Usimnyang'anye mwanamke mtoto

USIMNYANG'ANYE MWANAMKE MTOTO!

Anaandika, Robert Heriel.
Mtibeli.

Hapa Duniani kitu cha thamani kuliko vyote Kwa mwanamke ni mtoto wake. Hata hivyo watoto ndio huweza kuonyesha waziwazi Mchango wa mwanamke ndani ya jamii.

Huko kwingine inaweza isiwe sana lakini linapokuja suala la watoto na uzazi hapo ndipo Role kuu ya mwanamke ndani ya jamii hudhihirika waziwazi!

Mnyang'anye yote mwanamke lakini kamwe usimnyang'anye mtoto aliyemzaa. Hiyo sio haki.

Ikiwa imetokea mkatofautiana na mkeo au mwanamke uliyezaa naye mtoto mpaka ikafikia hatua inawapasa kutengana basi hapo itakupasa umuachie mtoto.

Labda iwe kwa hiyari yake mwenyewe, apende mtoto akae nawe lakini kamwe usitumie mabavu kumnyang'anya mwanamke mtoto aliyemzaa. Haitakusaidia lolote na wala hautapata chochote. Niamini!

Unachoweza kufanya ni kutumia akili uliyopewa na Mungu kama Mwanaume kumshawishi mwanamke wako huyo na bahati nzuri wanawake wameumbwa kushawishika, hivyo kama una akili njema lazima mwanamke atakubali.

Lakini usiongozwe na hisia kama mwanamke ikafikia hatua ukataka kupambana na mwanamke huo sio Uanaume, bali uanamke, mwanamke ndiye hupenda kupambana na Mwanaume, lakini wanaume halisi kamwe hawawezi kupambana na wanawake isipokuwa udhaifu wa wanawake kujiimarisha.

Ikiwa mazingira ya Mwanamke sio mazuri na yanaweza kumuathiri mtoto wenu, jitahidi kumshawishi mwanamke aone hiyo hatari, jiepushe kusema Mtoto ni wako, bali tumia zaidi Kauli, mtoto wetu au mtoto wake(ukimrejelea huyo mama) jaribu Kueleza namna gani unatamani mtoto huyo afike mbali ili baadaye aje kuwa msaada Mkubwa Kwa Mama yake huyo.
Jaribu kumueleza kuwa ulitàmani utimize ndoto za huyo mwanamke lakini haikuwa riziki na mipango ya Mungu haijaruhusu ninyi kuwa pamoja. Ila unaamini Kama utamsaidia mtoto wake basi malengo ya huyo mwanamke yatatimia kupitia huyo mtoto.

Jaribu kuchukua nafasi ya Huyo mwanamke, jaribu kuelewa nafasi yake, jaribu kumuona Kuku akinyang'anywa vifaranga wake bila ridhaa yake vile anakuwa, jiweke nafasi hiyo, hapo unaweza kupata robo ya maumivu ambayo mwanamke huyapitia pale anaponyang'anywa mtoto wake aliyemzaa.

Ikiwa mimba iliingia Kwa dharura Kwa mwanamke ambaye mlikuwa mnastareheshana naye tuu na wala Hamkuwa na malengo ya kuwa mume na mke basi utamuachia mtoto lakini utoe matumizi kadiri ya uwezo wako.
Ikiwa mwanamke huyo atakuwa anakusumbua kuwa humlei mtoto wako licha ya kuwa wewe unapambana kutoa walau upatacho, wala usiumizwe na maneno ya huyo mwanamke kiasi cha kususa na kumkemea.

Fahamu wanawake ni watu wa kuongozwa na hisia ndipo akili ifuate, msamehe mwambie utajitahidi ilimradi mtoto wenu aishi vizuri. Jaribu kumwambia yeye asibaki kulaumu Bali naye anaweza kuchangia Kwa kukuombea ili Mungu azidi kufungua riziki.
Mwanamke atakujibu nyokonyoko lakini akikaa pekeake atakuelewa pale akili yake ukirudi baada ya hisia zake kuondoka.

Mwambie huyo mwanamke kuwa hata hivyo unamsifu Kwa namna anavyo pambana kuhakikisha mtoto wenu anapata mahitaji yake. Msitu, mtukuze na jaribu kujiweka Low key utashangaa yeye naye anakusifu huku akisema matatizo yako madogo madogo Kwa mfano; tatizo Baba nani unakaa kimya Sana huniambii chochote, sasa Mimi ukikaa kimya naona unazingua, Ila ukiniambia Kam hivi najua kuwa unania sema uwezo mdogo" hivyo ndivyo atasema.

