Usiku... Usiku... Usiku!!!

Mtalingolo

JF-Expert Member
Aug 4, 2011
2,181
409
Ukitazama mambo mengi mema kwa maovu, ya busara na yasobusara mengi hufanywa usiku.

STAREHE: Wengi kati ya wapenda starehe hupendelea sana kutoka sehem mbali mbali nyakati za usiku na kukutana kwenye kumbi za starehe na kufanya mambo yao ya starehe.
Matamasha mengi ya kutafuta walimbwende, masupa staa wa muziki au chipukizi, tuzo na medal nying hutolewa nyakati za usiku.
MIPANGO: pia mipango mingi hupangwa nyakati za usiku, iwe ni mipango ya heri au ya shari yote kwa yote hupangwa nyakati za usiku(iliyo mingi).

MASOMO:kwa wale wanaosoma nadhani mnaweza kukubaliana na mimi kuwa wakati mzuri kwa kujisomea(hasa kumeza ma desa) ni usiku hasa kukiwa kumetuli kabisa.

MAOVU: Mengi ya maovu ambayo yamejaa ktk ulimwengu wetu wa sasa hufanyika nyakati za usiku na ndiomaana ni rahisi sana kuskia mchawi kakutwa kanaswa sehemu fulani alfajiri, manaake alikuwa akiwanga usiku...

MAOMBI(kusali): kwa baadhi ya dini kama sio zote(sina uhakika) huamka nyakati za usiku na kusali/kuomba kwa imani zao(visimamo vya usiku).

PRODUCTION: hapa nazungumzia ktk kila idara ya uzalishaji, nyingi hufanyika nyakati za usiku, tukiangalia uumbaji wa mwanadamu hufanywa wakati wa usiku kwa walio wengi, ukienda nchi za wenzetu hufanya shughuli za uzalishaji nyakati za usiku...

Mengi hufanywa nyakati za usiku, naweza kuwa cjataja yote, hebu 2changie mawazo juu ya mambo tuyajuayo yanayofanyika sana nyakati za usiku na faida au madhara yake pia mtupatie..

Nawasilisha...
 
uumbaji wa binadamu ndo shughuli muhimu zaidi ambayo hufanyika usiku
zingine ni vyai tu.
 
Back
Top Bottom