Usimwage damu isiyo na hatia kwa maana wala usimuonee mnyonge

TumainiEl

JF-Expert Member
Jan 13, 2010
6,188
11,221
Usimwage damu isiyo na hatia wala usimuonee mtu mnyonge, yatima, mjane au mtu ambaye hata ukimfanyia ubaya huwezi pata majibu ya maswali yako.

Unaweza ukafikiri nina nguvu nina pesa na Mamlaka hivyo na roho hizi mali yangu, nakuapia mwisho unakuwa mbaya sana sana.

Gemedari mkubwa ktk Israel alipewa amri amuue Uria. Kweli akamuuwa ila pamoja na mema yote alie mfanyia mfalme, mfalme alipokuwa mzee alimwambia mwanae Suleiman asimuache roho yake yule gemedar aishi na kweli aliuwawa vile vile kwa upanga.

Usitoe uhai wa mwanadam kwa makusudi au kwakupanga maana dam ya mtu huyo itakutesa mpaka kaburini ndio maana muuwaji anatapa tapa maana anaogopa kifo japo yeye ni mtoa roho. Kwanini anatapatapa wakati yeye ni mtoa roho? Haya ni maneno ya Mungu kwa Kaini baada ya kumuuwa Abili nduguye. Almwambia dam ya ndugu yako ina nililia ardhini"

Unapo mwaga dam nakuongoza mauwaji dam za ulio watoa roho zinakulilia nakukusumbuwa nakuapia hakuna mchawi wala nabii anaweza kukupa usingizi wa hofu uta tapa tapa utahangaika utahama kila nyumba ila dam ya ulio wauwa inakulilia na mara nyingi mwisho mtu hufa kwa hofu.

Pesa au mali isikudanganye kutoa uhai wa mtu hata kama ni masikin nakuapia utalipa hiyo damu wewe na uzao wako.

Ndio maana duniani kuna mambo yakutisha sana. Why? Mungu yupo Mungu yupo.
 
Imeandikwa

"Mtendeee ndugu yako kadiri ya vile upedavyo kutendewa wewe."

Ukiua na wewe utauawa

When you do things good to others, Good things come back you and

the same

when you do bad things it will come back to you
na hyo ni laana ya kizazi cha kwanza hata cha nne cha uzao wako.
 
Waulize wanawake wote waliowahi kuzichoropoa mimba. Kilio wanachosikia wakiingia kwenye vyoo ndo maana hawaendi vyoo vya mashimo. Hiyo ni mimba yake tu, Je, mtoto wa mwenzio tena ukuite ni baba au mama wa mtu
 
Mwaka 2017 tarehe 7 Sept Kule Kimara Dar zilivunjwa nyumba zilizokua mita 121 kutoka katikati ya barabara. Nilimuona mwanamke mmoja aliyevunjiwa nyumba yake bila kulipwa wala taarifa.

Yule mmama alihangaika kama ndege aliyevunjiwa kiota chake chenye vifaranga wake. Waliovunja ile nyumba baada ya kuvunja wakaenda kupaki tingatinga Lao karibu na bar ya karibu.

Kuna mzee mmoja watoto wake walimuambia ' mzee wanavunja nyumba' basi mzee alinena mara tatu. Wanavunja , wanavunja, wanavunja then akaanguka akafa. Just like that......
 
Ni kweli, kumwaga damu ya mtu asiye na hatia ni deni kubwa ambalo lazima lilipwe na mhusika pamoja na familia yake.
 
Hapa mpaka midomo inatetemeka, Naamini lazma mtoa mada ni mtu wa jikoni, alimtahadharisha Ben kwasababu alijua nini kitamkuta.

Nikirudi kwenye thread zake za leo zinaonesha Kuna kitu kinawasumbua wale waliowaua Watanzania bila hatia akiwemo Ben na kujeruhiwa kwa tundu lissu, kama ndivyo nami nasema na iwe hivyo! Sipendi maonezi mimi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kanuni hii huenda haifanyi kazi kwa watu walopokaji kama Mdude.
 
Usimwage damu isiyo na hatia wala usimuonee mtu mnyonge, yatima, mjane au mtu ambaye hata ukimfanyia ubaya huwezi pata majibu ya maswali yako.

Unaweza ukafikiri nina nguvu nina pesa na Mamlaka hivyo na roho hizi mali yangu, nakuapia mwisho unakuwa mbaya sana sana.

Gemedari mkubwa ktk Israel alipewa amri amuue Uria. Kweli akamuuwa ila pamoja na mema yote alie mfanyia mfalme, mfalme alipokuwa mzee alimwambia mwanae Suleiman asimuache roho yake yule gemedar aishi na kweli aliuwawa vile vile kwa upanga.

Usitoe uhai wa mwanadam kwa makusudi au kwakupanga maana dam ya mtu huyo itakutesa mpaka kaburini ndio maana muuwaji anatapa tapa maana anaogopa kifo japo yeye ni mtoa roho. Kwanini anatapatapa wakati yeye ni mtoa roho? Haya ni maneno ya Mungu kwa Kaini baada ya kumuuwa Abili nduguye. Almwambia dam ya ndugu yako ina nililia ardhini"

Unapo mwaga dam nakuongoza mauwaji dam za ulio watoa roho zinakulilia nakukusumbuwa nakuapia hakuna mchawi wala nabii anaweza kukupa usingizi wa hofu uta tapa tapa utahangaika utahama kila nyumba ila dam ya ulio wauwa inakulilia na mara nyingi mwisho mtu hufa kwa hofu.

Pesa au mali isikudanganye kutoa uhai wa mtu hata kama ni masikin nakuapia utalipa hiyo damu wewe na uzao wako.

Ndio maana duniani kuna mambo yakutisha sana. Why? Mungu yupo Mungu yupo.
Ilikuwa 2020 May leo yanatimia na watu wanatapa tapa...
 
Back
Top Bottom