Mwanamke hupenda utukufu, sifa na kushukuriwa.

Hata kama ni Mkeo umemuoa ndani, na unamtunza vizuri. Usipende kujitukukuza na kutukuza pesa na kazi yako.
Mwambie Mkeo hivi; Unajua Mama Nanii! Bila wewe humu ndani sijui kama watoto wangu wangekuwa na Afya na wasafi kiasi hiki, najivunia kuwa na Mke Kama wewe, sijui ingekuwaje Kama nisingekuoa"

Utaona mwanamke atakavyoongeza juhudi na kukupenda.

Sio ukifika kila siku unajitamba; Mimi natoa pesa kila siku, bila Mimi humu ndani wewe usingenenepa hivi; bila Mimi usingekuwa unapendeza Kama hivi"
Hii hupunguza upendo Kwa mwanamke na kukuona unamajivuno na kumnyanyasa.

Sema; Wangapi wanapesa na kazi kama yangu lakini wamedhoofu na kufubaa! Lakini tazama Mimi nilivyonawiri, unafikiri mke wangu bila ya wewe Mimi ningekuwa mtanashati hivi, ningekuwa na kakitambi Noma Kama haka! Embu kaguse kakitambi Noma Kako" anashika kitambi chako huku anacheka

Hivyo ndivyo kuishi na Mwanamke Kwa Akili!

Wanawake wanaongozwa na Hisia ndio maana hupenda kusifiwa na kutukuzwa.

Mwambie Mwanamke kuwa, sijui utafanyaje kuishi na watoto maana unajua yeye ndiye mwenye uwezo huo
Mwambie Kwa vile ameolewa na Bwana mwingine ungependelea kuishi na mtoto wako huku yeye kila siku akitaka awasiliane naye.
Lengo la kuishi na mtoto ni Kwa sababu za kimazingara kwani unapoishi kuna Huduma nzuri za kijamii Kama shule, hospital, na sehemu za watoto kwenda kufurahi tofauti na anapoishi yeye.
Mwambie, Ila ni hiyari yake kumruhusu mtoto au laa, Ila yote ni Kwa furaha ya mtoto ambayo unaamini pia ni furaha yake Kama mama.

Mwambie unajali furaha yake, na Kama umeshindwa kuitimiza kwake basi utaitimiza kupitia mtoto wenu.

Usimlazimishe Mwanamke akupe mtoto. Hiyo sio Sawa. Sio haki. Mtoto ni wamama ambaye wanawake hutupa wanaume Kama zawadi kubwa ambayo ingetosha kulingana na upendo tunaowapaga.

Ni lazima Vijana tuwafunze namna Bora ya kuishi na wanawake, Kuwatunza na kuwafanya wawe sehemu yetu licha ya madhaifu Yao ambayo kimsingi ndio hunogesha usichana na uanamke wao.

Mwisho; wanawake nanyi nawasihi linapokuja ishu ya mtoto mujali zaidi maslahi ya mtoto kuliko kutanguliza maslahi yenu. Ikiwa utaona upande wa mwanaume mtoto wako ndio atapata mahitaji yake yote na kupata urahisi wa kufikia Future yake basi waruhusuni wanaume wakae na watoto wenu.

Lakini kama unaona mazingira ya Baba WA mtoto ni magumu na mtoto hatafikia malengo yake ya baadaye basi mlee mwenyewe!

Sio unang'ang'ania kuishi na mtoto wakati huna uwezo wa kumtunza Mtoto, mwishowe unamtesa mtoto analeta kero ndan ya jamii Kwa kuwa kibaka, chokoraa n.k.
Unategemea kufanya ukahaba ndio ulee mtoto hiyo haijakaa Sawa.
Lazima watu tukubali Hali zetu, kuwa Mimi siwezi Kulea mtoto Kwa Hali yangu hii, iwe Kwa mwanaume au mwanamke.

Nimemaliza!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es Salaam
Mkuu nyuzi zako nazifwatilia sana hua zinakua na madini mengi sana!! Your the real Critical thinker br! Hongera sana mkuu.
 
mbeleni tutakuwa na kizazi cha ovyo,wanaume hawajitambui wanamwaga mbegu tu wanawake nao wanategesha mimba matokeo yake watoto wanalelewa upande mmoja,mtoto aliyelelewa kwenye mazingira hayo haoni umuhimu wa ndoa
 
Back
Top Bottom