usilale ukiwa kazini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

usilale ukiwa kazini

Discussion in 'International Forum' started by engmtolera, Mar 7, 2011.

 1. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #1
  Mar 7, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Mahakama moja nchini Malaysia imemhukumu kwenda jela miaka mitano mwizi mmoja aliyekutwa kalala katika nyumba aliyovunja kwenda kufanya wizi.
  [​IMG]  Usilale ukiwa 'kazini'..

  Mtandao wa habari wa Canadian press umemkariri mwendesha mashitaka Mohammad Ashraff Diah akisema mwizi huyo alivunja nyumba moja kusini mwa Malaysia wiki iliyopita na kujilaza kitandani na kupitiwa na usingizi fofofo.

  Mwenye nyumba hiyo aliporejea asubuhi alimkuta mwizi huyo bado kalala, na kuamua kuita polisi kabla ya mwizi huyo kuamka. Mwizi huyo alikurupuka baada ya polisi kuwasili, na kujaribu kukimbia. Mwizi huyo alikamatwa na dola kadhaa alizokuwa ameimba katika nyumba hiyo. Mwendehsa mashikata Ashraff amesema juzi Jumatano kuwa mwizi huyo alikiri makosa ya wizi, ingawa hakusema lolote kuhusu suala la kulala..
   
 2. L

  Leornado JF-Expert Member

  #2
  Mar 7, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,534
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Atakuwa aliwekewa mtego na mwenye nyumba, na amenasa.
   
 3. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #3
  Mar 8, 2011
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Labda pia aliiba wiski akanywa kibao
   
 4. m

  mzambia JF-Expert Member

  #4
  Mar 8, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  lazima alikunywa vilevi tu huwezi kulala kazini kwani mwizi amekuwa komba au ngeleja
   
Loading...