Tunaishi katika nyakati/zama za mwisho kabisa huku unabii kuhusu UNYAKUO WA WATAKATIFU WALIOKO DUNIANI /KURUDI KWA YESU MARA YA PILI kukiwa kumekaribia sana kwa mujibu wa ufunuo na maandiko.
WAKATI WAKATI TULIONAO NI MCHACHE SANA...sisi kama RAIA WA MBINGUNI tunaosafiri safari ya kuelekea MBINGUNI kwenye makao yetu ya kudumu,tukijua hapa duniani sio kwetu na tunapita tu na maisha ya duniani ni ya muda mfupi sana.
1)hatujui saa wala dakika ambayo tutatwaliwa tutaondolewa/MUDA wetu wa kuishi hapa duniani utaisha ama unyakuoa utatokea ,hivyo kila dakika ya MUDA tulionayo tukiwa hapa duniani ni mali endapo tuki itumia kwa utukufu wa Mungu ,na itakuwa ni hasara tukitumia muda wetu mwingi zaidi na kuwekeza TUKIZITUMIKIA MALI na kupenda pesa na kuzitafuta pesa,
nyakati za mwisho.
watu watapenda pesa kuliko chochote ,kuliko kumpenda Mungu,kuliko utu..upendo kati ya mtu na utu UTAPOA ,watu watapenda viti/mali kuliko utu/Mungu..na wengi hali wakiitamani pesa watajifarakanisha na imani yao na kujichomankwa maumivu makali.
PIA wengi sasa watakuwa wanaitumikia pesa badala ya kumtumikia MUNGU ,na huwezi kuwatumikia ma bwana wawili,yani umtumikie Mungu na utumikie Mali,lazima utampenda mmoja zaidi .
Biblia imetupa maneno ya hekima katika hili..kwamba tulinde sana moyo wote kwani ndipo zitokapo chemichemi za uzima kwa maana kule hazina yako iliko ndiko uliko moyo wako yaani kama utawekeza zadi katika kiyafikia mafanikio ya hapa duniani kuliko unavyowekeza katika hazina yako ya mbinguni kwa Mungu, mkwamba ni rahisi kwa ngamia kupenya kwenye tundu la sindano kuliko ilivyo kwa tajiri kwa sababu moyo wako utakuwa zaidi kule ulikowekeza MUDA wako zaidi na hiyo pia ni IBADA YA SANAMU KUTUMIKIA MALI..badala ya Mali zitumike kumtumikia Mungu,ikiwemo MUDA ,muda nao ni mali unagawaje muda wako katika masaa 24 ya siku ,unawekeza zaidi wapi huko ulikowekeza zaidi ndiyo ibada yako ndiyo moyo wako uliko..
watu wengine hatuji kwenye ibada kusali kama kuna kazi ya kuingiza ipo inakuhitaji kufanya MUDA huo ambayo itakuingizia hela au lipo jambo ambalo inaliona ni muhimu kuhudhuria au kufanya MUDA huo,tunakuja kwenye ibada muda ambao tunafikiri hatuna mambo mengine dearest ya kufanya muda huo.
Ila biblia inatumbia tuutafute kwanza ufalme wa mbingu,na mengine yote tutazidishiwa,na kwamba BWANA asipoujenga mji au asipoulinda mji yeye aujengao na kuulindao afanya kazi bure.
Kama unakusanya bila uwepo/kumtanguliza Mungu basi haukusanyi bali UNATAPANYA yani ni sawa na kuweka katika MFUKO ULIOTIBOKA.
Msingi imara wa kujenga/ kufanya jambo lolote ni kujenga juu ya MWAMBA IMARA ambao ni YESU.
hata dhoruba ikija jambo lilojengwa kwa kuanza na msingi imara YESU halitatikisika/halitatetereka halitabomoka.
Na mtu mwenye akili nyingi na aliyechagua fungu lililo JEMA ni yule tu anayemtanguliza na kumtegemea Mungu wakati wote na muda wote..GOD FIRST(MUNGU KWANZA)mengine yote yafuate NYUMA baadae.
Heri anayemtumikia Mungu kuanzia wakati wa UJANA WAKE mpaka mwisho amechagua fungu lililo JEMA.
Hakuna aliyewahi kumtumikia Mungu halafu BWANA akampungukia akamuacha yeye na uzao wa watoto wake.
Kumtumikia MUNGU sio ujinga ,wala sio kupoteza MUDA ,vijana wanaoimba kwaya kanisani au kuhubiri injili au kufanya kazi za kanisa SIO KWAMBA NI WAJINGA au wanapoteza MUDA au hawafanyi kazi au wanachezea muda wao ,ila nawaonea wivu wamechagua fungu lililo jema ,na hawa NDIO WENYE AKILI..na watauona mkono wa Mungu katika maisha yao na watoto wao..SADAKA WALIYOITOA YA MUDA WAO wa ujana wao katika kumtumikia Mungu.
SIOKWELI kwamba watu WOTE ambao tunapitia hali duni za kiuchumi,hatujajipata kiuchumi,bado tuna jitafuta kimaisha kwamba ETI hatufanyi kazi kwa bidii,ama hatuna akili,ama ni wavuvu ama ni wazembe..la hasha ,WAPO bbaadhi yaa masikini wanafanya kazi kwa bidii,wamesoma kuliko wengine ,wanaomba ajira ,wanajishighulisha na wanamtumikia MUNGU lakini bado WAKATI WA BWANA kuwainua hauhafika...SARA alipata mtoto katika uzee wake ..MUNGU huwa anajibu kwa wakati wake ,hachelewi wala hawai.
Tusijipambanie kwa nguvu zetu wenyewe,ipo njia ionekanayo ni njema machoni pa mwanadamu ila mwisho wake ni mauti,
PIA TUSIJILINGANISHE NA MTU YEYOTE
Utaona mwenzako wa umri rika lako ama mnafanya shughuli moja ama mnapokea mshahara sawa ,ama mnalingana elimu,umri ,n.k..lakini ghafla unaona mwenzako mmeanza pamoja ila yeye ana mafanikio makubwa kuliko wewe,
HUJUI hayo mafanikio ameyapataje...MAISHA SIO MASHINDANO haushindani na yeyote,kila mtu anakusudi lake na ameitwa kutumika kwa nafasi yake na wakati wake na kuna vitu tofauti vipawa na karama tofauti kwa watu tofauti na hata vidole vya mikono yako havilingani.Na kila mtu na kila jambo lina wakati wake.
WAKATI wa Mungu ni sahihi,tuwe na IMANI isiyokuwa na mashaka ,TUMAINI,na UVUMILIVU..na yale matunda ya Roho mtakatifu..tukikosa hivi ndio utaona IBRAHIMU na SARA walipofika ukomo wa uwezo na akili za kibinadamu katika kusubiri kupata mtoto ,wakajipigania wao wenyewe wakaishia kupata mtoto ISHIMAILI ,lakini Mungu alikuwa amewaandalia ISAKA. ukikimbia kwa haraka ,USIHARAKIE MAISHA ,utajikuta hata kazini unachukua RUSHWA,UNAIBA /ufisadi,wizi,unadhulumu unafanya biashara haramu,madili ili UPATE MAFANIKIO YA HARAKA HARAKA..ukijipambania mwenyewe kwa akili za mwanadamu..na hiyo njia hata kama inaonekana ni njema machoni pa wanadamu ila mwisho wake ni MAUTI
.kwa hiyo hata ukichelewa kupata MAFANIKIO kama mtoto kazi,nyumba na gari ndoa,kazi/ajira,mgonjwa umekosa AFYA,n.k
Mungu ATAKUREJESHEA kicheko (Isaka),atakurejeshea wakati /ataukomboa wakati/muda hiyo AFYA iliyougua atakurudishia afya,na miaka iliyoliwa na tunutu,nzige,madumadu.
YOTE KATIKA YOTE
Tumtangulize Mungu kwanza pamoja na mbio zetu za kutafuta mafanikio ,pesa na misha ya hapa duniani ambapo sipo kwetu tunapita,tuwe na kiasi,tufanye yote kwa utukufu wa Mungu.
GOD FIRST..MUNGU KWANZA.