Denis1729
Member
- Sep 9, 2021
- 34
- 109
Ndoa ni kiungo muhimu zaidi chenye raha na starehe kubwa wahusika wanapochunga mipaka na kutunzana vilivyo. Kwa upande mwingine, huweza kuwa chanzo na masikitiko makubwa maishani iwapo hutatumia hekima kwa mambo yanayohusiana nayo.
Je, wajua kuwa ulimi ndiyo huunda na kubomoa ndoa? Haya ni baadhi ya mambo ambayo kamwe hufai kutumia, na siri za kutotoa ili ndoa yako idumu.
Usiwahi kumwambia rafiki ama mtu yeyote kuhusu jinsi mumeo ama mkeo alivyo hodari kitandani. Yasalie kuwa kati yenyu tu.
Usimwambie mtu kumtongoza mkeo ama mumeo kama njia ya kudhibitisha kama ana uaminifu.
Usimwambie yeyote kuhusu makosa ya zamani ya mwenzio.
Usiwahi kuwaambia majirani au familia kuhusu uwezo wa mumeo kifedha.
Usimwambie mtu kuhusu jinsi mumeo au mkeo ni mdhaifu kitandani, watakuaibisha kwa kumcheka.
Usiwaaambie watoto kuwa baba au mama yao ni mtu mbaya.
Usiwe na mazoea ya kutangaza kwa urahisi shida, au tofauti zenyu. Watatumia nafasi hiyo kuwatenganisha kabisa.
Usimwambie hata mchungaji wenu kuhusu jinsi mvavyokwaruzana nyumbani, wengine watatumia hiyo katika kuandaa mahubiri.
Usiwahi kumwambia mama mkwe kuhusu kiwango cha pesa ambacho mumeo hukupa,
atakuwa na kinyongo bure.
Usiwaambie rafiki zako kuhusu jinsi mkeo au mumeo alivyo na tabia mbaya, fanya kila njia kuibadilisha tabia hiyo.
Hakuna ndoa hata moja duniani ambayo haina panda shuka, inahitaji wawili kulainisha tofauti zao na kufurahia maisha kama wanandoa.
Je, wajua kuwa ndoa tu ndiyo shule ambapo unapewaa cheti cha kufuzi kabla kuanza ya masomo na mtihani? Kila mmoja awe tayari kuchunga na kutunza uhusiano wake kikamilifu.