Usiku wa Ngugi wa Thiong'o Mjini Dar es Salaam

Usiku wa Ngugi wa Thiong'o Mjini Dar es Salaam

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
22,454
Reaction score
32,980
USIKU WA NGUGI WA THIONG'O ALLIANCE FRANCAISE

Leo wachapaji vitabu mashuhuri Mkuki na Nyota walimwadhimisha nguli wa manguli katika fasihi ya Afrika Ngugi wa Thiong'o katika Ukumbi wa Alliace Francaise.

Kulikuwa na mjadala uliowashirikisha Prof. Penina Mlama, Mkuki Bgoya na Mohamed Said.

Mjadala uliongozwa na kijana mdogo Marc wa Mkuki na Nyota.

Walter Bgoya na Abdilatif Abdalla marafiki wakubwa wa Ngugi walifunua chano kutokea Ujerumani mtandaoni kupitia screen kubwa kila mmoja akieleza vipi alifahamiana na Ngugi na wakatupitisha katika urafiki na udugu wao wa miaka mingi uliodumu hadi walipomuhitimisha rafiki yao.

Ulikuwa usiku wa kumbukumbu kubwa uliohudhuriwa na waandishi chipukizi na watu wengine wapenzi wa fasihi na wasomi wa vitabu.

Mkuki na Nyota walitufanyia hisani kubwa pale walipohitimisha shughuli hii kwa kukizindua kitabu cha Ngugi wa Thiong'o, "Tisa Timilifu," ambacho Ngugi alikiandika kwa Kikikuyu kisha kikatafsiriwa kwa Kiingereza na sasa kwa Kiswahili.

Kitabu hiki ni utenzi.
Mshehereshaji alitusomea Mlango mmoja: "Usiku wa Giza Totoro."

Nikisema nidadavue utenzi huu tutakesha.
Ikutoshe Ngugi anatamba: "Mimi Giza Jeusi Lishindalo Giza Totoro."

Tegua kitendawili hicho ndani ya utenzi huu wa Kikikuyu ukiwa unaweza.
Shughuli ilikuwa mubashara na In Shaa Allah video ikiwa tayari itawekwa mtandaoni.

1749159013273.png

1749159068290.png

1749159171956.png

1749159255197.png
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom