Usimwamini mtu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Usimwamini mtu

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by Lekanjobe Kubinika, Jun 30, 2010.

 1. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #1
  Jun 30, 2010
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Sirudii tena!!!
  Posted by GLOBAL on April 14, 2010 at 9:16am
  View GLOBAL's News
  Jamaa mmoja alikuwa na mke mzuri sana. Kwa kuwa jamaa huyu kazi yake ilikuwa ni udereva wa malori , muda mwingi alikuwa safarini na hilo lilimyima raha, maana alikuwa akiogopa watoto wa mjini wasije wakamchukulia mke wake!

  Jamaa ili kuweka sawa hilo akaamua atafute mlinzi kwa ajili ya kumlinda mke wake asimwendee kinyume. Ndipo akaamua amfuate mdogo wake kijijini ili aje aifanye kazi hiyo.
  Yule mke baada ya kuona amebanwa sana kiasi cha kushindwa kabisa kwenda kokote, ikambidi aanze kumshawishi yule mlinzi ‘mdogo mtu’ mradi amsaidie kumaliza haja yake kutokana na jamaa kutokuwepo kwa muda mrefu.

  Dogo huyo kwanza alikataa katakata kumgeuka kaka yake, lakini alipolazimishwa sana alikubali kutembea huku akitetemeka kwa hofu kwamba kaka yake akijua itakuwa soo, hata alipomaliza kuvunja amri ya sita na shemeji yake aliendelea kumsisitiza shemeji yake kuwa iwe siri kubwa.
  Siku iliyofuata kaka yake alirudi safari. Dogo akawa na mchecheto kupita kiasi basi akawa anatetemeka muda wote hasa alipokuwa anasalimiana na kaka yake.

  Wakati wamekaa sebuleni akanyanyuka na kutoka nje ili japo asiwe karibu na kaka yake maana vile alivyokuwa akimtazama hofu ilimzidi akawa anatetemeka utadhani alikuwa ana homa!
  Basi bwana ile anafungua tu mlango kutoka nje, shati lake kubwa alilovaa likanasa kwenye kitasa cha mlango kwa nyuma.

  Mara moja dogo akadhani kaka yake alishajua juu ya uchafu waliofanya, hivyo ndiyo anamvuta kwa hasira ajieleze. Hapo hapo bila hata kugeuka nyuma akaanza kupiga kelele kwa hofu Samahani kaka sirudii tena! Lakini yote haya kayataka shemeji!

  Kaka mtu aliyekuwa kimya kitini, alishangazwa na hilo akamwangalia mdogo wake kisha akamwangalia mkewe na kumuuliza,
  “Vipi huyu amechanganyikiwa? Mkewe aye akatoa macho akipepesa huku na huko huku akitetemeka.  Other:
   
 2. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #2
  Jul 5, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  aiseee hiyo ipo inakuwa ni automatically kama utakuwa na ghofu na kitu lazima hali hiyo itjitokeza.....ndio mkubwa asante na nimekusomaaaaaaaa.:pound::pound::pound::pound::pound:
   
 3. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #3
  Jul 5, 2010
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mazoea hujenga tabia. Kuna mambo ambayo uzalendo hushindikana. Uaminifu unapofikia kikomo mambo yanaweza kubadilika. Mwanamke ni binadamu anayefikiri pia, tena kwa maswala hayo ni wajanja kuliko tunavyofikiri. Anaweza kutoka chumba jirani na usigundue ukawa nawe unajishughulisha na kumsifu kwa uaminifu wake, naye akakufanyia manjonjo kukupoteza ili uendelee kulala usingizi fofofo.

  Yupo mama ambaye alipoona nyumba yake haipati mtoto kwa miaka kadhaa, akawakumbuka washikaji zake wa enzi za shuleni. Walipoenda kwenye semina za kikazi na kukutana huko wakafanya kweli baada ya manung'uniko ya kutokuwa na mtoto bado. Alipogundua kwamba amenasa kitu akatimua mbio kwenda nyumbani kwa mumewe na kujifanya alimkumbuka sana na kilichomleta ni mikasi tu. Mumewe alifura hi kusikia maneno hayo matamu, akashughulika sana. Mama akarudi zake kwenye semina ambako walendeleza libeneke lao na washikaji. Kisha mumewe akapigiwa simu eti kale kamchezo kamejibu safari hii.

  Mpaka leo jamaa anajua mtoto ni wa kwake, lakini mama anasimulia rafiki zake walio karibu sana kama story. Hajapata mtoto mwingine tena, eti jamaa anasema anatosha waliyepewa na Mungu. Mke anaogopa kurudi tena kwa washikaji bomu lisijelipuka. mtoto sasa ni graduate na anafanya kazi, hakuna mfanano wowote na mzee. Mzee mwenyewe pamoja na kwamba naye ni mtaalam aliyebobea kwenye eneo la afya, hayaamini matokeo ya maabara yaliyomtuhumu yeye kwamba anazo kasoro kwenye mbegu zake zilizosababisha madhara kwenye hatua za kiumbe kipya.
   
 4. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #4
  Jul 5, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Mkuu Lekanjobe nilishawahi kusema somewhere kwamba Wanaume tunapojidai we are playing a winning game we are actualy the biggest LOOSERs! Ipo ya jamaa ninayemfahamu ambaye yeye alikuwa na kamchezo ka kumega nje mara kwa mara; Mkewe akamtafadhalisha aache huo mchezo ; jamaa akaweka pamba masikioni; Mwanamama akaamua kufanya kweli akajitafutia ka Serengeti boy amabko alikaleta ome pale kwa mwavuli wa ndugu kalikaa mwezi mzima na kakawa kanjivinjari bila shida mpaka siku Mungu alipomhurumia jamaa na kumrudisha nyumbani ghafla na kuwafuma wakiwa kitandani. Alipokuja juu na kutaka kutoa adhabu akaanza kuhesabiwa issue zake moja baada ya nyingine na Mama na kuambiwa anavyojisikia sasa ndivyo hata Mamaa amekuwa akijisikia katika mara zoote alizokuwa Jamaa natoka nje ya ndoa ......ilibidi awe mpole na sasa wanaishi na mkewe (Sijui kama ni kwa usalama) Lakini jamaa kashika adabu yake!............Usiombee yakukute haya!
   
Loading...