Usimdhamini 'foreigner' police... Nilinusurika kuingia lupango!

Nikiona bandiko hapa liko na jina lako, hakika huwa najua kuna madini mhimu kwa afya yangu ya ubongo (burudani+elimu ya maisha pia).
Huwa nakuelewa sana brother.
 
Wamarekani wana kitu wanaita classified information... Yaani habari fulani kwa kundi fulani la watu... Na muda ukipita haiwi classified tena bali hutolewa kwa umma.. Lakini ni baada ya kujiridhisha haina madhara tena....

Kiswahili tunasema mavi ya kale hayanuki... Kisa hiki ni cha muda mrefu sana... Sitataja wahusika kwa majina na baadhi kwa vyeo

Nilikuwa nafanya kazi na raia 6 wa kigeni, ofisi kuu ikiwa Dar na ndogo ikiwa Lugoba... Tiktak za maisha na kutaka kutoboa kwa haraka hawa ndugu wakafanya makaratee yao na mamlaka ya mapato.. Dili ikavia na mzigo ukakamatwa.... Klichofuata ilikuwa ni kuwatafuta wahusika...
Bila kujua kinachoendelea Dar siku moja tukiwa tunarudi Dar kupitia Chalinze tukadakwa Kibaha... Lakini kwenye maelezo ikaonekana waliodakwa ni waajiriwa tu... Mabosi walikuwa dar 3 na walishakimbia kusikojulikana... Hawa 3 niliokuwa nao walikuwa waajiriwa tu kama mimi, hivyo nikaombwa niwadhamini... Kwa Makubaliano kuwa jumatatu yake (siku iyo ilikuwa ijumaa) niwarudishe Kibaha Polisi

Baada ya kukamilisha mchakato wa dhamana ilikuwa saa tatu usiku... Tulikamatwa saa tano asubuhi... Wale wageni hawakutaka tena kwenda Dar hivyo wakalala kibaha mimi nikarudi Dar nikijua hii ni ishu ndogo hivyo jumatatu yake nikafanya mambo mengine nikisahau kabisa ishu ya polisi na wale wageni jumamosi yake walirudi Lugoba
Jumanne asubuhi ndio nikaondoka Dar kurudi Lugoba nikiwa na gari ya ofisi.... Saa tano asubuhi hivi nikiwa napita kibaha nikapata simu ya polisi kuniuliza niko wapi..... Nikadanganya kuwa niko mbezi akanikumbusha kuwa jana yake nilipaswa kuwapeleka police na sikufanya hivyo.... Hivyo nimeanza kutafutwa
Wakati nazidi kuumiza kichwa msiri wangu akaniambia nasubiriwa kibaha nikamatwe.... Duu wakati niko kwa Mathias.... Nakaribia miembe saba nikapigiwa tena simu kuwa police wametoka Chalinze wanaenda Lugoba kuwakamata wale wageni tuunganishwe kwenye kesi moja.. Pona yangu ni mimi kuwawahi polisi na kuwakabidhi polisi wale wageni...

Nitafanyaje sasa!!! Siwezi kupaa niko Kwa mfipa wakati huo na polisi wa Chalinze tayari wako njiani kwenda Lugoba na muda si mrefu itajulikana nimeshapita Kibaha hivyo zitawekwa barriers mpaka Chalinze... Kwa vyovyote inabidi nisikamatwe na wale wageni wasikamatwe... Mpaka niwapate mimi kwanza

Gari yetu ya ofisi ilikuwa maarufu sana kwa askari wote wa patrol na trafiki kuanzia Lugoba mpaka Dar... Namba zake, rangi zake na shepu yake iliifanya itambulike kirahisi.... Mahesabu yangu ilikuwa ni kufika Mlandizi bila kukamatwa lakini pia kuhakikisha wageni hawakamatwi
Nafika checkpoint msiri wangu akanitonya kuwa gari imeonekana ikipita Kibaha muda si mrefu hivyo taarifa zishafika kwenye barriers zote.. Nisipite nizuiliwe popote nitakapopatikana..... Ilibidi akili ichemke haraka sana.... Kutoka checkpoint pale TRA kuna barrier 4 mpaka kufika Mlandizi na barrier kubwa iko madafu... Kwahiyo ili nisikamatwe inabidi kutembea off road lakini kwa tahadhari... Hatua iliyofuata ni kuwapigia wageni simu wafunge geti kwa na waruke ukuta watoke kwa nyuma... Nikawalekeza pa kusubiria wakati nawatumia gari toka Chalinze
Nilifanikiwa kufika Mlandizi bila kunaswa kwa kupitia njia za vichochoroni.... Nilifanikiwa kuwatoa wageni Lugoba mpaka Chalinze nikawabadilishia gari.... Jumla zilitumika tax 4 mpaka kuwafikisha mlandizi... Hapo nikawa na amani sasa

.... Mwisho wa sehemu ya kwanza.....
Kumbe wewe ni mhalifu unaleta maburuki nchini then your days are numbered!!
 
Nadhani sheria inaruhusu kurudi kituoni muda wowote kubatilisha kuwa mdhamini pindi mambo yanapoanza kuleta sintofahamu! Ningewapeleka mahali tulivu niwafungie ndani wote kitakachofata wakahadithiane lupango. Tho itategemea wanamsaada gani kwenye maisha yangu
 
Kuna sababu zinasababisha hiyo hali.. Kwa mfano uzi huu... Baada tu ya kuuweka kuna watu nje ya forum hawakupendezwa nao kwa sababu nisizofahamu....
Unajaribu kumridhisha binadamu, utaweza?
Binadamu hatosheki, hata ukimpa nini, milele hatoridhika
 
Kuna sababu zinasababisha hiyo hali.. Kwa mfano uzi huu... Baada tu ya kuuweka kuna watu nje ya forum hawakupendezwa nao kwa sababu nisizofahamu....
Unajaribu kumridhisha binadamu, utaweza?
Binadamu hatosheki, hata ukimpa nini, milele hatoridhika
 
Fiction yako nzur Sana,fanya uitengenezee na muvi kabsa mkuuu
Sio fiction ni habari ya kweli na kuna sehemu kubwa sikuiweka hapa... Ingekuwa fiction ningesema hivyo tangu mwanzo na nisingeomba moderator aifute hii post
 
Back
Top Bottom