingizi fofofo.
Yupo mama ambaye alipoona nyumba yake haipati mtoto kwa miaka kadhaa, akawakumbuka washikaji zake wa enzi za shuleni. Walipoenda kwenye semina za kikazi na kukutana huko wakafanya kweli baada ya manung'uniko ya kutokuwa na mtoto bado. Alipogundua kwamba amenasa kitu akatimua mbio kwenda nyumbani kwa mumewe na kujifanya alimkumbuka sana na kilichomleta ni mikasi tu. Mumewe alifura hi kusikia maneno hayo matamu, akashughulika sana. Mama akarudi zake kwenye semina ambako walendeleza libeneke lao na washikaji. Kisha mumewe akapigiwa simu eti kale kamchezo kamejibu safari hii.
Mpaka leo jamaa anajua mtoto ni wa kwake, lakini mama anasimulia rafiki zake walio karibu sana kama story. Hajapata mtoto mwingine tena, eti jamaa anasema anatosha waliyepewa na Mungu. Mke anaogopa kurudi tena kwa washikaji bomu lisijelipuka. mtoto sasa ni graduate na anafanya kazi, hakuna mfanano wowote na mzee. Mzee mwenyewe pamoja na kwamba naye ni mtaalam aliyebobea kwenye eneo la afya, hayaamini matokeo ya maabara yaliyomtuhumu yeye kwamba anazo kasoro kwenye mbegu zake zilizosababisha madhara kwenye hatua za kiumbe kipya.