Usimjibu mkeo Kifidhuli!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Usimjibu mkeo Kifidhuli!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Kigarama, Apr 15, 2012.

 1. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #1
  Apr 15, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mahusiano kati ya wapendanao hujengwa zaidi na hisia za moyo (Feelings), zikipotea hakuna mapenzi yanabaki mazoea!!

  kati ya mambo ambayo yanavuruga mapenzi kati ya wanaume na wanawake ni majibu ya kifidhuli ambayo wanaume huyatoa kwa wake zao. Kuna mwanamke mmoja aliwahi kumnunulia mume wake shati jeusi la mikono mirefu pale mnazi mmoja Dar es salaam mwaka 1974. Kwa bahati mbaya yule mwanaume hakulipenda lile shati kwani mashati ya mikono mirefu si stahili yake ya mtindo.

  Sasa badala ya kujibu kistaarabu jamaa likamtoka la kumtoka " wewe ina maana ni kipofu huoni mashati ambayo huwa navaa?" binti wa watu akanyong'onyea asijue la kufanya na shati lake mkononi. Miaka 30 baadaye wakiwa wazee jamaa aliletewa shati nyumbani na wauza mitumba, kwa bahati mbaya hakuwepo ila mkewe alikuwepo. Wauza mitumba walishindwa kuuza kwani mkewe akajibu mwenyewe kulihitaji hayupo.

  Mzee kurudi anauliza kama kuna wauza mitumba walikuja kuleta mashati, akaambiwa walikuja. Alipouliza ni kwa nini mkewe hakumchukulia akajibiwa kwamba " tangu lini nikajua aina ya mashati unayovaa?" Mzee akakumbushwa kisa cha miaka 30 iliyopita. Wajukuu zake kusikia ilivyokuwa wakabaki na butwaa kumbe babu yao aliwahi kununuliwa shati na bibi yao akalikataa!!

  Wanawake wanaweza wasiwe na kinyongo lakini wana uwezo wa kuweka mambo mioyoni mwao kwa muda mrefu sana. Kwa mfano kama mkeo akikuuliza "nikupikie nini leo" anatarajia umjibu kwa staha. Na kwa bahati mbaya sana wanaume wengi hawaelewi maana ya hili swali. Wanawake hawawezi kusema leo nimetamani kula na wewe chakula cha jioni kwa hiyo wahi kurudi badala ya kwenda kwenye pombe. Wao swali la nikupikie nini linabeba maana kubwa sana.

  Wanaume tujifunze kutokuwajibu kifidhuli wake zetu!!

   
 2. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #2
  Apr 15, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 801
  Trophy Points: 280
  Ngoja waje waponde; ila uzuri wengi huponda lkn hufanyia kazi kisirisiri!
   
 3. sun wu

  sun wu JF-Expert Member

  #3
  Apr 15, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 2,025
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 0
  No body deserves kujibiwa kifedhuli awe mkeo, mume wako au mfanyakazi wako..
   
 4. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #4
  Apr 15, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 801
  Trophy Points: 280
  Very true! Kwa mwanamke imekuwa issue kwa vile kuna reaction itafuata after action ingawa yaweza chukua ages. Nani anapenda kuwa hit back?

  Ideally, unapaswa kutenda wema for the sake of it na sio kwa kutegemea kutendewa in return!
   
 5. h

  hayaka JF-Expert Member

  #5
  Apr 15, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  majibu ya dharau yanapunguza mapenzi ndani ya nyumba. Haijalishi yupi anamjibu mwenzio. Kuheshimiana ni muhimu.
   
 6. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #6
  Apr 15, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  mdau,hli umelifanyia utafiti?
   
 7. sun wu

  sun wu JF-Expert Member

  #7
  Apr 15, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 2,025
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 0
  Then do you believe in the saying that.....

  Men forget but never forgive.., women forgive but never forget...:)
   
 8. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #8
  Apr 15, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  dah,
  4 sure
   
 9. uttoh2002

  uttoh2002 JF-Expert Member

  #9
  Apr 15, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 3,679
  Likes Received: 2,743
  Trophy Points: 280
  Good message, but dont generalize it, both Men and Women need to strike a balance! that is the fact, kuna situation a Man has to do more, likewise the Woman, shida ni unapogeneralize kwamba wanaume ndo wawe hivyo.


   
 10. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #10
  Apr 15, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  Mkuu umetisha!!
   
 11. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #11
  Apr 15, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 801
  Trophy Points: 280
  Hapana, wishful thinking tu!
   
 12. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #12
  Apr 15, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 12,030
  Likes Received: 2,677
  Trophy Points: 280
  Kila mtu na maisha yake bana.
   
 13. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #13
  Apr 15, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 801
  Trophy Points: 280
  Aisee yaweza kuwa kuwa na chembe za ukweli ndani yake.
   
 14. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #14
  Apr 15, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,918
  Likes Received: 83,432
  Trophy Points: 280

  Naunga mkono kauli yako Mkuu.
   
 15. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #15
  Apr 15, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Sija generalize ndugu yangu nimetumia asilimia. Asilimia kubwa ya wanaume ndiyo wanakuwa wa kwanza kuwajibu wenzi wao kifidhuli.
   
 16. uttoh2002

  uttoh2002 JF-Expert Member

  #16
  Apr 15, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 3,679
  Likes Received: 2,743
  Trophy Points: 280
  Good to know, I get it, but just a note, it takes both Man and Woman to make a health Marriage.
   
 17. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #17
  Apr 15, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Umenikumbusha mbali sana. asante sana
   
 18. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #18
  Apr 15, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Ulimsamehe lakini...?
   
 19. Foundation

  Foundation JF-Expert Member

  #19
  Apr 15, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 1,458
  Likes Received: 256
  Trophy Points: 180
  Mimi niliwahi shuhudia mke anamtukana mumewe tusi.Alimwambia mumewe wewe mseng............ huku akifoka. Hao wanandoa walikuwa wana zaidi ya miaka 30 wakati huo,ilikuwa mwishoni mwa miaka ya 90. Mume ni tumgambile, mama ni mtu wa kaskazini huko.

  Alipoondoka mkewe, yule mzee alinipa maneno ya husia baada ya hapo,nikaona kama ananipotezea muda tu kwa sababu nilikuwa na miaka kama 16, hata mapenzi sijui. Ila maneno yake nayakumbumbuka mpaka leo.

  Narudi kwa mtoa mada, haitakiwi kumjibu mtu yoyote ovyo hata kidogo, hata wanawake wanawajibu vibaya waume ua wapenzi wao. Kujibu ovyo hakuna gender ila tabia ya mtu tu
   
 20. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #20
  Apr 15, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Foundation mimi mada hii inaegemea kwenye hoja ya Sun Wu hapo chini...Wanaume tuna tabia ya kusahau lakini hatuna tabia ya kusamehe tunapotendewa kosa na wenza wetu. Lakini wanawake wana uwezo mkubwa sana wa kusamehe wenza wao lakini kusahau ni mwiko!! Kwa maana hiyo kama mwanamke akamjibu kifidhuli mwanaume yeye mwanaume kesho yake atachukulia kama ni siku "mpya" lakini kwa mwanamke atakusamehe papo hapo (on the spot) lakini jua kwamba ulichomfanyia akita mtoka rohoni mwake milele.
   
Loading...